Je umewahi kujiuliza kwanini hujawahi kuanguka chini sakafuni kutoka kitandani ? Hata kama ungekuwa una usingizi mzito kiasi gani ikifika wakati wa kujigeuza unageuka tu!!
Jibu hili hapa!!
Binadamu haanguki kitandani akijigeuza kwa sababu ubongo hauzimi kabisa. Mfumo wa ndani wa proprioception unasaidia ubongo kutambua nafasi ya mwili na mipaka ya kitanda kupitia shinikizo la godoro. Ukikaribia ukingoni, ubongo unatambua hatari na kukugeuza upande salama bila wewe kuamka.
Pia, wakati wa ndoto nzito, ubongo hupooza misuli kwa muda (REM atonia) ili kukuzuia usiruse viungo na kuanguka. Hii ni tabia ambayo ubongo wa mtu mzima umejifunza na kuikariri tangu utotoni, tofauti na watoto wadogo ambao mifumo yao bado haijakomaa na huanguka mara kwa mara.