Kwanini mtu mzima akilala hawezi kuanguka kitandani anapojigeuza

Ubongo wako ulikariri mipaka ya godoro ndani ya usiku mmoja hadi wiki mbili tu. Wakati ukiwa macho kabla ya kulala, ubongo ulisajili ramani mpya ya kitanda. Ulipolala, sensa za mwili zilitambua mabadiliko ya shinikizo ukingoni mwa godoro na kukuzuia usianguke kwa kutumia uwezo wa haraka wa ubongo kubadilika (neuroplasticity)
 
Tabia Iliyojifunza (Habitual Memory)Watoto wadogo huanguka kitandani mara kwa mara kwa sababu ubongo wao bado haujajifunza mipaka ya kitanda. Unapokuwa mtu mzima, ubongo unakuwa umeshakariri ukubwa wa kitanda chako


.
mpaka sasa mimi nimelala kwenye masandalusi chini,ila nikienda ugenini kwenye vitanda vya watu sidondoki. Hii imekaaje ndugu mtaalamu?
 
Pia ijulikane kuwa mtu anapozaliwa huzaliwa akiwa na aina mbili za uoga, hii ni survival instict...
1. Uoga juu ya kuanguka
2. Uoga juu ya makelele

Chunguza watoto wadogo hata mtoto mchanga, akitaka kuanguka anavyoweweseka kutafuta mahali pa kujishika...
 
Tabia Iliyojifunza (Habitual Memory)Watoto wadogo huanguka kitandani mara kwa mara kwa sababu ubongo wao bado haujajifunza mipaka ya kitanda. Unapokuwa mtu mzima, ubongo unakuwa umeshakariri ukubwa wa kitanda chako


.
Uko sahihi mkuu, lakini toka ukiwa mdogo mpaka mtu mzima unakuwa unala kwenye kitanda kimoja mpaka ubongo ukariri ukubwa wa kitanda chako
 
Naunga mkono hoja, nina swali jingine je kwanini mtu hapigi chafya akiwa usingizini?
 
Mbona vitanda vya boarding Double Deka wameweka ukingo wa kuzuia mtu kudondoka?

 
mpaka sasa mimi nimelala kwenye masandalusi chini,ila nikienda ugenini kwenye vitanda vya watu sidondoki. Hii imekaaje ndugu mtaalamu?
Ugenini, ubongo wako unalala nusu (First-Night Effect) na upande mmoja unabaki "macho" kama rada. Ubongo unatambua mabadiliko ya kimo na mazingira mapya. Hali hii inaongeza tahadhari, ambapo sensa zako zinapima ukingo wa kitanda kwa umakini mkubwa na kukugeuza haraka kabla ya kudondoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…