Kwanini Mkuu wa Majeshi hapewi heshima?

Zipo kombati za aina nyingi mkuu hii nikutokana na eneo mnalokwenda so kama ni jangwani mtavaa kombati zinazolandana na eneo huwa tunaziita MSADAMU
nikweli hata mimi nimetoa mfano tuu wa vazi la vita ya jangwani, ila vazi hutegemea na mazingira ya vita (bado tupo pamoja)
 
Kwanza naomba nikukosoe ninavyojua mimi mwanajeshi haitaji ulinzi au msafara maana yeye ndo mkuu wa ulinzi. Na katika msafara wake wa kwenda ofisini mkuu wa majeshi gari lake lenye nyota nne linakuwa mbele na La MP linakuwa nyuma mpaka atakapofika ofisini mbele ya gari lake panakuwa na pikipiki ya traffic ya kumuepusha na foleni. Kama nimekosea naomba nikosolewe.
 
Cha pili kaka inaelekea haujaenda jeshini hawataki mtu anaefanya kazi kwa ajili ya kupewa sifa. Je aiku hizo sifa zisipokuwepo ? Nchi si itapinduliwa wanaangalia nidhamu binafsi na nidhamu kwa Amiri Mkuu
 
...kama ndio ivo kwa nn kwenye sherehe za uhuru CDF ndio anakuwa benet na Prezdaa na siyo IGP?
 
Nimesema CCM kama chama sio mtu.Kumbuka kuna Jamaa hapo juu alisema kuhusu wanajeshi ambao wana nguvu kuliko askari elfu wa CCM.Sasa nikataka kujua kama kuna Jeshi tanzania hii ambalo lina uwezo wa kukataa amri ya CCM.NIPO TAYARI KUREKEBISHWA.
Kwani ccm ni MTU!?
 
Umejitahidi sana kuonesha ukuu wa police kwa jwtz, safi sana maana polisi kwa sifa hukawii kusema IGP NI MKUU WA CDF
 
...kama ndio ivo kwa nn kwenye sherehe za uhuru CDF ndio anakuwa benet na Prezdaa na siyo IGP?
Sababu sherehe zile zimeandaliwa na jwtz.yule ndiye mwenyeji wa sherehe zile uwanjani pale.
 
Bonge la point
 
Ngoja nivitafute hizi sheria nisome halafu nitarudi
 
Umejitahidi sana kuonesha ukuu wa police kwa jwtz, safi sana maana polisi kwa sifa hukawii kusema IGP NI MKUU WA CDF
na hata hivyo polisi ndiyo wahusika wakuu wa usalama wa ndani, na kwa mfumo wa vyombo vyetu IGP anawajibika kwa Rais moja kwa moja na si mtu mwingine yeyote yule.Sanasana polisi waache tabia ya kuchukua virushwa rushwa kutoka kwa watu maskini maana hivyo ndivyo vinavyo washushia heshima kwenye jamii. polisi mnamamlaka makubwaa sanaa ambayo hata mtu kama MKURUGENZI, MEYA, DIWANI, MBUNGE, hana hivyo msijitie aibu, nyie ni watu wakubwaa sana kwenye jamii mnao paswa kuonesha njia za unyoofu, sanasana toeni maoni kwa viongozi wenu (ingawa ni ngumu kwa mifumo yenu) iliwapiganie masilahi yenu ya halali ya boreshwe ili mfanye kazi bila hofu ya njaa ya maisha.

kwa mamlaka makubwa na adhimu waliyopewa polisi na sheria zetu, kama polisi wange kuwa wa adirifu basi kusinge kuwa na haja ya kupoteza pesa kwa kuunda vyombo vingivingi mfano Takukuru, kwani polisi wanasimamia msaafu wote wa makosa ya jinai hapa ncnini, sasa rushwa si jinai? ni kwamba polisi waache kuji tia aibu kwa virushwa rushwa, iliwaweze tekeleza majukumu yao kwa ufasaha na jamii iweze pata imani na chombo hiki.

pamoja na mamlaka makubwa waliyo pewa na sheria bado jeshi la polisi la hitaji kufumuliwa lote kwani inaonekana mifumo kandamizi na mifumo ya rushwa imeota sugu ndani ya jeshi hili, hata utoaji wa vyeo vyao bado niwa kiupendeleo na rushwarushwa tuu, Askari wa jeshi hili wamesha lalamikia hili kwa muda mrefu kwenye vyombo vya habari (MAGAZETI) . hii itasaidia kuboresha utendaji, shule yeyote huitaji viranja basi hata jamii yahitaji viranja na kimsingi 'POLISI NI VIRANJA WA JAMII', "SOCIAL ORDER DEPENDS ON YOU POLICE OFFICERS"

Elimu za vijana wanao chukuliwa kuwa wanajeshi wa jeshi hili la polisi pia ziangaliwe, serikali iboreshe mishahara kisha isimamie kikamilifu ili polisi wafanye kazi kwa uadirifu bila rushwa wala upendeleo, (mtu yeyote aliye na hatia basi akamatwe na kufikishwa mahakamani na upelelezi ukamilishwe kwa haraka na kwa usahihi ili haki itendeke)
 
Haha KWA class pengine elimunilionayo kuanzia babampaka wajomba zako wanaweza wasinikaribie huko ntakuaibisha
hata maji marefu ni prof.....
unajisifia na elimu ya TZ mkuu.....
weee kaa huko huko bongo af wenzio wanabeba box ulaya wanatokaaaa............
msomi hawez kuwa CCM ever
 
Bonge la point
Una uhakika na hiyo paragraph ya katikati hasa kwenye maneno yenye mstari??????????
 
Mko sahihi wakuu, lakini kitu kimoja tu ni kuwa Mkuu was UWT anariport moja kwa moja kwa raisi na siyo kwa CDF kama mlivyoelezea, na ndio maana uWT wana watu wao jeshini.

Nakubaliana na wewe mkurugenzi huwa na direct line .....lakini kimfumo CDF ndie joint chief ....wa ulinzi na usalama .......hata hawa IGP, CGP ...huwa na direct line kwa President kwenye baadhi ya mambo
Na Mara nyingi imetokea viongozi wa kisiasa ..Mawaziri wanaopelekwa pale Mambo ya Ndani au Ulinzi inatokea ambao wanakuwa hawajui mipaka wakifikiri hawa wakuu wanatakiwa kuripoti Kwao Kilapilo Kitu....na inafikia baadhi ya Mawaziri hadi wanatoa maagizo ya kufukuza kazi Askari hadharani.....wanakuwa wanavuka mipaka kwakuwa haya majeshi yana mifumo na taratibu....waziri Kama hajapendezwa na jambo inatakiwa amuambie IGP ,CGF,CGP,CGI.....
Tatizo Kama Hilo ndio lilimuondoa Shamsi wizara ya ulinzi ....na pia mambo ya Ndani ...alifikiri kwakuwa alipata kuwa Waziri Kiongozi basi anaweza kuwa arrogant kwa maafisa waandamizi....Kama uraiaani akasahau kuwa kwenye hizi taasisi waziri yupo ceremonial tu lakini boss ni Amiri Jeshi Mkuu.
 
Una uhakika na hiyo paragraph ya katikati hasa kwenye maneno yenye mstari??????????
[emoji1] [emoji1] mkuu kuna vitu humu ukisoma unabaki kucheka tu.

Na kupita tu huku umeongeza siku ya kuishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…