Hakuna Rais aliyemfikia JaKaya kwa idadi za kilometa za lami alizojenga. Kikwete alitengeneza barabara ndefu zenye kilometa nyingi kuunganisha mikoa Tanzania. JPm alitengeneza barabara za kilometa moja au mbili za halmashauri/mitaa Hilo halipingiki. Na alimwachia miradi au mipango iliyomrahisishia Jpm kukamilisha hiyo miradi
Kama mnavunja jiwe, mpo watano, wa kwanza akapiga weeeee akachoka, akaja wa pili akapiga weeee akachoka, wa tatu naye akapiga weee akachoka, wa nne akapigaaa kukatokea na krek ila akachoka wa tano akapiga mara moja likavunjika swali ni Je wa tano ana nguvu sana? Au nyundo za wa kwanza hadi wa nne zina mchango?
JPM kafanya mambo mazuri, ila ni UPUMBAVU sana kutenganisha mazuri yake na awamu zilizopita.
Anayesifia kwa kuponda waliopita ni MPUUZI, JINGA JINGA ZEZETA LISILO NA MAANA YOYOTE.
Angevunja na jeshi, na utumishi wasitumike hao waliofundishwa na kupewa training na awamu zilizopita afundishe wa kwake ili apewe sifa za kipekee.
Kama alirithi maendeleo basi apewe sifa ya kuendeleza walipoishia wenzake na si kusifiwa kama vile hakujawahi kuwa na maendeleo kabla yake.
HALAFU MAENDELEO YA NCHI SI LAMI NA MADARAJA TU, HATA KUHAKIKISHA KUWA NCHI NI SALAMA NA WATU WANAFANYA BIASHARA ZAO BILA KUKIMBIA NCHI NI MAENDELEO.