Kwanini Mwamposa asiende kwenye mahosiptali kuombea wagonjwa na tukaona wanapona?

Kwanini Mwamposa asiende kwenye mahosiptali kuombea wagonjwa na tukaona wanapona?

Anayetoa na kusmba huduma ni mwamposa au mgongwa?

Hivi baada ya huyo yesu na muhamadi kuna WATUME na MANABII wengine waliozaliwa MBEYA?
Wajinga ndiyo waliwao!!

Kuna kizazi kinaweza kuishi bila unabii katika maisha ya kiroho? Mitume na Manabii wapo maana pasipo hao hatuwezi kujua wala kusikia Maono ya Mungu kwenye maisha yetu.
 
Si kila jambo uondoka kwa maombi, mengine ni kwa maarifa tu.
Huwezi omba kazi umelala

Maombi ni msingi wa kila kitu. Kama ambavyo huwezi kuomba kazi huku umelala vivyo hivyo huwezi tafuta kazi bila kuomba. Utaswampa mpaka uote sugu za kisigino
 
Mimi nina tatizo flani naumwa

Nimezunguka kwa hao wote mnaoita ni manabii na waombeaji.

Nimepakwa mafuta ya upako nmeombewa sana kwa miaka mingi. Mpaka nikakata tamaa

Nawahakikishia wenye matatizo halisi hawaponi. Wanaotoa shuhuda wamepangwa ili sisi wenye matatizo halisi tupigwe pesa.

Wale wengine atakuja siku ya kwanza anaombewa anapona ndio wanawaonesha kwenye TV

Sisi ambao hatuponi unaambiwa huna imani na haujaokoka ndo mana haujapona (wakati kwenye ushuhuda unakuta mpaka malaya wamepona) kwahio wanakupangia ratiba ya mafundisho kuongeza imani yako na kuokoka utakua unaenda kila siku na matukio yote utaambiwa uwe unahudhuria.

Utaliwa pesa mpaka uchoke.

Kama huamini mpeleke ndugu yako ambae anaumwa serious kwelikweli muone kama atapona.

For years nmehangaika mpaka nmejifunza kuishi nalo. Maana wote ni walewale tu utapoteza muda na pesa.

Hata hao mnaowasifiaga hapa ni waongo tu.

Take it or leave it ila me naongelea my personal experience. Hili tatizo nnalo since 2008, now nmejifunza kuishi nalo tu
Pole sana mkuu,mtegemee Mungu utapona achana na hao matapeli kwenye makanisa
 
Anaweza yote Kwa wanaomwamini halazimishi mtu

Aliye hospitali anaamini dawa zaidi haiwezekani unfuate hospital mtu ana Imani kwenye dawa
Kote duniani Kuna uponyaji aina mbili wa Hospital na spiritual Healing .Mtu mwenyewe huamua aende wapi Huwa hawaingilia
Ona hili zuzu
 
Mimi nina tatizo flani naumwa

Nimezunguka kwa hao wote mnaoita ni manabii na waombeaji.

Nimepakwa mafuta ya upako nmeombewa sana kwa miaka mingi. Mpaka nikakata tamaa

Nawahakikishia wenye matatizo halisi hawaponi. Wanaotoa shuhuda wamepangwa ili sisi wenye matatizo halisi tupigwe pesa.

Wale wengine atakuja siku ya kwanza anaombewa anapona ndio wanawaonesha kwenye TV

Sisi ambao hatuponi unaambiwa huna imani na haujaokoka ndo mana haujapona (wakati kwenye ushuhuda unakuta mpaka malaya wamepona) kwahio wanakupangia ratiba ya mafundisho kuongeza imani yako na kuokoka utakua unaenda kila siku na matukio yote utaambiwa uwe unahudhuria.

Utaliwa pesa mpaka uchoke.

Kama huamini mpeleke ndugu yako ambae anaumwa serious kwelikweli muone kama atapona.

For years nmehangaika mpaka nmejifunza kuishi nalo. Maana wote ni walewale tu utapoteza muda na pesa.

Hata hao mnaowasifiaga hapa ni waongo tu.

Take it or leave it ila me naongelea my personal experience. Hili tatizo nnalo since 2008, now nmejifunza kuishi nalo tu

Don’t give up on God. Muujiza wako usitake ufanane na wa mwengine kwasababu kila mtu analo kusudi lake. Kwenye Biblia kuna Mwanamke alitokwa damu miaka 12. She waited for 12 years to see her miracle. Sarah & Abraham waited for 90+ years kupata mtoto. Pale ambapo God seems not to make sense anymore, ndo muda ambapo anadhihirika.
 
Anaye hitaji maombi anaenda mwenyewe kuombewa huko kunako husika.
Benki zinawafuata wateja wake.

Hata watumishi wa Mungu pia wanawafuataga wateja wao pale inapobidi.
Kuna mikutano mingi ya Injiri inaandaliwa siku zote na wanaohitaji mahubiri wanashiriki kikamilifu.

Ukitaka mkopo Benki lazima wewe binafsi uende Benki kukamilisha maombi yako na Kamwe pale kwenye mafundisho Yao huwezi kuletewa pesa

Mambo ya Roho Mtakatifu wanayafahamu wahusika na wanayaamini.

Wanaohitaji maombezi wanayapata na wanaridhika. Hata huko Benki sio kila Mteja anaweza pata pesa.
Ni lazima vigezo vya kupata pesa vitimizwe.

Kuwakashifu watumishi wa Mungu ni kukosa maadili.

Wakashifuji wapo tu hata Yesu Mwenyewe alikashifiwa.

Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza, ni vema kuuliza kuliko kujifanya mjuaji.

Hakuna mtu aliyekuwa na nia ya maombezi akayakosa, na maombi hayalazimishwi.

Nenda sehemu husika, fuata vigezo utapata maombezi sahihi. Haya Mambo ni ya Kiimani na sio ya Kisayansi.

Na hata hiyo sayansi hadi leo imeshindwa kutimiza mahitaji ya Binadamu.

Haspitali zipo na kila siku vifo vinatokea huko Mahospitalini.

Je tuwakashifu Wataalamu wa afya kwa kusababisha vifo?

Ulimwengu una kanuni zake, na bado haujatoa majibu ya ustawi wa Binadamu, zaidi ya kuleta unafuu mchache kwa wachache.

Kama mtu haamini Mambo ya Dini hana sababu ya kusifu au kukebehi Mambo ya Dini.
Hujajibu maswali niliyoweka haya good day
 
Kuna kizazi kinaweza kuishi bila unabii katika maisha ya kiroho? Mitume na Manabii wapo maana pasipo hao hatuwezi kujua wala kusikia Maono ya Mungu kwenye maisha yetu.
Why Mungu asikutokee wewe akakupa maono... mbona Mungu anamtegemea binadamu ili asambaze ujumbe na sisi wote tumuamini tu huyo binadama kiholelaholela
 
Kuna kapicha kalisambaaga mtandaoni kakionyesha mchungaji anaeweza kufufua watu kama skosei ni gwajima akiwa anatoa heshima za mwisho kwenye jeneza la mama yake sasa kwa jinsi kila mmoja wetu anavyompenda mama yake kwann jamaa asimfufue kama kweli anafufua wafu wanakuja kutoa ushuhuda. Akili kichwani sio kila kitu ni kweli mambo kibao ni maigizo.

Kuna mchungaji yupo maweni kigamboni anakuja bondeni anachukua mateja anawapa nguo safi wanaoga vizuri wanaenda kutoa ushuhuda wakimaliza anawapa chakula nq pesa wanasepa. Nyie mnabaki kujua ni kweli kumbe mateja wa bondeni wamekusanywa
 
Kuna kifo mpango wa Mungu na Kuna kifo mpango wa wanadamu.
Wanaofufuliwa ni WA mpango wa binadamu hata mganga tu anao uwezo wa kumfufua aliyekufa kwa mpango wa wanadamu.
Soma aina za Vifo utaelewa.
Hilo la mateja Kila penye original feki hawakosekani kama hauna maarifa huwezi watofautisha
 
Pana mitume na manabii wa ukwel na wa uongo Pana magonjwa ya kiroho,ya kimwili,ya tabia.
Pana kuumwa kwa mpango wa Mungu na Kwa wanadamu.
 
Shetani ndie uleta magonjwa, kwann Tza hawakuathirika sana na corona jibu ni maombi
Coz rais wako alificha data na ukweli kuhusu athari zake.. ni strategy nzuri ya kutumia dini coz ndo upumbavu wa wabongo ulipo so nae akapita mulemule...
 
Kuna jamaa alipanda daladala jioni mida ya buguruni watu wamenasa kwenye foleni muda mrefu halafu wamechoka kinyama, si akataka kuanza kuhubiri bhana.... Bila kujali imani zao abiria wote walimgeukia na kumfokea kwa sauti "ebu usitupigie kelele" jamaa akaamua kushuka tu.
 
😅Hee hayo mambo ya quantum physics na yesu hebu niache mi simo huku
Jiongeze katika elimu ya quantum mechanics ( quantum physics) mambo mengi yanayosemwa ni ya kiroho utayaelewa vizuri tu. Mungu hakutuumba tusiwe na uelewa kuhusu mambo yake.
 
Back
Top Bottom