Kwanini mtu mzima akilala hawezi kuanguka kitandani anapojigeuza

Experience mkuu
 
Duka la skonga sio...

Pale kontena bwana DC wa Ubungo alikuwa hakosekani akimpigia misele Anna...😄
Hahaaa KONTENA zilikuwa mbili ,Kontena la kwanza jeupe Duka la Anna na la pili jekundu lilikuwa pale Assembly ground linatazamana na gate la Dining hall.

Ile Pisi Anna ilikuwa ya moto sana ,DC mkware sana ndiyo maana picha zake na Giggy money zilivuja.
 
Na vp kuhusu wtt kujikojolea wanapokuwa wamelala? Wengine huwahi kuwacha...kuna wtt miaka 3 au 4 anakuwa kawacha kujikojolea kitandani huwa anashtuka na kwenda chooni. Ila kwa Wengine wanafika hata miaka 10 au 15 bado wanajikojolea. Hawashtuki wakiwa wamebanwa na mkojo mpk wanajikojolea kitandani.
 
Wapo wanaojikuta chini... Na wakilala sakafuni wanajikuta mlangoni...


Cc: Mahondaw
Wanaojikuta chini au mlangoni wana changamoto ya somnambulism (kutembea usingizini) au REM sleep behavior disorder. Katika hali hizi, mfumo wa kupooza misuli (REM atonia) unafeli, na kufanya ubongo kufuatisha ndoto kwa vitendo
 
Wanaojikojolea ukubwani wanalala fofofo kupitiliza, hivyo ubongo hushindwa kusikia ishara za kibofu kilichojaa. Pia, miili yao hupungukiwa homoni ya ADH (Antidiuretic Hormone) inayopunguza mkojo usiku, au mawasiliano kati ya kibofu na ubongo yanachelewa kukomaa kibaolojia. Tatizo hili mara nyingi hurithiwa kifamilia
 

Kontena lile jeupe karibu na school chapel 😊...

Ila nasikia siku hizi skonga yote ipo ndani ya ukuta, sisi wazee wa kitei cha mama Tony tungepata shida sanaaa...
 
Wanaojikuta chini au mlangoni wana changamoto ya somnambulism (kutembea usingizini) au REM sleep behavior disorder. Katika hali hizi, mfumo wa kupooza misuli (REM atonia) unafeli, na kufanya ubongo kufuatisha ndoto kwa vitendo
Kuna dogo aliamshwa kwenda kula, alipo amka tu akaanza kwenda sokoni hapo ni usiku kama saa 3 akakutana na wanao mjua kumwuliza unaenda wapi? akawajibu naenda kukojoa. na ni mdogo!
 
Kuna dogo aliamshwa kwenda kula, alipo amka tu akaanza kwenda sokoni hapo ni usiku kama saa 3 akakutana na wanao mjua kumwuliza unaenda wapi? akawajibu naenda kukojoa. na ni mdogo!
Matukio kama haya hutokea mara kwa mara na kisayansi yanajulikana kama Confusional Arousal (Kuzinduka kwa Kuchanganyikiwa). Hali hii inatofautiana kidogo na kutembea usingizini kwa kawaida.

-:Alipoamshwa ghafla kutoka kwenye usingizi mzito, sehemu ya ubongo inayojihusisha na matendo ya mwili (motor cortex) ilizinduka, lakini sehemu inayohusika na ufahamu na mantiki (prefrontal cortex) ilibaki imelala.

-Ubongo wake ulipokea ishara ya kubanwa na mkojo, lakini kwa sababu ya kuchanganyikiwa, ukaona njia ya kwenda sokoni ndiyo njia ya kwenda chooni.

-Alikuwa na uwezo wa kujibu "naenda kukojoa" kwa sababu sehemu ya lugha ilikuwa imezinduka kiasi, lakini hakuwa na ufahamu wa mazingira halisi
 
Duh! sawa mkuu. halafu kuna zile ndoto za kukojoa kitandani labda mpo mnacheza mpira ukaenda kukojoa pembeni ya uwanja, yani unaanza kukojoa vizuri tu ile unamalizia kupush mkojo ndo unashituka kumbe uko kitandani hii imekaaje mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…