Kwanini Mwanza Wanauza magari bei rahisi kuliko Dar es Salaam?

Kwanini Mwanza Wanauza magari bei rahisi kuliko Dar es Salaam?

Gari za Mwanza ni bei chee kweli shida ni wamiliki wa magar huko hawajui kuyatunza
Unakuta gari mtu anatembelea vioo wazi ili aonekane na watu wakat gar ina ac inasababisha ichoke ndani mapema
Unakuta mtu hajui mambo ya kufanya service gari inakufa vipur ye yuko tu anakomaa so unashangaa gari mpya inaanza kumsumbua

Yes gari za mwanza used ni cheap but ukibahatisha ambayo haisumbui shukuru Mungu

Oh kumbe sababu ni magari yao mabovu kutokana na utunzaji mbovu. Nashukuru kwa kunielewesha.

Ingawa nina watu wangu kadhaa wamenunu mwanza na zipo very clean… nitaendelea kufuatilia kwa watu wengi zaidi ili nisije kuingizwa chaka na gari zao
 
Ni kawaida miji mikubwa Bei zinatofautiana na miji mingine
Sio kwa kila kitu hapana
Ila upande wa magari Bei huwa kubwa kwa sababu ya madalali na vipato vikubwa pia vinachangia

Hapa nilipo magari huwa yapo juu ila nikienda nje ya mji sana yanakuwa chini zaidi
 
Hio ni sababu ya kijinga kusema gari mbovu, unless useme unanunua namba A mwanza.

Ila kama utanunua gari DZL leo hii Mwanza lazma utaikuta iko in clean condition. Mwanza watu wana hela ya kubadili magari so hawana tamaa. Ni jamii tu ya watu wa kule.
 
Hapa nimekupata vizuri kabisa, hii nadhani ni moja ya sababu za msingi za tofauti hizi za bei
 
Af unakuta kila dalali kaweka laki 5 juu [emoji3][emoji3][emoji3] mwisho wa siku gari unakuta bei juu sana. Gari ya 15m kwa mwenyewe dalali unakuta analiuza 18M kumbe kuna cheni ya watu 6.

Hahhahah alafu wanakwambia, AC mpaka unaganda, chuma anaisukuma mwanamke wa kihindi anataka kurudi kwao fasta[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Habari za asubuhi wakuu.

Kwa muda kidogo nimekua nikifanya utafiti mdogo wa madalali wauzaji wa magari instagram na social media nyingine.

Kuna kitu nimegundua nikaona nijadiliane nipate majibu sahihi.

Nimeona madalali wa mwanza wanauza gari kwa bei rahisi sana ukilinganisha na wa Dar es Salaam (kwa gari zenye specificationa sawa)

Mfano
Toyota crown
mwanza nakuta nyingi average milion 8 (zinaanza 7m mpaka 10m hivi) ila dar es salaam average milion 11 (zinaanzia 10m mpaka 13m)

Toyota mark x
Mwanza around 5.5m mpaka 7m, ila Dar es salaam around 8m mpaka 11m

Toyota kluger
Mwanza 9m mpaka 14m.. ila Dar es salaam 14 mpaka 18

Toyota harrier tako la nyani
Mwanza 14m mpaka 18m
Dar 16 - 22m

Sasa ndugu zangu naomba kujua sababu ya utofauti huu mkubwa wa bei! Je madalali wa Dar ni kwamba wanapiga cha juu kingi au watu wa mwanza wana pesa sana ndio sababu wanauza bei ndogo?

Maana nimeshawishika kidogo kununua harrier kwa hawa jamaa wa Mwanza maana bei zao kitonga sana.

Nawasilisha
Kingine gari ukiipata direct kwa mmiliki inakuwa bei chee sana. Wanachofanya Dar kuna ile wanaita kulenga, dalali anainunua gari kwa tajiri lets say kwa 8m-9m kisha anauza 11m.

Sasa wakiongezeka madalali wenzie lazma waongeze cha juu ndio unakuta gari inafika 12.5m
 
Hio ni sababu ya kijinga kusema gari mbovu, unless useme unanunua namba A mwanza.

Ila kama utanunua gari DZL leo hii Mwanza lazma utaikuta iko in clean condition. Mwanza watu wana hela ya kubadili magari so hawana tamaa. Ni jamii tu ya watu wa kule.

Yes! ndio maana hapo nikamuuliza mkuu hapo mbona unakuta nyingine ni very clean, na pia nna wadau kadhaa wamenunua huko na ziko very clean.
 
Kingine gari ukiipata direct kwa mmiliki inakuwa bei chee sana. Wanachofanya Dar kuna ile wanaita kulenga, dalali anainunua gari kwa tajiri lets say kwa 8m-9m kisha anauza 11m.

Sasa wakiongezeka madalali wenzie lazma waongeze cha juu ndio unakuta gari inafika 12.5m

Dah aiseeh hapo kuipata gari straight kwa mmiliki ndio changamoto ilipo.

Unaeza kutusaidia mbinu gani tunaweza tumia kuwakepa madalali, kumpata mmiliki moja kwa moja?

Maana unaweza kuta unaliwa zaidi ya 4m na madalali
 
Back
Top Bottom