Kwanini Mwekezaji mpya wa Mabasi ya Mwendokasi (DART) Kampuni ya Emirates National Group kutoka Falme za Kiarabu kachelewa kuanza kazi?

Kwanini Mwekezaji mpya wa Mabasi ya Mwendokasi (DART) Kampuni ya Emirates National Group kutoka Falme za Kiarabu kachelewa kuanza kazi?

Hata Richmond alikujaga muarab jeneral wa jeshi mstaafu akawa mmiliki baada ya bunge kutaka kujua mmiliki.
Exactly. Viongozi walikuwa wanatuona mafala. Halafu huyo jenerali akawa hataki kuonekana sura yake.
 
Mwekezaji huyo Mwarabu aanze haraka , huduma ya mabasi ya mwendokasi ni mbaya mno mabasi ni machache sana na yanajaza kupita kiasi. Hii ni hatari sana kwa afya mtu mwenye kifua Kikuu anaweza kuambukiza basi zima maana hata kupumua ni shida ndani ya basi.
Mabasi mengi ni express vituo vingi hayasimami kabisa kama Usalama, Mwembechai, Kagera nk.
Mabasi ya kwenda Muhimbili asubuhi ni machache sana yakuhesabu.
Yaani huu usafiri ni kero mno kwasasa waendeshaji wamefeli pakubwa , kwasasa ukiingia kituo cha katikati unaweza kukaa saa nzima bila kupata usafiri.
Kweli hiki chama chetu kimechoka hata usafiri tu wameshindwa kusimamia shame on them!
 
Ikifika hapo kila abiria atakaa kwenye seat yake
Huo ndio utaratibu tunaoutaka na kwa kuwa watakuwa na tank zao za mafuta kigamboni basi shughuli itakuwa nyepesi kuliko hawa wanaolalamika uendeshaji ni mgumu wakati barabara yote ni yao na abiria wote ni wao hawana mpinzani
 
Hivi kweli hakuna Wazawa ambao wanaweza kuwekeza kwenye Mradi huu?
Mf.Abood, Shabiby,nk
Shida ya wazawa ni uswahili tu. Kutakuwa hamna tofauti ni kama mtu aliyegeuza kofia kutoka mbele na kuielekezea nyuma.
 
Inawezekana anazungushwa kwa kuwa hajatoa 'kitu kdg' kama kawaida ya wanaoidhinisha!
Si akaombe uzoefu kwa "ze dP"
 
Kuna watu wakacoment hii thread kama mtoa thread ana akili nzuri😂😂😂😂... Kiko wapi?
 
Gazeti la Mwananchi la 31 Oktoba 2022 liliripoti habari ya kupatikana mwekezaji mpya wa kuendesha mabasi ya mwendokasi (DART), Kampuni ya Emirates National Group kutoka Falme za Kiarabu.

Taarifa ya serikali kupitia gazeti hilo ilisema kampuni hiyo ingeanza kazi Novemba 2022. Makubaliano ni kwamba; mwanzoni kampuni hiyo itaingiza mabasi 177, na ndani ya miezi 6 (kuanzia Nov 2022) itaingiza jumla ya mabasi 750. Pia, watarejesha mfumo wa malipo ya kadi pekee katika vituo vya mwendokasi.

Hata hivyo, hadi sasa wananchi hatuoni hayo mabasi mapya, hatuoni kuboreshwa kwa huduma ya usafiri wa mwendokasi na wala hatuwaoni watendaji wa Kampuni ya Emirates National Group kutoka Falme za Kiarabu.

Tatizo ni nini? Mbona wananchi hatuelezwi? Waarabu wamepatwa na nini? Kama wameshindwa hatuwezi kupata waarabu wengine wawekeze kwa kuzingatia waarabu wamefanikiwa sana katika sekta ya usafirishaji?

Information is power.

Soma DAR: DART kuondoa tiketi vituo vya Mwendokasi, malipo ya kadi kurejea
Ohooooooo
 
Back
Top Bottom