Kwanini Mwalimu Nyerere aliwafukuza Waisrael akawaacha Wapalestina?

Kwanini Mwalimu Nyerere aliwafukuza Waisrael akawaacha Wapalestina?

Sema Nyerere angekuwa na ushirikiano wa kidiplomasia na Israeli, tungekuwa mbali sana na wangetusaidia kwenye vita vya Kagera maana Amin aliwateka Wayahudi kabla ya operation Entebbe.

Kiufupi kuwaunga mkono Palestine, Nyerere akizingua sana. Ndo maana tuko hivi mpaka Leo.
Pelekeni uvivu na uzembe wenu kule na siyo kubaki kumsingizia Nyerere.
 
Akiwa Rais wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere aliwafukuza nchini wanadiplomasia wa Israel na kuwaacha wanadiplomasia wa Palestina.

Ni kwa nini Mwalimu aliwafukuza waisrael na kuwaacha wapalestina??

johnthebaptist wewe si ulikuwepo zama zile pale Twiga hotel mtaa wa Samora Jijini Dar es salaam? Hebu tuelezee.
Ndio maana ameiletea hii nchi laana
 
Nyerere alikuwa.mpenda vita zisizomhusu
Alikuwa mpenda kununua ugomvi iwe wa palestina,iwe wa nchi za kusini mwa Afrika,iwe Uganda,Jimbo.la Biafra Nigeria, iwe wapiganaji waasi wa Polisario wa Sahara wataka kujitenga na Morocco nk yeye kupigana tu na kuunga mkono mavita tu

Nyerere alikuwa Mura mpenda vita.

Ndio maana tumechelewa kuendelea
Sijui mitaala yetu kama inafundisha vijana historia ya nchi yetu ili kutambua misimamo ya nchi na sababu za wakati huo tusingeshuhudia huu utumbo ulioandika.
 
Again mtu mwenye Busara na Utu hatoi msaada ili kesho asaidiwe anafanya hivyo kama kuna injustice...

Kwa logic yako nikiona mwanamke anabakwa nisimsaidie sababu kesho anaweza akanitukana, au kile aliyenitukana juzi leo akiwa anaonewa na mimi naweza kukemea nikae kimya ?

Hii logic ya wapi hii ? Binafsi adui ni injustice na sio kuangalia anayefanya injustice kama ni ndugu au rafiki yako..., hata kama ndugu zangu wanakula watu siwezi kutetea upuuzi sababu ni ndugu
Una akili sana sana. Hawa watu wa shule za kata ni bure kabisa. Kuna kipindi ebola ilipamba moto kweli kweli na kuna wazungu walijitolea kuja Afrika kusaidia kutibu wagonjwa. Matokeo yake kuna waliambukizwa na kufariki. Jambo kama hili mtu mwenye upeo mdogo kama hawa jamaa anaweza kusema walijitakia na wasijue kuwa walifanya jambo zuri sana kwa dunia. Vivyo hivyo, kupinga uovu duniani ni kazi ya binadamu yoyote aliyestaarabika ili kuifanya dunia iwe mahali pazuri pa kuishi. Ulaya kuna vikundi vya watu vinafanya maandamano kila siku kupinga uharibifu wa mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo. Binadamu yeyote mwenye akili hufanya mema na kupinga maovu bila kujali malipo.
 
Sijui mitaala yetu kama inafundisha vijana historia ya nchi yetu ili kutambua misimamo ya nchi na sababu za wakati huo tusingeshuhudia huu utumbo ulioandika.
Elimu ya Bongo imeingia mdudu. Wengi wamekariri ili kushinda mitihani na hawakusoma kuelewa.
 
Kumkosoa mtu ndio kumchukia? Mbona unatumia akili za mashabiki wa soka Tanzania.
Nyerere mwenyewe alitaja makosa yake kwenye Tujisahihishe, ina maana alikuwa anajichukia?

Nyerere ni Rais bora zaidi kati ya waliotokea Tanzania, kwangu mimi. Kuwa Rais wangu bora hakunifanyi nisiseme makosa yake
Hahahah
 
Haya alisaidia wapalestina ilipofika vita kupiga na Uganda wapalestina wakawa wanamuunga mkono Idd Amin kutupiga sisi watanzania tena Nyerere mwenyewe aliyekuwa akiwaunga mkono akiwa Raisi
Ushirikiano kati ya nchi na nchi unategemeana na Viongozi na siyo wananchi
 
Kama nchi tulifaidika ni na tunafaidi nini hadi leo kwenye hizo nchi ambazo tulizipigania?

Kenya hawakupigania uhuru wa Africa ya kusini lakini Afrika kusini ilipopata uhuru tu wakenya wakarihusiwa kuingia Afrika ya kusini Visa free sisi tukibanwa kuingia kwa mbinde na kulipia Visa huku watanzania hadi leo wanakimbizwa kama kuku

Nini tumefaidika na Palestina? Nini tumefaidika na hizo nchi zingine zaidi ya uchumi wetu kuporomoka kwa sababu ya gharama za vita na watu wetu kufa vitani kwenye nchi zao

Nyerere alikuwa mpenda sifa zisizo na maana

Sifa tutakula? Kuwa ohh tulipigania uhuru so what ? Vijana wetu wanamaliza vyuo ajira hawana.Sisi kupiga miyowe tu ohh tulipigania uhuru nchi kibao
Huenda hatujanufika ila kutetea ubinadamu ni heshima tosha.
Na hiyo ni asili tu kuungana na nayeonewa hata kama hatakulipa.
Unauliza tumenufaika nini basi hujui ushawishi wa Tanzania hapa Africa.
Kwa taarifa yako Kenya imeshindwa kupitisha wanadiplomasia wake kwenye nafasi za juu AU au UN kutokana na kutokuwa na harakati wakati wa uhuru. Muulize Amina Abdallah aliyekuwa waziri wa mambo ya nje ya Kenya enzi za Uhuru jr akuambie.
 
Hupimi success in Dollar wakati hiyo success imetumia Dollars au hizo harakati Tanzania tulizifanya bure bila gharama.

Basi sawa unamtetea Nyerere kwenye suala la Palestina. Vipi suala la Biafra kujitenga nalo Nyerere aliunga mkono nalo unamteteaje. Suala la Morocco kujitenga nalo aliwaunga mkono separatists.
Wakati huo amefanya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo hataki utengano.

Nchi hata vyoo hamna ila vipaumbele vikawa kiherehere kila kona ya dunia. Sasa nini ilikuwa maana ya kuwa mwanachama wa NAM. Hizo sera za Nyerere zilikuwa zake binafsi, hazikuwa na mtazamo wowote kitaifa na mashiko hamna. Leo hii hata kiongozi awe nani pale Iran hawezi kuitambua Israel, sababu ni sera ya kitaifa sio sera ya mtu binafsi.

Nyerere alikuwa na kiherehere chenye kuhatarisha usalama wetu, uchumi na utengamano. Ndio kilisababisha ampe hifadhi Milton Obote baada ya kupinduliwa na Amin pale Uganda. Uliona wapi kwingine nchi maskini, kiongozi wa nchi anapewa political asylum nchi jirani kabisa na anakuja na wapiganaji wake wanapewa mafunzo na uwezeshaji.

Hao wenyewe Israel hawanunui ugomvi usiowahusu na wasio na maslahi nao. Israel haija silaha Ukraine wala kuisaidi Urusi, wakati huo Ukraine imetoa statement ya kuinga mkono Israel dhidi ya Hamas. Sababu Ukraine inapata support kutoka kwa walewale wanaoipa support Israel.

Diplomasia za nchi haziendi kishamba hivyo kama misaada ya waumini wa kanisa. Utaishia kuwa tambala la deki, huna mshirika kazi kujitia ujuaji kwa kila mgogoro duniani. China wana uchumi mkubwa ila unaona wamekula mute kwani wajinga? Wana migogoro yao wanayolazimika kuingia, sio kila kitu unajifanya unachukua upande.
Kunyamazia kumkemea muonezi nawe unakuwa sehemu ya uonevu.
Kwa sera zetu za ujamaa tuliamini watu wote ni sawa Sasa utanyamazije ukandamizaji wa kibeberu kwa watu wanyonge?
Kuhusu Sahara Magharibi na Biafra kumbuka kule walikuwa wnanyanyaswa sna na Koroko/Nigeria je angekaa kimya watu wauwawe?
Kuhusu Tanzania muungano ulikuwa wa hiari Wala hakuna aliyelazimishwa.
Utakuwa kiongozi namna gani kama huwezi chukia msimamo?
Yaani Kila kitu yes yes yes huwezi kuwa kiongozi namna hiyo.
 
Waisrael wa leo sio wale wa kale. Hawa wa leo inatakiwa wafukuzwe popote wanapoonekana
Ukimuona uisrael jua US yupo nyuma yake kua makini mnachoongea,US yy anafuta vita nje ya nchi yake iliapate rasilimali za bure nakuuza siraha be very very careful na hao watu.
 
Israel ilikuwa inakalia maeneo ya Misri (Sinai) baada ya ile vita ya siku sita.

Misri alikuwa mwanachama wa umaja wa nchi huru za Afrika. It was that simple. Nchi nyingi za Afrika zilisitisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel.

Wapelestina walikuja kitugeuka wakati wa vita ya Kagera kwa kupigana upande wa Nduli.
Wao pamoja na gadaf
 
Unauliza tumenufaika nini basi hujui ushawishi wa Tanzania hapa Africa.
Kwa taarifa yako Kenya imeshindwa kupitisha wanadiplomasia wake kwenye nafasi za juu AU au UN kutokana na kutokuwa na harakati wakati wa uhuru. Muulize Amina Abdallah aliyekuwa waziri wa mambo ya nje ya Kenya enzi za Uhuru jr akuambie.
Sawa baada Ya Amina Abdallah mkenya kupitishwa kwa Ushawishi wa Tanzania sisi kama nchi tulipata nini kutoka Kenya kama asante ya.huo ushawishi?
 
Back
Top Bottom