Kwanini Mwalimu Nyerere aliwafukuza Waisrael akawaacha Wapalestina?

Kwanini Mwalimu Nyerere aliwafukuza Waisrael akawaacha Wapalestina?

Sema Nyerere angekuwa na ushirikiano wa kidiplomasia na Israeli, tungekuwa mbali sana na wangetusaidia kwenye vita vya Kagera maana Amin aliwateka Wayahudi kabla ya operation Entebbe.

Kiufupi kuwaunga mkono Palestine, Nyerere akizingua sana. Ndo maana tuko hivi mpaka Leo.
Nchi gani mkuu imesaidiwa na Israel ikatoboa? Ila zipo Nchi kibao Zimesaidiwa na Palestina na zipo vyema...

Mfano mzuri Chille, Walienda Wapalestina kule wame integrate na Society wameinua Uchumi na ku innovate mambo mengi wakati huo.

Wapalestina Hao hao wamezisaidia Nchi za Gulf hadi unaziona leo zimeendelea, Zamani waarabu wengi walikua wafanyabiashara hao wa gulf, hawajui lolote kuhusu vitu kama Diplomasia na Uongozi wakatake advantage ya hio conflict na ku poach talent za Palestina ambao wengi ni Wasomi.
 
Tatizo nyerere alifungamana sana na wavaa kobazi na aliwasikiliza sana. Walimshauri mambo mengi ya kijinga moja wapo ni hilo la kuitimua israel [emoji1134] na kusupport palestine ingali haina manufaa. Mambo mengine ni kama kuchagua Kiswahili kama lugha ya taifa. Kuiunganisha tanganyika na zanzibar etc. lile jamaa ndo maana hata wenzie walikuwa hawampendi wanamuona mwehu.
 
Sema Nyerere angekuwa na ushirikiano wa kidiplomasia na Israeli, tungekuwa mbali sana na wangetusaidia kwenye vita vya Kagera maana Amin aliwateka Wayahudi kabla ya operation Entebbe.

Kiufupi kuwaunga mkono Palestine, Nyerere akizingua sana. Ndo maana tuko hivi mpaka Leo.
Haya ni mawazo ya kitumwa na kitwana
 
Akiwa Rais wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere aliwafukuza nchini wanadiplomasia wa Israel na kuwaacha wanadiplomasia wa Palestina.

Ni kwa nini Mwalimu aliwafukuza waisrael na kuwaacha wapalestina??

johnthebaptist wewe si ulikuwepo zama zile pale Twiga hotel mtaa wa Samora Jijini Dar es salaam? Hebu tuelezee.
Ndio maana nchi ikaingia kwenye laana,njaa,kipindupundu,safura,minyoo na umaskini wa kupindukia.
 
Nyerere alisitisha uhusiano na Israel katika kutekeleza sera zake za kupinga ukandamizaji na uonevu wa binadamu wa aina yoyote ambao ungetokea mahali popote bila kujali rangi na itikadi.

Kwa mtazamo na msimamo wake huo ndiyo uliomfanya aiunge mkono Palestina kwa hali na mali kwa gharama ya kuvunja uhusiano na Israel,nchi ambayo kiuchumi ilikuwa na mwelekeo wa kuwa mshirika makini na muhimu kwa Tanzania.

Kama ambavyo alivyoifanya Tanzania kutumia rasilimali zake kusaidia kwa hali na mali nchi za Zimbabwe, Namibia ,Msumbiji,Angola na Afrika ya kusini katika harakati zao za kudai uhuru na haki,..ndivyo Nyerere alivyoiunga mkono Palestina.

Lakini kwa mshangao wake Nyerere, ilikuwa ni Palestina hiyo hiyo iliyomuunga mkono Idd Amin wakati wa vita ya Kagera mwaka 1978.
Ikumbukwe Palestina na Libya ni nchi zilizoiunga mkono Uganda kwa kutoa silaha na wapiganaji ardhini.
Tanzania iliungwa mkono na Algeria kwa nguvu zote kwa kupewa shehena ya silaha nyingi hadi vita ilipoisha.

Kwa kupitia funzo hilo,nafikiri Tanzania ni vizuri kuendelea na sera yetu ya kutofungamana na upande wowote.
Hii sera maana yake ni ..siyo lazima rafiki yako awe rafiki yangu,au adui yako lazima awe adui yangu pia,..ugomvi wenu siyo lazima unihusu...,na ugomvi wangu na mtu siyo lazima wengine wahusike
Hata waisraili walitusaidia watanzania katika vita ya Uganda.
Katika siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.
 
Kama nchi tulifaidika ni na tunafaidi nini hadi leo kwenye hizo nchi ambazo tulizipigania?

Kenya hawakupigania uhuru wa Africa ya kusini lakini Afrika kusini ilipopata uhuru tu wakenya wakarihusiwa kuingia Afrika ya kusini Visa free sisi tukibanwa kuingia kwa mbinde na kulipia Visa huku watanzania hadi leo wanakimbizwa kama kuku

Nini tumefaidika na Palestina? Nini tumefaidika na hizo nchi zingine zaidi ya uchumi wetu kuporomoka kwa sababu ya gharama za vita na watu wetu kufa vitani kwenye nchi zao

Nyerere alikuwa mpenda sifa zisizo na maana

Sifa tutakula? Kuwa ohh tulipigania uhuru so what ? Vijana wetu wanamaliza vyuo ajira hawana.Sisi kupiga miyowe tu ohh tulipigania uhuru nchi kibao
Mkuu unaonaje maisha ya Tanzania na Kenya? Kenya ni matajiri kushinda sisi ila Watanzania wengi wanaishi maisha mazuri, wana UMASIKINI wa kutupwa huko kwao.

Na kabla ya issue za madawa ya kulevya kuharibu jina la Tanzania kimataifa Passport yetu ilikua na Nguvu na Nchi nyingi walithamini raia toka Tanzania. Dubai tu hapo ilikua ukiwa na Passport ya Tanzania kazi nje nje kama hufahamu Hadi Polisi na wanajeshi wenye vyeo vikubwa vikubwa walitoka Tanzania.

kwa Wakati huo wa Nyerere Aliliheshimisha Taifa na alitimiza wajibu wake, mpaka leo Nchi yetu watu wanaishi kwa kupendana sababu ni mentality hio.

Na sio Tanzania tu kuna Nchi nyingi tu za Ki Africa zimetoa sana misaada kwa wengine ila hilo halijafanya wasiwe na maendeleo badala yake wameendelea zaidi. Jinsi unavyosaidia mtu ndio jinsi Mwenyez Mungu anakuongezea.
 
Hata waisraili walitusaidia watanzania katika vita ya Uganda.
Katika siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.
Kuna siri nyingi hii vita, Israel alikua anamsupport Iddi Amin hadi alivyopinduliwa Obote tetesi ni Uingereza na Israel walio tumia Amin kumpindua.

Ila wakati wa chokochoko ya Vita Amin akaenda Israel kutafuta msaada alivyotoka kule na Jet aliyopewa na Waisrael akaenda moja kwa moja Libya, alivyotoka Libya akaanza kuwaponda Waisrael, so kuna uwezekano Israel walikataa kumsaidia na Libya wakakubali hivyo akaamua kuchange Gia angani. Waisrael wakakasirika sana hasa ndege yao kwenda Libya, kuna uwezekano kweli kulikua na Mkono wa Israel kwenye hii vita.
 
Naam Tanzania haifungamani na Upande wowote wala sio kila Ugomvi inaingilia wala ilikuwa inaingilia..., bali kuna ugomvi na ugomvi..., wewe jirani yako wakiwa wanapigana vibao na mkeo nadhani havikuhusu.., ila ukiona anachukua panga kwenda kumkata mwenza wake, unless wewe ni punguani itakuwa haufanyi la maana kuacha kukemea....

Kama nchi tuna Principles at our Principles at that time tulikuwa hatukai kimya kuacha kutetea kila tunachokiona ni injustices..., na sio nani anaweza kutufadhili zaidi (Baniani Mbaya Kiatu chake Dawa)
Huo unaitwa umbeya

Vikongwe enzi za Nyerere ndio mnaelewa huo ujinga kizazi cha sasa sio rahisi kuelewa

Mambo ya ngoswe mwachie ngoswe. unachungulia kujua mume kachukua panga kutaka kukata mkewe lazima uwe mumbeya.aliyekubuhu kutwa kuchungulia mambo ya jirani.na mkewe
 
Kuna siri nyingi hii vita, Israel alikua anamsupport Iddi Amin hadi alivyopinduliwa Obote tetesi ni Uingereza na Israel walio tumia Amin kumpindua.

Ila wakati wa chokochoko ya Vita Amin akaenda Israel kutafuta msaada alivyotoka kule na Jet aliyopewa na Waisrael akaenda moja kwa moja Libya, alivyotoka Libya akaanza kuwaponda Waisrael, so kuna uwezekano Israel walikataa kumsaidia na Libya wakakubali hivyo akaamua kuchange Gia angani. Waisrael wakakasirika sana hasa ndege yao kwenda Libya, kuna uwezekano kweli kulikua na Mkono wa Israel kwenye hii vita.
Hivi vita vina siri kubwa sana, watu wengi hatujui uhalisia wa hii mifarakano na kwa nini haipatiwi suluhisho. Hivyo tutabaki kushindana kiushabiki kutokana na imani zetu bila ya kuelewa undani wa huu mgogoro.
 
Huo unaitwa umbeya

Vikongwe enzi za Nyerere ndio mnaelewa huo ujinga kizazi cha sasa sio rahisi kuelewa

Mambo ya ngoswe mwachie ngoswe. unachungulia kujua mume kachukua panga kutaka kukata mkewe lazima uwe mumbeya.aliyekubuhu kutwa kuchungulia mambo ya jirani.na mkewe
Wakati Rwanda na Burundi wanachinjana na sisi majirani / UN / OAU inaangalia unadhani kama binadamu wa karne hii tunaweza kuepuka lawama na upuuzi tuliofanya..., Kumbuka hapo walioumia ni watoto na the Weak...., Sasa jiulize mwenye akili ni nani yule anayeangalia mtu kumchinja mke wake eti asiwe Mbeya au yule anayetetea sababu anao uwezo wa kutetea na anatetea the Weak ?

Kwa Taarifa yako huo ndio Ubinadamu na Ustaarabu hauna usasa wala ukale....
 
Nyerere alikuwa.mpenda vita zisizomhusu
Alikuwa mpenda kununua ugomvi iwe wa palestina,iwe wa nchi za kusini mwa Afrika,iwe Uganda,Jimbo.la Biafra Nigeria, iwe wapiganaji waasi wa Polisario wa Sahara wataka kujitenga na Morocco nk yeye kupigana tu na kuunga mkono mavita tu

Nyerere alikuwa Mura mpenda vita.

Ndio maana tumechelewa kuendelea
Nyerere hakuwa Mura. Tafadhali alikuwa mzanaki waliotoka huko rwanda/Burundi ndugu zake TALL. Ndio maana wanapenda vita. Wakurya hayuko hivyo
 
Akiwa Rais wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere aliwafukuza nchini wanadiplomasia wa Israel na kuwaacha wanadiplomasia wa Palestina.

Ni kwa nini Mwalimu aliwafukuza waisrael na kuwaacha wapalestina??

johnthebaptist wewe si ulikuwepo zama zile pale Twiga hotel mtaa wa Samora Jijini Dar es salaam? Hebu tuelezee.
Sindio LAANA yetu ilianzia hapo?
 
Israel imewatesa Sana wapalestina(Arabs, Christians, Muslims), imechukua ardhi Yao kibabe, yaani wayahudi wanaweza kuamka asubuhi, wakavsmia mtaa, wakavunja nyumba za watu, au, wakafurusha watu kutoka kwenye nyumba, waka kaa wenyewe,kisa tu wanakuambia hili eneo ni Mali ya babu zetu, Ibrahim, Isaack na yacobo!!
Sie tunaoishi Leo, kuna MTU alimuona Ibrahim?
Wapalestina wakitaka kukuza uchumi wao, kulima,kwenda nje, kuagiza bidhaa, hata kutumia maji tu, Muyahudi, hataki,wakigundua chanzo, cha maji, kesho myahudi anasema chake!
Unaweza ukafikiri jews wanawachukia wapalestina kwa sababu ni wengi wa Islam, LA hasha, ndani ya Israel, kuna raia wenye asili ya kiarab, na wengine wakristo, lakini wote Hao wanabaguliwa!
"If you treat people like dogs, they will eventually start behaving like one" And that is what Hamas Al qassam brigade did,
Sasa na Hezbollah kutokea rebanon, na wao wamejiunga na Vita.
Yetu macho tu.
 
Sema Nyerere angekuwa na ushirikiano wa kidiplomasia na Israeli, tungekuwa mbali sana na wangetusaidia kwenye vita vya Kagera maana Amin aliwateka Wayahudi kabla ya operation Entebbe.

Kiufupi kuwaunga mkono Palestine, Nyerere akizingua sana. Ndo maana tuko hivi mpaka Leo.
Tumelaaniwa...
 
Kama nchi tulifaidika ni na tunafaidi nini hadi leo kwenye hizo nchi ambazo tulizipigania?

Kenya hawakupigania uhuru wa Africa ya kusini lakini Afrika kusini ilipopata uhuru tu wakenya wakarihusiwa kuingia Afrika ya kusini Visa free sisi tukibanwa kuingia kwa mbinde na kulipia Visa huku watanzania hadi leo wanakimbizwa kama kuku

Nini tumefaidika na Palestina? Nini tumefaidika na hizo nchi zingine zaidi ya uchumi wetu kuporomoka kwa sababu ya gharama za vita na watu wetu kufa vitani kwenye nchi zao

Nyerere alikuwa mpenda sifa zisizo na maana

Sifa tutakula? Kuwa ohh tulipigania uhuru so what ? Vijana wetu wanamaliza vyuo ajira hawana.Sisi kupiga miyowe tu ohh tulipigania uhuru nchi kibao
Yaani kama namkumbuka SAVIMBI vile....
 
Akiwa Rais wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere aliwafukuza nchini wanadiplomasia wa Israel na kuwaacha wanadiplomasia wa Palestina.

Ni kwa nini Mwalimu aliwafukuza waisrael na kuwaacha wapalestina??

johnthebaptist wewe si ulikuwepo zama zile pale Twiga hotel mtaa wa Samora Jijini Dar es salaam? Hebu tuelezee.
Nyerere aliitikia wito wa umoja wa nchi za Afrika, OAU wakati huo, kuvunja uhusiano wa kibalozi na Israel kufuatia vita vya Yom Kippur kati ya Israel na Waarabu mwaka 1973. Yom Kippur ni sikukuu ya Kiyahudi. Misri na Syria ziliamua kushambulia Israel kwa pamoja, Misri upande huu na Syria upande ule, siku hiyo ya sikukuu ya Kiyahudi wakijua ulinzi utakuwa pungufu. Kweli ndani ya siku tatu walifanikiwa kutwaa maeneo kadhaa ya Sinai (kwa Misri) na Golan Heights (kwa Syria) ambayo yalikuwa yametekwa na Israel katika 'Vita vya Siku Sita' vya Mwaka 1967. Israel ikajipanga na kurudisha mapigano na kuyatwaa upya ndani ya wiki mbili maeneo yote yaliyokuwa yamekombolewa na wakaenda mbali zaidi na kutwaa maeneo mengine mapya.
Kutokana na kuongezeka kwa maeneo ya nchi za Kiarabu yaliyokuwa yanakaliwa na Israel, na kuonyesha mshikamano na Waarabu kwa ubabe huo wa Israel, OAU iliamua kuvunja uhusiano na Israel. Nchi mbili pekee za Afrika ndizo hazikuenda na uamuzi huo; nazo ni Malawi na Afrika Kusini, bado ikiwa ya kibaguzi siku hizo.
Juzi Jumamosi Wapalestina wameshambulia Israel wakijua siku hiyo ni ya mapumziko kwa Israel. Sijui nini kitafuata.
 
Israel ilikuwa inakalia maeneo ya Misri (Sinai) baada ya ile vita ya siku sita.

Misri alikuwa mwanachama wa umaja wa nchi huru za Afrika. It was that simple. Nchi nyingi za Afrika zilisitisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel.

Wapelestina walikuja kitugeuka wakati wa vita ya Kagera kwa kupigana upande wa Nduli.
Ndege ya wa-Israel iliyowahi kutekwa Entebbe Uganda mwaka 1976, Wapalestina wote waliachiwa. Pengine sababu ndiyo hiyo kwamba Idd Amin alikuwa ameshajenga urafiki na wapalestina
 
Back
Top Bottom