Kwanini mtu mzima akilala hawezi kuanguka kitandani anapojigeuza

Kwanini mtu mzima akilala hawezi kuanguka kitandani anapojigeuza

Kontena lile jeupe karibu na school chapel 😊...

Ila nasikia siku hizi skonga yote ipo ndani ya ukuta, sisi wazee wa kitei cha mama Tony tungepata shida sanaaa...
Hahahaa ukienda unapotea kabisa ,full fensi 😛 😛
 
Duh! sawa mkuu. halafu kuna zile ndoto za kukojoa kitandani labda mpo mnacheza mpira ukaenda kukojoa pembeni ya uwanja, yani unaanza kukojoa vizuri tu ile unamalizia kupush mkojo ndo unashituka kumbe uko kitandani hii imekaaje mkuu!
Kibofu kikijaa kweli, ubongo unatengeneza ndoto yenye mazingira salama (kama uwanjani) kuhalalisha ukweli huo. Ubongo unaruhusu misuli kulegea, mkojo unatoka kitandani. Unamalizia kusukuma, baridi ya mkojo kwenye ngozi inalipua mifumo ya dharura ya ubongo na kukushtua ukiwa umeshachelewa
 
Mimi nimeanguka sana asee. Na Kuna wakati nilikuwa natembea Hadi naenda kuoga bwawani usiku ndo naamka sasa nikikanyaga maji nachomola mbio nikidhani nilichukuliwa na wachawi! Kwa sasa Nina muda mrefu sana sijaanguka tena yaani toka nioe sijawahi anguka tena kitandani hata kama nimelala mwenyewe.
 
Hongera kwa ndoa yako na kupona changamoto hiyo! Tabia ya kutembea na kwenda kuoga bwawani usingizini (somnambulism) huku ukidhani ni wachawi ilitokana na ubongo wako kushindwa kupooza misuli, ukachanganya ndoto na uhalisia.

Kukoma kwa tatizo hilo baada ya kuoa kunatokana na sababu kuu mbili: 1.Baada ya kubaleghe na kuingia utu uzima, mifumo ya neva inayolinda usingizi inakomaa na kuimarika.

2.Ndoa na utulivu wa maisha hupunguza msongo wa mawazo, ambao ndio kichocheo kikuu cha kutembea usingizini.
 
Kibofu kikijaa kweli, ubongo unatengeneza ndoto yenye mazingira salama (kama uwanjani) kuhalalisha ukweli huo. Ubongo unaruhusu misuli kulegea, mkojo unatoka kitandani. Unamalizia kusukuma, baridi ya mkojo kwenye ngozi inalipua mifumo ya dharura ya ubongo na kukushtua ukiwa umeshachelewa
Duh! inasikitisha sana. yana haya maelezo ukimpa mother hatahakuelewi yani kila ukikojoa tu asubuhi yake unakutana na kipigo kimoja makini, hadi imesha niharibu kisaikolojia.
 
Duh! inasikitisha sana. yana haya maelezo ukimpa mother hatahakuelewi yani kila ukikojoa tu asubuhi yake unakutana na kipigo kimoja makini, hadi imesha niharibu kisaikolojia.
Kwani una umri gani wewe kwa sasa? Je bado mama mzazi ana manage privacy yako kama mahali unapolala na unachovaa?
 
Stuxnet mjuba vp ile hali hujaota unajamiiana ila unakuta umepiga bao au unastuka haraka unakuta ilikuwa kidogo uchafue mazingira imekaaje kitaalamu
 
Je umewahi kujiuliza kwanini hujawahi kuanguka chini sakafuni kutoka kitandani ? Hata kama ungekuwa una usingizi mzito kiasi gani ikifika wakati wa kujigeuza unageuka tu!!

Jibu hili hapa!!

Binadamu haanguki kitandani akijigeuza kwa sababu ubongo hauzimi kabisa. Mfumo wa ndani wa proprioception unasaidia ubongo kutambua nafasi ya mwili na mipaka ya kitanda kupitia shinikizo la godoro. Ukikaribia ukingoni, ubongo unatambua hatari na kukugeuza upande salama bila wewe kuamka.

Pia, wakati wa ndoto nzito, ubongo hupooza misuli kwa muda (REM atonia) ili kukuzuia usiruse viungo na kuanguka. Hii ni tabia ambayo ubongo wa mtu mzima umejifunza na kuikariri tangu utotoni, tofauti na watoto wadogo ambao mifumo yao bado haijakomaa na huanguka mara kwa mara.
Kuna wanaoanguka, ila kinachomsaidia mtu mzima ni umakini wa kiutu -uzima.
 
Kwani una umri gani wewe kwa sasa? Je bado mama mzazi ana manage privacy yako kama mahali unapolala na unachovaa?
hapa nazungumzia my childhood standard six, ndo hizi mambo niliachaga automatically till now days! 20years. sipo home!
 
Stuxnet mjuba vp ile hali hujaota unajamiiana ila unakuta umepiga bao au unastuka haraka unakuta ilikuwa kidogo uchafue mazingira imekaaje kitaalamu
Mchanganyiko wa shinikizo la shahawa zilizojaa na msuguano mdogo wa chupi au godoro unalipua mfumo wa neva wa uti wa mgongo unaosimamia kutoa shahawa (ejaculation reflex). Kushtuka kwako haraka kunatokea kwa sababu misuli inaposinyaa kutoa shahawa, ubongo unapokea ishara kubwa ya msisimko na kukuamsha ghafla ili "ulinde mazingira
 
hapa nazungumzia my childhood standard six, ndo hizi mambo niliachaga automatically till now days! 20years. sipo home!
Hapo sawa. Na kwenye posts zangu za nyuma nilisema kuwa kadri umri unavyoongeza above 15 tatizo linakwisha lenyewe
 
Nini kitanda! Bodaboda ukipita vijiweni kwao saa 7&8 mchana unakuta wameuchapa usingizi hapo juu kwenye boda zao na hawaanguki.
 
Nini kitanda! Bodaboda ukipita vijiweni kwao saa 7&8 mchana unakuta wameuchapa usingizi hapo juu kwenye boda zao na hawaanguki.
Tayari ubongo zao zimeshatambua mazingira ya viti vya pikipiki
 
Back
Top Bottom