Kwanini Mwamposa asiende kwenye mahosiptali kuombea wagonjwa na tukaona wanapona?

Why Mungu asikutokee wewe akakupa maono... mbona Mungu anamtegemea binadamu ili asambaze ujumbe na sisi wote tumuamini tu huyo binadama kiholelaholela

Mungu hujidhihirisha kwa watu kupitia karama mbalimbali. Sio unabii tu. kuna uimbaji, uhubiri, ualimu kwa kutaja vichache. Katika hili, Biblia inasema.

“Basi kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni mmoja. Pia kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni mmoja. Kisha kuna aina tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule anayeongoza kazi zote kwa kila mtu. Roho Mtakatifu hudhi hirishwa kwa kila mtu kwa faida ya wote.” 1 WAKORINTHO 12: 4-7

Mungu hamtegemei Mwanadamu kusambaza ujumbe wake maana anaweza kuagiza Malaika zake wakafanya kazi hiyo. Lakini Mungu anampa nafasi Mwanadamu ili tuonyane sisi kwa sisi na kufundishana hata katika udhaifu wetu kwasababu maisha ya duniani yaliandaliwa kwaajili ya Mwanadamu na Mungu ajidhihirishe katikati yao wenyewe.

“Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.” WAKOLOSAI 3:16-17

Hatupaswi kuamini kila roho kiholela. Biblia inasema;

“ Wapenzi msiamini kila roho bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwasababu manabii wengi wa uongo wametokea duniani.” 1 YOHANA 4:1-2
 
hospitali wanaamini katika Tiba ya kisayansi mkuu na wala hairuhusiwi mtu kwenda kutoa tiba ya mombi walatiba asili. kama unaumwa nenda Kawe akakuombee utapona. Hata Yesu mwenyewe hakuwahi kwenda Hospital hata aliposikia rafiki yake Mkubwa Lazaro anaumwa hakutaka kwenda kumwangalia walakumuombea hadialipokufa.

Kama unahitaji Kuombewa au una ndugu yako mgonjwa basi mpeleke akafanyiwe maombi kisha uje na mrejesho

Mwisho sio magonjwa yote yanatibika kwa maombi.

Ugonjwa gani hautibiki kwa maombi?
 
Mungu hujidhihirisha kwa watu kupitia karama mbalimbali. Sio unabii tu. kuna uimbaji, uhubiri, ualimu kwa kutaja vichache. Katika hili, Biblia inasema.

“Basi kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni mmoja. Pia kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni mmoja. Kisha kuna aina tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule anayeongoza kazi zote kwa kila mtu. Roho Mtakatifu hudhi hirishwa kwa kila mtu kwa faida ya wote.” 1 WAKORINTHO 12: 4-7

Mungu hamtegemei Mwanadamu kusambaza ujumbe wake maana anaweza kuagiza Malaika zake wakafanya kazi hiyo. Lakini Mungu anampa nafasi Mwanadamu ili tuonyane sisi kwa sisi na kufundishana hata katika udhaifu wetu kwasababu maisha ya duniani yaliandaliwa kwaajili ya Mwanadamu na Mungu ajidhihirishe katikati yao wenyewe.

“Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.” WAKOLOSAI 3:16-17

Hatupaswi kuamini kila roho kiholela. Biblia inasema;

“ Wapenzi msiamini kila roho bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwasababu manabii wengi wa uongo wametokea duniani.” 1 YOHANA 4:1-2
Mabii wote wa uongo walitokea duniani kwani yeye yesu alitokea wapi kama siyo duniani?
 
Hili ndio swali ninalojiuliza kama kweli huyu ni mchungaji wa ukweli.

Kwa mfano, kwanini tusimuone Mwamposa akiwa Ocean Road hospitali anaombea wagonjwa wa kansa na tukaona wananyanyuka vitandani au madaktari wakathibitisha kupona kwa hao wagonjwa?

Uhuru wa kuabudu umegeuka mtaji kwa wajanja wachache huku wajinga wakiwawatajirisha wenzao.
Mwamposa hana lolote ni tapeli tu kama matapeli wengine tuwajuao mjini plus na ujinga wa waumini.
 
Hakuna aliyefufuliwa na yesu hata mmoja kwanini yeye hakujifufua inamaana hakutaka yeye kuishi?

Lazaro alifufuliwa na Yesu (Soma YOHANA 11) Yesu alipokufa, siku ya tatu alifufuka na alikaa tena Duniani kwa siku 40 kabla ya kupaa. Hujui maandiko wala historia unakuja kwenye mjadala kubwabwaja?!
 
Mungu hujidhihirisha kwa watu kupitia karama mbalimbali. Sio unabii tu. kuna uimbaji, uhubiri, ualimu kwa kutaja vichache. Katika hili, Biblia inasema.

“Basi kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni mmoja. Pia kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni mmoja. Kisha kuna aina tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule anayeongoza kazi zote kwa kila mtu. Roho Mtakatifu hudhi hirishwa kwa kila mtu kwa faida ya wote.” 1 WAKORINTHO 12: 4-7

Mungu hamtegemei Mwanadamu kusambaza ujumbe wake maana anaweza kuagiza Malaika zake wakafanya kazi hiyo. Lakini Mungu anampa nafasi Mwanadamu ili tuonyane sisi kwa sisi na kufundishana hata katika udhaifu wetu kwasababu maisha ya duniani yaliandaliwa kwaajili ya Mwanadamu na Mungu ajidhihirishe katikati yao wenyewe.

“Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.” WAKOLOSAI 3:16-17

Hatupaswi kuamini kila roho kiholela. Biblia inasema;

“ Wapenzi msiamini kila roho bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwasababu manabii wengi wa uongo wametokea duniani.” 1 YOHANA 4:1-2
Hebu toa reference za hekaya zote afu ndo uongee na Mimi
 
Lazaro alifufuliwa na Yesu (Soma YOHANA 11) Yesu alipokufa, siku ya tatu alifufuka na alikaa tena Duniani kwa siku 40 kabla ya kupaa. Hujui maandiko wala historia unakuja kwenye mjadala kubwabwaja?!
Maandiko? Historia? We umesoma historia mpaka form 4 ushawahi fundishwa mtu kufufuka Palestine katika century ya 1
 
Mwamposa hana lolote ni tapeli tu kama matapeli wengine tuwajuao mjini plus na ujinga wa waumini.

Wakati wewe unamuona tapeli, kuna watu wanapokea miujiza na baraka za Mungu kupitia yeye. Watu wanapona, wanapata kazi, wanafunguliwa kiuchumi etc! Kutoamini kwako haitokufanya uonekane mjanja au mwerevu kuliko wengine maana njia zako hazina manufaa kwa yoyote.
 
Yesu Anaweza yote Kwa wanaomwamini halazimishi mtu

Aliye hospitali anaamini dawa zaidi haiwezekani umfuate hospital mtu ana Imani kwenye dawa
Kote duniani Kuna uponyaji aina mbili wa Hospital na spiritual Healing .Mtu mwenyewe huamua aende wapi Huwa hawaingiliani
Una kichwa kizito sana,, mgonjwa yupo ICU au wodi ya kawaida na ameshatumia dawa za kila aina but hakuna unafuu anaoupata, ataendelea kuwa na imani na hizo dawa??

Kesho asikie kuna mtume au nabii anaenda kufanya uponyaji hospitali aliyolazwa, je atashindwa kuwa na hata chembe ya imani kwamba anaenda kupona sasa???
 
Maandiko? Historia? We umesoma historia mpaka form 4 ushawahi fundishwa mtu kufufuka Palestine katika century ya 1

Kwahiyo uliposoma vitabu vya mitaala (vitabu vichache vilivyochaguliwa na Serikali vitumike kufundishia mashuleni) ukawa umemaliza hapo?[emoji28] yani unasoma summary ya history unasema umesoma historia? Kukusaidia tu, tafuta vitabu vya Jewish Historian, JOSEPHUS. Utasoma humo habari za kufufuka kwa Kristo
 
Hebu toa reference za hekaya zote afu ndo uongee na Mimi

Wasomi huzungumza kwa reference. Kama huna source ya taarifa zako hatuwezi kuendelea na huu mjadala maana utakua unaongea hisia zako na sio maarifa. Subiri mijadala ya Mapenzi maana huko ndo hisia zinahitajika zaidi. Lakini hapa tunataka source ya taarifa zako.
 
Hata ukitukana matusi yote unayoyajua,huwezi kuubadili ukweli uliopo,kuna watu wanapona shida zao kwa Mwamposya,tena shida zilizowasumbua kwa miaka mingi,wakati nyinyi wenye kiburi cha uzima mnaendelea kupikiana majungu,waacheni wenye shida zao waendelee,kufunguliwa.
Aende Muhimbili hospital akawaponye ndugu zetu pale kama kweli ni nabii, mwamposa ni tapeli mkubwa
 
Anayeponya ni Mungu sio Mwamposa. Na miujiza sio maonyesho ya mazingaombwe kwamba unataka tu uone ufurahishe macho yako. Kila jambo hutendeka kwa kusudi la Mungu.
 
Wakati wewe unamuona tapeli, kuna watu wanapokea miujiza na baraka za Mungu kupitia yeye. Watu wanapona, wanapata kazi, wanafunguliwa kiuchumi etc! Kutoamini kwako haitokufanya uonekane mjanja au mwerevu kuliko wengine maana njia zako hazina manufaa kwa yoyote.
Sawa kabisa. Ila mimi daima naamini ni tapeli mkubwa na wanaomuamini wako brainwashed.
 
Back
Top Bottom