Wewe mtu humwoni kimwili, hajulikani alianzaje kuwepo, hajulikani aliishi wapi kabla hajaiumba hiyo MBINGU anayoiishi sasa, mara sijui hana MWANZO wala MWISHO.
Sasa kiumbe wa hivo utaniambiaje anaeleweka ?
Mungu angekuwa ndani ya time dimension basi chanzo chake kingejulikana na mwisho wake pia
Unauhakika kuwa hayuko ndani ya time dimension ama tu unamtoa kumpeleka mbali ili asihojiwe?
Umejuaje yuko nje ya dimension ya muda na unadai kuwa haeleweki ndugu. Umemuelewaje kuwa yuko nje ya Muda watati umedeclare haeleweki?
You can't see a contradiction here mr.
Huyo Mungu ni nadharia tu na ni mawazo ya watu tu, kila mmoja hujaribu kumuelezea ajuavyo yeye.
Ukitaka kujua hilo, ni jinsi mnavyomuelezea sasa ni tofauti kabsa na zamani alivoelezewa. Zamani hao mitume (kama mnavodai kwa mujibu wenu watu wa imani) wenu hawakumuelezea Mungu kuhusu kuwa nje ya time dimension,
Mungu kaanza kuelezewa kuwa nje ya time dimension baada ya kujengeka kwa nadharia ya space_time katika mfululizo wa mabadiliko na uvumbuzi katika sayansi.
Sayansi ni threat kwa dini coz imeviproof wrong hvo vtabu vyenu vya mafundisho visivyo na update. Vitabu vilivyopitwa na wakati, vitabu vyenye idea kuwa dunia ni tambarare, vitabu vyenye idea kuwa jua linazunguka dunia and etcetera.
Sayansi imewaletea mwamko wa kuwa na wanazuoni (wa kidini) ili kuleta maelezo mapya ya nyongeza ili kuvitetea vitabu hivyo, ingawaje wanadai kitabu cha Mungu kinajitosheleza.
Sasa kama kinajitosheleza why nkisoma kwa ufahamu naona kuna makosa lakini naambiwa nisisome kama gazeti ili sasa yaingizwe mafundisho mapya yaliyoelezewa na wanazuoni ili kuepusha aibu iliyomo kwenye vitabu vyao vinavodaiwa kujitosheleza.
Sasa na ndio maana
wafia dini huhisi kama sayansi iko kushindana na wao, wengine hadi wameigroup kwenye upande wa adui yao (shetani). Na wengine hudai kuwa hata ni mpango wa shetani(sayansi).
Kwasababu sayansi ni threat kwa dini hivyo baadhi wa wana dini wenye kujaribu kuskia hoja za kisayansi na kuzijadili hutumia hii theory ya space_time ili kumtoa Mungu wao mtegoni.
Lakini nnaamini kabisa kuwa Mungu aliyejieleza kwenye vitabu vyenu (vitabu vitakatifu kwa mujibu wenu) hakusema yuko nje ya time dimension.
Na nnaamini pia si kila mwana dini ataelezea kama wewe kuwa Mungu yuko nje ya time dimension. Ni kwamba utanyumbulika tu kulingana na mijadala ili uwe against.
Ukisoma kwa ufahamu hvo vitabu utaelewa kabisa mtunzi wa fadihi zile alimaanisha mbinguni ni hapo juu ya mawingu tu.
Nashangaa sana kuwa Mungu alisemwa yuko mbinguni kwenye mawingu hapo lakini baada ya Sayans kufika ametolewa nje ya dimension ya Muda.
Sasa huyo mungu mbona hataki kuface watu wake anaowapenda?
Au ni kwasababu tu hayupo?
Huoni kuwa ni mwanzo wa kujenga mawazo hasi juu ya uwepo wake. Binafsi Sioni sababu ya kuamini kitu chenye kubadilika badilika namna hii.
Nakunali kujifunza vitu vipya vyenye uhalisia.
Hope sayansi itatoka nje ya muda pia sijui mtasema yuko wapi sasa.
Ni afadhali Huyo Mungu mnavyozidi kumficha huko nje ya Muda, nje ya ulimwengu na kokote mnakompeleka.
Ila right kama kweli angekuwepo ilikuwa ni rahisi Kumuangamiza.