Kwanini mtaani kuna dhana mbaya kuhusu ndugu?

Selemani Sele

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2023
Posts
319
Reaction score
711
Utasikia;

1. Usikae na ndugu yako ni shida
2. Usiajiri ndugu utakuja kulia
3. Ndugu ni wa kukaa nao mbali na nyingine nyingi

Nafikiri umoja kwa familia na undugu wa damu ndio msingi mkubwa wa maendeleo ya jamii zetu. Tusitegemee kupata maendeleo kama taifa endapo jamii hasa ndugu hawawezi kushirikiana kwenye uzalishaji mali na kazi, hili ni tatizo kubwa sana.

Hebu tutoe maoni huku tukiangalia mifano ya biblia; Kaini na Abeli, Yacobo na Esao, Daudi na ndugu zake, Yusuph na ndugu zake, Isaka na Ishmail, Israel na Palestine.
 
Siwezi thubutu kukaa na ndugu nina experience na matukio yao ingawa sitaki kuyasema hapa
 
me nimetoka kutimua nipo mwenyewe kwenye kaofisi changu wiki sasa.
-wavivu
-hawapendi kusemwa
-hawajiongezi mpaka uwaamrishe.
-wanachukulia vitu kawaida
-sio waaminifu
-wanapenda uwalipe zaidi mbali na makubaliano pale unapopata hawajui kuwa wewe ndo faida yako.
-hawajali mda wanaleta mazoea ya udugu.
- siri zako nyingi zinafika kwa ndugu.

japo kuna wengine wametulia ila wachache.
 
Utasikia;

1. Usikae na ndugu yako ni shida
2. Usiajiri ndugu utakuja kulia
3. Ndugu ni wa kukaa nao mbali na nyingine nyingi

Nafikiri umoja kwa familia na undugu wa damu ndio msingi mkubwa wa maendeleo ya jamii zetu. Tusitegemee kupata maendeleo kama taifa endapo jamii hasa ndugu hawawezi kushirikiana kwenye uzalishaji mali na kazi, hili ni tatizo kubwa sana.

Hebu tutoe maoni huku tukiangalia mifano ya biblia; Kaini na Abeli, Yacobo na Esao, Daudi na ndugu zake, Yusuph na ndugu zake, Isaka na Ishmail, Israel na Palestine.
Huu mwaka wa 20 mzee anajuta kuajiri ndugu ni wavivu
Kumbe majibu unayo.
 
Ujamaa una faida kama ndugu wanapenda kujituma, ila fanya kwa moyo usitegemee malipo na shukrani, zikija sawa ila zisipokuja hewala

mara nyingi tunafanya wema ili tuweze kusaidia ili wao wafike mahali salama ukoo uendelee kuwa imara

hamna kitu kinachosikitisha kama kuwa na ndugu viazi, unakuta jitu halipendi kusoma, kazi halitaki, kazi kutembeza rungu, ukimleta nyumbani anatembeza ukuni kuanzia kwa mahausigeli hadi vibinti vya mtaani basi vurumai tu

kibinti nacho utakuta hakitulii, kinagawa utamu mpaka basi ila kujiongeza walau afanye biashara unakuta hola, inaumiza sana.

Huwa nasoma historia za wenzetu unakuta wana Ukoo wenye nguvu kila mmoja kajipata na wana biashara za maana,

huwa nasikitika sana nikiangalia na kwetu waliopo hata tukijitahidi kunyanyuana unakuta watu wanajirudisha nyuma wenyewe
 
Waafrika wengi wana uwezo mdogo wa kufikiri na uaminifu ni 0%. Nina mtu nimefahamiana naye mitandaoni tu anaishi canada amewekeza tanzania ana nyumba kibao za kupangisha na mimi ndio nasimamia miradi yake yote hata ndugu zake hawajui maana walishamfelisha wayback na sasa ndugu yao kawekeza africa na anayesimamia ni mtu baki hatukuwahi kujuana kabla.
 
The great Professor Yesu alishaliongelea hili.
Screenshot_20240108-102942.jpg
 
Utasikia;

1. Usikae na ndugu yako ni shida
2. Usiajiri ndugu utakuja kulia
3. Ndugu ni wa kukaa nao mbali na nyingine nyingi

Nafikiri umoja kwa familia na undugu wa damu ndio msingi mkubwa wa maendeleo ya jamii zetu. Tusitegemee kupata maendeleo kama taifa endapo jamii hasa ndugu hawawezi kushirikiana kwenye uzalishaji mali na kazi, hili ni tatizo kubwa sana.

Hebu tutoe maoni huku tukiangalia mifano ya biblia; Kaini na Abeli, Yacobo na Esao, Daudi na ndugu zake, Yusuph na ndugu zake, Isaka na Ishmail, Israel na Palestine.
Ndugu ni lawama sana badala ya kuleta ufanisi katika kazi basi wanatumia kigezo cha undugu kufanya kazi ambapo matokeo yake ni mabaya sana
 
Utasikia;

1. Usikae na ndugu yako ni shida
2. Usiajiri ndugu utakuja kulia
3. Ndugu ni wa kukaa nao mbali na nyingine nyingi

Nafikiri umoja kwa familia na undugu wa damu ndio msingi mkubwa wa maendeleo ya jamii zetu. Tusitegemee kupata maendeleo kama taifa endapo jamii hasa ndugu hawawezi kushirikiana kwenye uzalishaji mali na kazi, hili ni tatizo kubwa sana.

Hebu tutoe maoni huku tukiangalia mifano ya biblia; Kaini na Abeli, Yacobo na Esao, Daudi na ndugu zake, Yusuph na ndugu zake, Isaka na Ishmail, Israel na Palestine.
Labda wa kuzaliwa tumbo Moja, sio mbaya
 
Waafrika wengi wana uwezo mdogo wa kufikiri na uaminifu ni 0%. Nina mtu nimefahamiana naye mitandaoni tu anaishi canada amewekeza tanzania ana nyumba kibao za kupangisha na mimi ndio nasimamia miradi yake yote hata ndugu zake hawajui maana walishamfelisha wayback na sasa ndugu yao kawekeza africa na anayesimamia ni mtu baki hatukuwahi kujuana kabla.
Imagine 🤷
Mungu akubariki aisee Kwa huo uaminifu
 
Waafrika wengi wana uwezo mdogo wa kufikiri na uaminifu ni 0%. Nina mtu nimefahamiana naye mitandaoni tu anaishi canada amewekeza tanzania ana nyumba kibao za kupangisha na mimi ndio nasimamia miradi yake yote hata ndugu zake hawajui maana walishamfelisha wayback na sasa ndugu yao kawekeza africa na anayesimamia ni mtu baki hatukuwahi kujuana kabla.
Hilo nalo ni tatizo sana maana kuna uwezekano mkubwa wa uaminifu huo kupotea kwa muda mfupi tu....Nina experience na Hilo jambo yupo jamaa amekosa nyumba kabisa kumwamini mtu baki bila ndugu kujua
 
Back
Top Bottom