Akiwa Rais wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere aliwafukuza nchini wanadiplomasia wa Israel na kuwaacha wanadiplomasia wa Palestina.
Ni kwa nini Mwalimu aliwafukuza waisrael na kuwaacha wapalestina??
johnthebaptist wewe si ulikuwepo zama zile pale Twiga hotel mtaa wa Samora Jijini Dar es salaam? Hebu tuelezee.
Nyerere alisitisha uhusiano na Israel katika kutekeleza sera zake za kupinga ukandamizaji na uonevu wa binadamu wa aina yoyote ambao ungetokea mahali popote bila kujali rangi na itikadi.
Kwa mtazamo na msimamo wake huo ndiyo uliomfanya aiunge mkono Palestina kwa hali na mali kwa gharama ya kuvunja uhusiano na Israel,nchi ambayo kiuchumi ilikuwa na mwelekeo wa kuwa mshirika makini na muhimu kwa Tanzania.
Kama ambavyo alivyoifanya Tanzania kutumia rasilimali zake kusaidia kwa hali na mali nchi za Zimbabwe, Namibia ,Msumbiji,Angola na Afrika ya kusini katika harakati zao za kudai uhuru na haki,..ndivyo Nyerere alivyoiunga mkono Palestina.
Lakini kwa mshangao wake Nyerere, ilikuwa ni Palestina hiyo hiyo iliyomuunga mkono Idd Amin wakati wa vita ya Kagera mwaka 1978.
Ikumbukwe Palestina na Libya ni nchi zilizoiunga mkono Uganda kwa kutoa silaha na wapiganaji ardhini.
Tanzania iliungwa mkono na Algeria kwa nguvu zote kwa kupewa shehena ya silaha nyingi hadi vita ilipoisha.
Kwa kupitia funzo hilo,nafikiri Tanzania ni vizuri kuendelea na sera yetu ya kutofungamana na upande wowote.
Hii sera maana yake ni ..siyo lazima rafiki yako awe rafiki yangu,au adui yako lazima awe adui yangu pia,..ugomvi wenu siyo lazima unihusu...,na ugomvi wangu na mtu siyo lazima wengine wahusike