Kwanini Mwalimu Nyerere, pamoja kupewa PhD 23, tuzo lukuki, usomi na weledi vyake hakuwahi wala kupenda kuitwa daktari? Je, aliogopa au hakujua?

Ati daktari stive nyerere hivi maduduna ya kiafrika yanaona fahari kuitwa daktari huku hayana imoact yoyote kidunia? Akina Elon hawataki hata udaktari wa heshima lakini mamvo wanayofanya ni makubwa.
Akina Biten, Putin, Netanyahu huwezi kuwaita Dr hawataki sifa za kjinga jinga
 
Maisha ya kawaida kielimu unatakiwa uishie kwenye 'masters' tu; ukienda kutafuta PhD+ unakuwa umeamia daraja lingine la maisha ya utafiti, na hayo yanakuwa ndio maisha yako siku zote.

Wengi hawapendi kujiita hayo majina na hasa uko nje kwa sababu, kujiita huko unakupa deni la kufanya tafiti kadhaa kila mwaka, Je ni wangapi wanafanya hizo tafiti?

Ukijitambulisha wewe ni Dr au Prof. fulani, watu wataingia mtandaoni na kuangalia machapisho uliyoyatoa na yana 'standard' zipi. Hii ndio sababu kuu wenye hivyo vyeti kutokujitangaza.

Huu wa heshina hauna mahusiano na ule wa kusomea, kwa sababu hauna haja ya kufanya au kukudai tafiti; kwa hiyo ni muhimu kutofautisha.

Ni sawa na ukienda buchani, utamuona muuza nyama kavaa nguo nyeupe, na ukienda hospitalini utamkuta mtu anayetibu amevaa nguo nyeupe; lakini wote wamevaa makoti meupe.

kwa hiyo haitafsiri, wote waliovaa vazi jeupe, wanatibu.​
 
Zile simulizi za zamani zina muktadha, mantiki, pamoja na maudhui makubwa sana ndani yake. Mathalani ile ya mfalme akiwa uchi mtupu huku akiwa ameaminishwa kuwa kavaa mavazi ya thamani na fahari kubwa.

Ijapokuwa yeye binafsi, na kutokana na ujuha wale hakuweza kuyaona, bali aliiuamini upumbavu wake
Hali akijijua yeye ni uchi, na wala hakuweza kuyaona, alizuga na kujifanya anayaona kwa kuwa aliaminishwa hivyo.

Aidha, ijapokuwa wapambe wake pia wajitambua kuwa wao ni wadhambi, pia hawakuyaona, mavazi hayo bali walilazimika kumsifia tu huku wakiuona utupu wake.

Hali kadhalika ilikuwa pia kwa wafuasi wake wote, hata pale walipouona utupu wake hadharani, bado kwa unafiki wao walilazimika kusifia uzuri wa mavazi/mavuzi yake

Dogo asiye kuwa na hili wala lile ndiye pekee ambaye aliweza kuuanika upuuzi huo. CCM ipo uchi, na kila mtu huutambua ukweli huo. Vyombo vya ulinzi na usalama ijapokuwa huuona kwa wazi utupu vimeamua kusifia na kuulinda ufahari wa mavazi yake ambayo hayapo.

Mficha maradhi kilio humuumbua.
 
Ati daktari stive nyerere hivi maduduna ya kiafrika yanaona fahari kuitwa daktari huku hayana imoact yoyote kidunia? Akina Elon hawataki hata udaktari wa heshima lakini mamvo wanayofanya ni makubwa.
Kuna wengine wanaanza na CPA fulani,wale wa procurement nao wanaanza na PC nini sijui,bado kidogo ma HR certified nao wanaanza kujiita HR Fulani,sasa hao wote kaangalie wanachofanya huko maofisini,ni hasara tupu,rushwa za ngono kujipendekeza, uchawa na kugombea semina
Kimsingi hii nchi imekuwa ya wapenda misifa,viongozi wanataka waitwe mheshimiwa,kwenye dini nako wanataka waitwe sijui baba mtakatifu,Nabii mkuu nk, ndio maana hata wananchi mtaani wameamua kuitana mkuu,kiongozi,mara tajiri
 
Mkuu wanaotunukiwa PhD ya heshima hawaitwi daktari. Ni ulimbukeni tu
Kwa mfano Obama amegaiwa PhD 14 je ulisikia akiitwa Daktari Obama?
Tuachane na ujinga na UCHAWA !!!!
 
Mkuu wanaotunukiwa PhD ya heshima hawaitwi daktari. Ni ulimbukeni tu
Kwa mfano Obama amegaiwa PhD 14 je ulisikia akiitwa Daktari Obama?
Tuachane na ujinga na UCHAWA !!!!
Yule bibi anapenda PhD,kama anavyopenda ile amka na BBC asubuhi.
 
Siku zote Debe tupu haliachi kupiga kelele
 
Wakati nipo mdogo tulikuwa tukiambiwa raisi wa kwanza ni "mwalimu nyerere", basi walimu wote naanza kuwaogopa kwa kudhania ya kwamba wana akili sana kama nyerere alooo kumbe sasa
 
Hakuwa mshamba au kilaza kama hawa wengine ambao hawataki kusoma kupata hizo Phd za ukweli ila wananunua Udaktari na kutaka kutambulika hivyo. Mimi ni Injinia.but nimewakataza watu kuniiita hilo jina nataka tu niitwe jina langu Komeo.
 
Wakati nipo mdogo tulikuwa tukiambiwa raisi wa kwanza ni "mwalimu nyerere", basi walimu wote naanza kuwaogopa kwa kudhania ya kwamba wana akili sana kama nyerere alooo kumbe sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…