Kwanini Mwalimu Nyerere aliwafukuza Waisrael akawaacha Wapalestina?

Kama nchi tulifaidika ni na tunafaidi nini hadi leo kwenye hizo nchi ambazo tulizipigania?

Kenya hawakupigania uhuru wa Africa ya kusini lakini Afrika kusini ilipopata uhuru tu wakenya wakarihusiwa kuingia Afrika ya kusini Visa free sisi tukibanwa kuingia kwa mbinde na kulipia Visa huku watanzania hadi leo wanakimbizwa kama kuku

Nini tumefaidika na Palestina? Nini tumefaidika na hizo nchi zingine zaidi ya uchumi wetu kuporomoka kwa sababu ya gharama za vita na watu wetu kufa vitani kwenye nchi zao

Nyerere alikuwa mpenda sifa zisizo na maana

Sifa tutakula? Kuwa ohh tulipigania uhuru so what ? Vijana wetu wanamaliza vyuo ajira hawana.Sisi kupiga miyowe tu ohh tulipigania uhuru nchi kibao
 
Aseeee ni wajomba zetu wale?
Wamezifanyia nini nchi ambazo wanaushirikiano nazo?
 
Haya alisaidia wapalestina ilipofika vita kupiga na Uganda wapalestina wakawa wanamuunga mkono Idd Amin kutupiga sisi watanzania tena Nyerere mwenyewe aliyekuwa akiwaunga mkono akiwa Raisi
 
Are you sure tumechelewa kuendelea? Au unavaa miwani ya mbao tu? Kwa taarifa yako Tanzania ni moja na nchi 10 zenye uchumi mkubwa Afrika zikiwa ni pamoja na Nigeria, Egypt, Morocco, S/Africa, Ethiopia, Ghana, Kenya, Angola na Algeria
 
Sasa unajisaidiaje bila connection?
Connection inaleta transfer of technologies, una wataalam au magenius wa kubuni teknolojia yako mwenyewe? Kwa kizazi cha wabongo kinachowaza ngono muda wote?

Ok, Mama anatafta connection hope soon
Tutakua kama Dubai/any developed country
 
Are you sure tumechelewa kuendelea? Au unavaa miwani ya mbao tu? Kwa taarifa yako Tanzania ni moja na nchi 10 zenye uchumi mkubwa Afrika zikiwa ni pamoja na Nigeria, Egypt, Morocco, S/Africa, Ethiopia, Ghana, Kenya, Angola na Algeria
Uchumi mkubwa wa kwenye makaratasi hali halisi haiakisi hivyo mitaani na vijijini wanakoishi majority ya watanzania
 
Haya alisaidia wapalestina ilipofika vita kupiga na Uganda wapalestina wakawa wanamuunga mkono Idd Amin kutupiga sisi watanzania tena Nyerere mwenyewe aliyekuwa akiwaunga mkono akiwa Raisi
Again mtu mwenye Busara na Utu hatoi msaada ili kesho asaidiwe anafanya hivyo kama kuna injustice...

Kwa logic yako nikiona mwanamke anabakwa nisimsaidie sababu kesho anaweza akanitukana, au kile aliyenitukana juzi leo akiwa anaonewa na mimi naweza kukemea nikae kimya ?

Hii logic ya wapi hii ? Binafsi adui ni injustice na sio kuangalia anayefanya injustice kama ni ndugu au rafiki yako..., hata kama ndugu zangu wanakula watu siwezi kutetea upuuzi sababu ni ndugu
 
Soma niliposhajibu..., Principles Tumefaidika nini ? Unadhani kipindi kile Tanzania ilikuwa na Sifa kiasi gani kwenye upiginia Uhuru wa nchi nyingine za Kiafrika ? Waulize kina Museveni kuna kipindi alisema hii ni kama Hijja au Sehemu ambayo watu wa Imani wanakwenda kutoa Tribute (kizazi hiki mgekuwa na akili) mgeweza kuki-market watu wakawa wanakuja kutembea na kushukuru Msaada wa Babu zao waliopata kutoka Tanzania.... (that is Priceless) Lakini ukiwa unapima every Success na Dollar Signs huwezi kunielewa...
 
Daah unamaanisha sisi hatuna uwezo kujiendeleza wenyewe hadi tuwe na mafungamano na Taifa lingine litukwamue??🤔🤔
Eti ndo maana tuko hivi mpaka Leo?? Kweli??
So kuboronga kwa ccm na watendaji wa serikali ni kwa sababu hatukuwa na mahusiano mazuri na Israel?
 
Kumbe Palestine I mshenzi hivi🤔
Sikulijua hili
 
Are you sure tumechelewa kuendelea? Au unavaa miwani ya mbao tu? Kwa taarifa yako Tanzania ni moja na nchi 10 zenye uchumi mkubwa Afrika zikiwa ni pamoja na Nigeria, Egypt, Morocco, S/Africa, Ethiopia, Ghana, Kenya, Angola na Algeria

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Naam Tanzania haifungamani na Upande wowote wala sio kila Ugomvi inaingilia wala ilikuwa inaingilia..., bali kuna ugomvi na ugomvi..., wewe jirani zako wakiwa wanapigana vibao mme na mke nadhani havikuhusu.., ila ukiona mmoja anachukua panga kwenda kumkata mwenza wake, unless wewe ni punguani itakuwa haufanyi la maana kuacha kukemea....

Kama nchi tuna Principles and our Principles at that time tulikuwa hatukai kimya kuacha kutetea kila tunachokiona ni injustices..., na sio nani anaweza kutufadhili zaidi (Baniani Mbaya Kiatu chake Dawa)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…