Mimi sina shaka na utendaji wa waziri Magufuli au Raisi Magufuli.
Tunatambua mchango wake kwa kusimamia miradi mbalimbali.
Lakini tusibweteke na misifa,kwani wapo waliofanya makubwa na mambo mazito kuliko Mjomba Magu.
1.Hakuna Raisi alimimina viwanda kama Raisi Nyerere. Tena sio viwanda mandazi viwanda vingine heavy vyakuajiri hadi watu zaidi 10,000.Alijenga viwanda heavy industries zaidi ya 400.
2.Raisi Nyerere alijenga reli ya TAZARA chini ya miaka 5,harafu akajenga karakana kubwa kuliko karakana yoyote Sub-Saharan iliokuwa inaitwa Mangula Mechanical Tools(MMT)
3.Wakati wa Nyerere alijenga Refinery Kigamboni iliokuwa inaitwa TIPER
4.Raisi Nyerere alijenga mabwawa ya kuzalisha umeme ambayo ni Kidatu,Mtera na Kihansi pia na Nyumba ya Mungu.
5.Raisi Nyerere alijua dhana ya kujitegemea akajenga kiwanda kikubwa cha zana za kilimo kilichokuwa Ubungo UFI
6.Raisi Nyerere alijenga kiwanda kikubwa cha kuzalisha mbolea huko Tanga .
7.Ilipovunjika shirikisho la Afrika Mashariki Raisi Nyerere alianzisha shirika la ndege la taifa Air Tanzania ATC,alinunua ndege 8 kwa mpigo zikiwemo Boeing 737 ndege 2,Folker Friendship 2,Twin Otter n.k
8.Raisi Nyerere alijenga viwanda vikubwa vya kubangulia korosho zaidi ya vitano ukanda wa pwani.
9.Raisi Nyerere kama baba mpigania uhuru nchi mbali mbali.Alifanya Tanzania ikawa donor country wa kuzikomboa sio wa maneno tu, nchi nyingi haswa kusini mwa Afrika ikiwemo South Africa, Mozambique, Angola, Zimbabwe,Namibia, Guinea Bissau.
10.Huko maziwa ya Victoria alijenga meli mpya na cheleo, meli za abiria na mizigo kama MV,Bukoba,Butiama,Serengeti.n.k
Pia Alifufua Meli ya abiria Liemba,akajenga meli ya mafuta Sangara meli ya abiria Mwengozo