Kwanini Mo 'hatamuweza'Manara

Wewe unaumia nini kwa utapeli wa Mo pale Simba?
Mafanikio ya muda mfupi yasiwafumbe macho, mlumbuke pia hela sio kitu pekee kinacholeta mafanikio kwenye team, kuna hitajika vitu vingine pia.Kuna tena huko Duniani zia hela ila mpaka leo Zina miaka mingi bila makombe.

Kwa hilo la Manara,kila shabiki wa Simba Sc anaejitambua atakuwa amepata picha ya kinachoendelea pale.
 
Bila huyo tapeli Simba ingekua hapo ilipo?
Shida sio Simba ulipo, shida ni kutaka kujifanya Simba Sc kama kampuni lake.

Kwahiyo kumbe hatutakiwi kujadili kinachoendelea simba kwasababu ya nafasi iliyopo? Vipi siku ikishuka hapo ilipo? Au unadhani pesa pekee ndio imefanya Simba Sc iwe hapo? Kama unafikiria hivyo juilize kwanini AZAM FC hawako hapo.
 
Sawa, MO siku mbili hizi anatangaza kuachana na Simba, huyo Albino hawe yeye Sasa mfadhili wa Simba yeye na ukoo wake, si mnasema MO anajinufaisha yeye club hainufaiki,Sasa anaondoka hili Simba hifanye vizuri zaidi
 
Utopolo mumepata kichaka cha kujifariji baada ya kuukosa ubingwa kwa miaka minne hii na inaelekea mtaendelea kuteseka kwani msimu ujao tunabeba makombe yote kama kawaida yetu.
 
Utopolo ni wahanga wakubwa wa uwekezaji wa Mo Simba. Msimu ujao tunabeba makombe yote kama kawaida yetu,endelezeni majungu tu na usajili wenu wa hao wacheza ndombolo mliowaokota kwa bei che. Simba Nguvu Moja
Bilashaka wewe siyo mdau wa mpira .Wanaojua mpira wanajua kwamba si rahisi kihivyo.Muda utasema hata zile mechi ambazo Simba anacheza na Yanga mlikuwa mnasema lazima mtashinda tena kwa goli nyingi kilichokuwa kinawakuta unakifahamu mpaka mnapoteana na kulaumiana subiri mechi ya Tarehe 25/9 ,mkipigwa kipigo Cha mbwa mwizi huo mvurugano wake utakuwa zaidi ya huo wa Sasa wa vigoli kimoja kimoja mpaka Hindi janja alitishia kujiudhuru na kuacha timu.Tusubiri muda utasema
 
Hayo mingine yanaweza kuwa sawa lakini la kigwa linajulikana wazi alinyimwa mkopo wa bodaboda
 
Kwani mo anapvana na manara?
 
MO ni Mpole na Mnyenyekevu hapendi kujikweza wala kugombana na watu.

Manara yupo juu sana, mtoto wa Mjini Daresalama, Mtaa wa Kariakoo. Mjanja wa Mjini.

MO ana Moyo Imara sana la sivyo angeshajitoa kudhamini Simba.
Kila kukicha anakutana na Kejeri, dhihaka, matusi, kashfa humu mtandaoni.

Kisa Kaidhamini Simba, tena kwa kupewa Baraka zote na Wanachama wa Simba na Serikali.
Na mafanikio yanaonekana kwa timu za Simba Wanaume na Simba Wanawake.

Wadhamini wa timu nyingine hawaguswi kabisa. Wao ni Waheshimiwa.

Wakati tutaongea.
 
Ni mimi sana huyu Mudy
 
Umenichekesha 🤣🤣🤣 watz ni wazee wa tupo pamoja, sasa usiombe upate janga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…