Hupimi success in Dollar wakati hiyo success imetumia Dollars au hizo harakati Tanzania tulizifanya bure bila gharama.
Basi sawa unamtetea Nyerere kwenye suala la Palestina. Vipi suala la Biafra kujitenga nalo Nyerere aliunga mkono nalo unamteteaje. Suala la Morocco kujitenga nalo aliwaunga mkono separatists.
Wakati huo amefanya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo hataki utengano.
Nchi hata vyoo hamna ila vipaumbele vikawa kiherehere kila kona ya dunia. Sasa nini ilikuwa maana ya kuwa mwanachama wa NAM. Hizo sera za Nyerere zilikuwa zake binafsi, hazikuwa na mtazamo wowote kitaifa na mashiko hamna. Leo hii hata kiongozi awe nani pale Iran hawezi kuitambua Israel, sababu ni sera ya kitaifa sio sera ya mtu binafsi.
Nyerere alikuwa na kiherehere chenye kuhatarisha usalama wetu, uchumi na utengamano. Ndio kilisababisha ampe hifadhi Milton Obote baada ya kupinduliwa na Amin pale Uganda. Uliona wapi kwingine nchi maskini, kiongozi wa nchi anapewa political asylum nchi jirani kabisa na anakuja na wapiganaji wake wanapewa mafunzo na uwezeshaji.
Hao wenyewe Israel hawanunui ugomvi usiowahusu na wasio na maslahi nao. Israel haija silaha Ukraine wala kuisaidi Urusi, wakati huo Ukraine imetoa statement ya kuinga mkono Israel dhidi ya Hamas. Sababu Ukraine inapata support kutoka kwa walewale wanaoipa support Israel.
Diplomasia za nchi haziendi kishamba hivyo kama misaada ya waumini wa kanisa. Utaishia kuwa tambala la deki, huna mshirika kazi kujitia ujuaji kwa kila mgogoro duniani. China wana uchumi mkubwa ila unaona wamekula mute kwani wajinga? Wana migogoro yao wanayolazimika kuingia, sio kila kitu unajifanya unachukua upande.