Kwanini Mungu na shetani wote hawataki kufanya kazi na mtu mvivu asiye mbunifu?

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Mtu mvivu, legevu, asiyejali muda na mwenye maneno mengi kuliko vitendo Mungu hampendi na shetani hampendi. Waliomstari wa mbele (frontliners) kwa Mungu na kwa Ibirisi huwezi kukuta mtu mvivu asiyejali na mzembemzembe.

Hakuna nabii wa uongo mvivu asiye risk taker. Wako smart, wanaamka mapema, wanajituma, na wako ngangari kwenye misheni zao. Hata Illuminati na vyama vya siri sio vyama vya wavivu ni vya wachapakazi wenye matokeo kwenye kazi zao.

Hakuna nabii au mtu wa Mungu kwenye maandiko aliyekuwa mvivu, asiyejali Muda na asiye risk taker. Ni watu moto, werevu, wachapakazi, wanawahi kuamka na kuchelewa kulala.

Mungu anatoa Muongozo wake
Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya BWANA kwa ulegevu; Yeremia 48:10

Shetani na Yeye anatambulishwa.
Ayubu 1:7
BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.

Kwa bahati mbaya kupitia makanisa na misikiti yametengenezwa makundi ya watu na ratiba ambazo ni hamasishaji uvivu, uzembe na utegevu. Hawa ni aina ya watu ambao jamii, Shetani na Mungu hawawafurahii kabisa.

Shetani mambo yake anafanya akijua amebanwa na Muda. Hana sekunde ya kupoteza, na ndicho anachotarajia kutoka kwa wafuasi wake.

Nimewahi kumtoa mtu majini, Yale majini yakawa yanalalamika yaende wapi? Yakija huku tunayafukuza huko tunakotaka yarudi ndio wanafukuzwa balaa maana hakuna muda wa kupoteza kule. Siku ya kiyama wachaMungu wavivu wote Mungu atawakataa, Wachaibirisi wote wavivu ibirisi atawakataa. Hili litakuwa kundi ambalo litapotea kwa uchungu mkubwa. Hawana cha kujivunia.

Lengo la uzi huu ni kukumbusha kuwa muaminifu na mchapakazi kwenye upande uliouchagua ukijua uvivu na ulegevu hauna nafasi kwenye ufalme wa ibirisi na wa Mungu.

Idle mind is not devils workshop

Ni hayo tu, Usiseme sikusema.
 
Nina jamaa yangu kila siku analewa na hafsnyi kaxi, sijui hela anapataga wapi mana akilewa anaenda kulala
 
Mungu ndo hapendi mtu mvivu na legevu,shetani anapenda sana mtu mvivu,maana ndo rahisi sana kumtumia katika mambo yake ya ovyo,jua kwamba mtu mvivu ni rahisi hata kupungukiwa katika fikra zake,aweza kuburuzwa kirahisi akapelekwa hata kusikostahili!!,ndo yeye akiambiwa uwa fulani ili upate utajiri ni rahisi kutekeleza.
 
Back
Top Bottom