Anaye hitaji maombi anaenda mwenyewe kuombewa huko kunako husika.
Benki zinawafuata wateja wake.
Hata watumishi wa Mungu pia wanawafuataga wateja wao pale inapobidi.
Kuna mikutano mingi ya Injiri inaandaliwa siku zote na wanaohitaji mahubiri wanashiriki kikamilifu.
Ukitaka mkopo Benki lazima wewe binafsi uende Benki kukamilisha maombi yako na Kamwe pale kwenye mafundisho Yao huwezi kuletewa pesa
Mambo ya Roho Mtakatifu wanayafahamu wahusika na wanayaamini.
Wanaohitaji maombezi wanayapata na wanaridhika. Hata huko Benki sio kila Mteja anaweza pata pesa.
Ni lazima vigezo vya kupata pesa vitimizwe.
Kuwakashifu watumishi wa Mungu ni kukosa maadili.
Wakashifuji wapo tu hata Yesu Mwenyewe alikashifiwa.
Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza, ni vema kuuliza kuliko kujifanya mjuaji.
Hakuna mtu aliyekuwa na nia ya maombezi akayakosa, na maombi hayalazimishwi.
Nenda sehemu husika, fuata vigezo utapata maombezi sahihi. Haya Mambo ni ya Kiimani na sio ya Kisayansi.
Na hata hiyo sayansi hadi leo imeshindwa kutimiza mahitaji ya Binadamu.
Haspitali zipo na kila siku vifo vinatokea huko Mahospitalini.
Je tuwakashifu Wataalamu wa afya kwa kusababisha vifo?
Ulimwengu una kanuni zake, na bado haujatoa majibu ya ustawi wa Binadamu, zaidi ya kuleta unafuu mchache kwa wachache.
Kama mtu haamini Mambo ya Dini hana sababu ya kusifu au kukebehi Mambo ya Dini.