Kwanini mpaka sasa sipati ukimwi?

Kwanini mpaka sasa sipati ukimwi?

Nimewahi kusikia kuwa Mwathirika anayetumia dawa za kufubaza Virus (ARV) kwa usahihi yuko kwenye nafasi ndogo sana ya kuambukiza wengine.

Kwa maana zile dawa hupunguza kwa kiasi kikubwa wingi Wa Virusi kwenye Damu ya Muathirika.

Wataalamu watafafanua zaidi.

Wanasemaga kirusi hafi ile dawa inapunguzaje wingi wa virus?
 
ASANTE kwa mchango wako ndugu yangu acha tusubiri wataalam waje waseme kitu mwisho wa siku tujifunze mimi na wew na wengineo,lakini je haya magroup ya damu ukitaka kujua kama uko group gani na taarifa za group lako hospitali kuna vipimo vya kujua group lako na taarifa zake?kama vipo garama za vipimo hivo zikoje kama unafahamu Twilumba.
Vipimo vya kutambua blood group vipo ila sina uhakika wa gharama, ni vzr sana kujua blood groups yako na ya watu wako wa karibu, kuna dharura zinaweza tokea zikawa solved early!
 
HIV ya mkeo ni tofauti kidogo. HIV yake kazaliwa nayo maana yake hivyo Virus vya HIV kaweza kuvizibiti Afya yake ipo njema. Kitu cha muhim asipate maambukizi mengi kutoka kwa Mtu Mwingine hapo tatizo litaanza
 
Nisikitika sana mpaka leo Hatujui kisa kidogo kama chako. Wasomi na wanasayansi wetu wanasubiri kuteuliwa tu. HIV na Malaria tumewaachia wazungu waumize vichwa, walete majibu za tafiti zao na tiba pia. Swala lako kama ni kweli basi, tungekuona ukitumika katika tafiti. Ngoja tumwachie MUNGU NI MWEZA WA YOTE. Ujanja ni kuchanjwa corona ipo. Umechanja lakini?
Kiranga naomba utie neno hapa maana jamaa anakuchokoza huyu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
[emoji23][emoji23][emoji23]scan reading unaijua, wewe title tu inatosha kuliko kujichosha na long paragraphs, hafu kwanini wewe usi comment unachokijua Sasa mfyuuu
Sio lazima nicoment, Kama naona wajumbe wameseme nliyotaka kusema nanyamaza tu!! Afu inaonekana una kihere here na heshima yako Ni ndogo kwa mume wako
 
Kiongozi hapo umeonyesha kabisa kuwa muathirika anatumia dawa kwa hiyo hapo nadhani wewe kiongozi elimu ya huu ugonjwa kuna sehemu hujaielewa.Kinashokukinga wewe kutopata ugonjwa ni mke wako kutumia dawa kikamilifu. Sikushauri ufanye hili ila unaweza ku test zali kwa kumwambia aache kutumia dawa kisha uendelee kupiga show bila kinga,utakuja kutupa mrejesho hapa fasta.
Mkuu jamaa amekuja kujua kama mkewe ni mwathrika inawezekana kipindi Cha ujauzito Cha Mke wake baada ya kumuoa ila inawezekana ata kabla ya ndoa jamaa alikuwa anaendelea kufanya nae mapenzi bila kondomu

Kumbuka kuwa Mke wake pia alikuwa hajui kama ameathirika na dawa ameanza kutumia kipindi ambacho amegundulika ni mwathrika, I bet ndo hicho kipindi cha ujauzito, inaonekana jamaa alikuwa ana sex nae kabla ata hajaanza kupata dawa na hakupata maambukizi

kwahiyo hoja yako ya kusema Mke wake aache kutumia dawa Kisha jamaa aendelee na zoezi sex kutakuwa na tofauti gani na mwanzo kipindi ambacho Mke wake alikuwa hatumii dawa na jamaa hakupata maambukizi
 
Hongera sana mzehe

Ushauri wangu, wale wa translate kazi kwenu "kumesikika siku za hapo nyuma ni kwamba, dawa ya kupunguza makali ya vvu inatolewa soon, dawa hiyo itakuwa unapatiwa kila baada ya 6month's kama ckosei, sasa naomba muwasilishe ujumbe huu "hatutaki hiyo dawa, ngono zitarindima"
 
Mtu mwenye Virusi vya Ukimwi (VVU) anakuwa na uwezekano mdogo wa kuambukiza iwapo atakuwa anatumia dawa za kufubaza makali ya virusi (ARVs) vizuri na kwa muda mrefu.

Matumizi mazuri ya dawa hupelekea vizuri hata virusi kutoonekana katika vipimo (undetectable level)...

Nadhani hii ndo itakuwa sababu ya wewe kutoambukizwa.
Kutokana na maelezo ya mtoa mada ni kwamba alikuja kugundua kuwa mkewe ni mwathrika baada ya miezi kupita na inawezekana ilikuwa ni kipindi Cha ujauzito Cha mkewe

ila kabla ya hapo ata huyo mkewe alikuwa hajui kama nayeye ni mwathrika kwahiyo jamaa hicho kipindi chote ye alikuwa anafanya sex na mwathrika ambae hatumii dawa

Kwahiyo hapo sababu ya yeye kutokupata maambukizi haiwezi ikawa ni matumizi ya ARV Kwa Mke wake, tucheki sababu ingine kama ipo mkuu
 
Ukichunguza ukimwi ni laana so kwanini upati umetulia kama ishara ya toba.Ila ukitaka ukupate mnyanyapae au msaliti mkeo hakika utapata na hata watoto watakuja kupata .
 
Hata dawa wanazotumia sio dawa za kuua virus, na ukimwi wenyewe pia sio ugonjwa! Ni upungufu tu wa kinga mwilini.
Na pia mtu hafi kwa ukimwi bali kwa magojwa nyemelezi!

Kiufupi hakuna ugonjwa unaitwa ukimwi!

Pep Guardiola anapigana round ngapi na Antony Joshua,wakati tunapiga kura Rungwe awe spika wa bunge la Marekani.
 
Habari zenu

Ndugu zangu msichanganywe na kichwa cha habari na mkaja kunitusi na kunijibu ovyo,sio kwamba nataka nipate.Bali nataka Wataalam na wajuzi waje watupe elimu itakayotupatia faida mimi na nyinyi

Wengi tunaamini kwamba ngono ndio chanzo kikubwa cha maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi,hata katika kampeni mbalimbali tunahimizwa kuacha ngono zembe na tutumie kinga ili kujikinga na maradhi haya.

Sasa ni miaka mingi sana tangu nimuoe mke mwenye virusi vya ukimwi na sikuwahi kutumia kinga mpaka siku nilipojua kuwa ni muathirika imeshapita miezi mingi nikaenda kupima nikaambiwa niko salama nikapewa na kondom nakumbuka niliitumia siku moja tu na nikasema kwa roho safi kuwa liwalo na liwe kupata kutokupata yote ni sawa sote tutakufa na sinaga kabisa hofu wala kuwaza hata sikujali tena hiyo issue ili kumpa amani ya roho maana alishapatwa na mshtuko hata yeye hakutegemea kwan alikuwa ni mdogo na alizaliwa nao ni mama yake ndio alikuwa anaficha ukweli

Nikaishi nae yafika mwaka wa sita sasa na Mungu ametujaalia watoto wa kiume wawili ambao wao wako salama kwa kuwa nafuata taratibu zote za kidaktari juu ya watoto wanaozaliwa na mama mwenye HIV.

Huwa nasex nae kavukavu,wakat mwingine showshow za kufa mtu,kimaumbile niko vizuri,wakat mwingine michubuko na vidonda wakat wa sex na michubuano hutokea mara kwa mara kutokana show za vurugu zinazotokea.

Lakini sasa ni mwaka wa sita au watano leo nimempeleka akachukue dawa nikapima majibu yanakuja bado niko salama

Sasa najiuliza hivi kuna uwezekano gani miaka yote hiyo bado nisipate ukimwi,kwanini sipati ama ngono sio sababu kuu ya kupata ukimwi ama kuna vitu vingine vinachangia ama inakuwaje kuwaje hii hali.

Tukumbuke kuwa hata nikipata mimi sijali nafsi yangu ilishakunjua kiroho safi na siogop wala sina hofu yani naishi tu safi tu najua kufa kupo haijalishi NITAKUFAJE.

Wataalam,wajuzi na madakatari hebu mkuje kidogo mnieleze kitu kuhusu hili,huenda wengine wakapat elimu na kufaidika pia.

Matusi na kebehi si vyema wandugu ni bora upite tu pia nisieleweke vibaya kwenye bandiko langu hili kwani ni kweli ukimwi upo na unaua na hata nami nimeshuhudia.

Nawasilisha
Kama anatumia ARV, kishapoteza uwezo wa kuambukiza ukimwi huyo mkeo,
Au wewe ni hivyo virus havikuathiri,, chukulia case yako mfano wa watu wengine kutopata covid 19,hata akikoholewa na mgonjwa wa covid,,
Watu wengine ni resistant kwa haya magonjwa ya virus

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Swala sio wewe kupata virus ishu iko hvi. Huenda mwenza wako ana viral load <50cell/mm mtu hyo chance ya kuambukiza ni ndogo mnoo na hususani watu wanao tumia dawa ipasavyo i mean daily ..acha hao wanaona ruka ruka chance ya kuambkiza mtu hua ni ndogo .. ishu nyingne kuna jamii ya watu kweny cell zao hakna cell receptors ambapo ndio zinaruhusu viral kuji attach kweny wbc apate kuweka RNA zake (material)
 
Kiranga naomba utie neno hapa maana jamaa anakuchokoza huyu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hajafafanua hiyo sehemu aliyoandika Mungu muweza yote ni neno la imani au fact.

Kama ni imani, sina tatizo naye. Anatumia haki yake ya kikatiba kuamini anachotaka.

Kama anaandika factually, ana wajibu wa kuthibitisha kwamba alichoandika ni kitu cha kweli na hapotoshi jamii.
 
Hajafafanua hiyo sehemu aliyoandika Mungu muweza yote ni neno la imani au fact.

Kama ni imani, sina tatizo naye. Anatumia haki yake ya kikatiba kuamini anachotaka.

Kama anaandika factually, ana wajibu wa kuthibitisha kwamba alichoandika ni kitu cha kweli na hapotoshi jamii.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Kikusya toa neno hapa [emoji115][emoji115][emoji115]
 
Back
Top Bottom