Kwanini Mwalimu Nyerere, pamoja kupewa PhD 23, tuzo lukuki, usomi na weledi vyake hakuwahi wala kupenda kuitwa daktari? Je, aliogopa au hakujua?

Kwanini Mwalimu Nyerere, pamoja kupewa PhD 23, tuzo lukuki, usomi na weledi vyake hakuwahi wala kupenda kuitwa daktari? Je, aliogopa au hakujua?

View attachment 3146597

Kwa walioishi wakati wa utawala wa baba yenu wa taifa ambaye ni kaka yangu, wanakumbuka alivyokuwa msomi, mbobezi na mwanafalsa wa aina yake.

Pamoja na hayo na kutuzwa shahada za uzamivu 23, hakuwahi kuitwa au kujiita daktari.

Je hakujua ujiko wake? Aliogopa nini na kwanini? Je hili linamaanisha na kutufunza nini? Kwa wanaotaka kujua Mwalimu alikuwa na shahada ngapi ukiongezea na zile mbili alizosomea, BONYEZA HAPA TAFADHALI.
View attachment 3146595
Phd za zawadi ndio hupenda phd zao zitajwe
 
Nadhani alijiita mwalimu sababu alitumia siasa katika kutatua migogoro baina ya Tanzania na nchi pinzani, pia alim descpline idiamini hivyo inafaa kabisa kumuita mwalimu.
 
Mabumunda mengi yanapenda vitu vya dezo. Zingatia na elewa neno Bumunda.
 
Nafikiri kuitwa Mwalimu aliona ni bora zaidi na wengi walikuwa sio wasomi kwa hiyo akijiita tofauti angewapoteza

Mwalimu lilimfaa na wengi tulimuita hivyo
 
Ni choice ya mtu tu, hata Obama na mkewe wako level za udaktari wa kitaaluma, lakini hawapendi kutumia utangulizi huo. Ni suala la uhuru wa kikatiba. Kwa hiyo uhuru wako wa kuchagua unachopenda, usiutumie kumchagulia mwenzako,. Maisha sio kama uniform za shule ya msingi, kwamba mfanane wote
Eti choice ya mtu! Hebu tuache ujuaji kwenye masuala ya msingi. Mtu anayetunukiwa udaktari wa heshima hapaswi kuwa "addressed" kwa title ya Dr. Ni ulimbukeni na uchawa wa waTz ndio unaofanya watu wawaite hao wenye PhD za heshima kwa title ya Dr. Yaani ni vituko!!
 
Daktari kwa mtazamo wangu ni yule ambaye anatoa ufumbuzi wa jambo fulani kuisaidia jamii kuondokana na changamoto zinazo ikabili. Jamii yetu bado ipo na changamoto ya ujinga, maradhi, umasikini na sasa uchawa. Ili mtu aweze kuonekana ni daktari ni lazima kuyachukia na kuyatafutia ufumbuzi mambo hayo kwa nguvu zake zote, kinyune na hapo udaktari wake/wako/wangu hauna maana yoyote kwa jamii yetu
 
Na ww pia umekosa wazo la kuanzisha thread. Kwani ukiitwa Dr na usiitwe Dr itakuwa umepata au umekosa nn? Tujaribu kujadili au kuanzisha thread za maana zenye impact kwa issues za kitaifa. Mfano kikwete kuiba gesi mtwara.
Du hujui!!! Uliza google itakwambia. Yaani karne hii bado kuna watu wanauliza. maswali kama haya kweli! Lailahaillah!
 
Haya mambo sidhani kama yako popote duniani, zaidi ya Tanzania. Na Tanzania wanayoyakuza ni hawa CHAWA. Utakuta wanayemsifia hana sifa yoyote hivyo wanatafuta kilemba kumvika ili afit kwenye jamii.

Zamani nilikuwa naangalia CV za wabunge na mawaziri kwenye website ya Bunge, unakuta kuna mbunge CV yake inasema alimaza elimu ya msingi, akawa secretary ofisi za ccm, na kushika nafasi za chama basi sasa ni waziri au Mbunge.

Hao ndio watafutiwa vilemba kuvikwa, na CHAWA ndiwo hubeba jukumu hilo.
 
Back
Top Bottom