Kwanini Mwigulu akiwa na cheo Serikalini lazima awe na timu ligi kuu?

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Kipindi akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Nchi, alikuwa anamiliki timu ya Singida Utd ya pale mkoani Singida. Akajaza wachezaji wa kigeni kibao kama vile Michel Rusheshagonga, Shafik Batambuze, Tafazwa Kutinyu nk

Wadhamini nao wakajitokeza wa kutosha mpaka jezi ikawa imechafuka kwa matangazo ya wadhamini.

Miaka michache baadae akatumbuliwa na hayati Magufuli, hatimae na mrija wa pesa ukapungua, wadhamini wakajitoa Singida ikashuka na kusahaulika ligi kuu bara.

Aliporudishwa kwenye Baraza la Mawaziri enzi ya Magufuli, akakaa kwa adabu bila kujihusisha na umiliki wa timu.

Baada ya kifo cha hayati Magufuli, Mama Samia akawa Rais na kumchagua Mwigulu kuwa Waziri wa Fedha. Ndani ya mwaka mmoja tu, tayari timu yake mpya aliyoinunua ya DTB imepanda daraja huku baadhi ya wachezaji waliopandisha timu hiyo wakiwa ni wale wale waliotumika enzi ya Singida Utd.

Japo amekuwa akikanusha kuwa yeye sio mmiliki, lakini ukweli siku zote haujifichi. DTB ina mastaa kibao kama Juma Abdul, Amis Tambwe, David Mwantika, Nicholaus Gyan, Tafazwa Kutinyu, na wengineo wengi.

Hizi fedha huwa anatoa wapi? Ni kwanini huwa anamiliki akiwa na cheo tu Serikalini?
 
Kinachonikera sio suala la yeye kumiliki timu.

Ila ni jinsi DTB ilivyotumia rushwa kwa kuhonga marefa na baadhi ya timu zisizojielewa ili ipande ligi kuu.

Kuna haja ya ligi daraja la kwanza kumulikwa kwa ukaribu.
 
Kubwabwaja hakutokusaidi kitu, leta ushahidi ulivyoona anahonga timu pinzani vinginevyo kuna siku utavalishwa dela.
 
Kinachonikera sio suala la yeye kumiliki timu.

Ila ni jinsi DTB ilivyotumia rushwa kwa kuhonga marefa na baadhi ya timu zisizojielewa ili ipande ligi kuu.

Kuna haja ya ligi daraja la kwanza kumulikwa kwa ukaribu.
Kama ushahidi unao peleka TAKUKURU
 
Na home ground yake ni uwanja wa LIT (Namfua)
 
Kaa kwa upole ma gap ya upigaji ni mengi sana kwa wateule wachache.
Hata yanga sasa hivi huwaambii kitu.

Ukisikia symbion analipwa bilioni 350 ujue hizi hizi pesa ndio zinatumika kwenye starehe za wateule.

Katika mambo yote,sitamuelewa mama kabisa kwa kumteua Mwigulu kwa waziri wa fedha.
 
Hii si inamilikiwa na benki ya DIAMOND TRUST?..... Sidhani kama anahusika nayo.....Hata Singida United, Mwigulu hakuwa mmiliki wake.. Walikuwepo wakina Yusufu na Mo nao waliisaidia kupanda daraja... Mo alivyopata dili la kuinunua Simba, Ndio akaitelekeza Singida United... Si tuliokuwa Singida tunaelewa kilichokuwa kinaendelea pale Singida United.
 
Hiyo haimilikiwa na bank, ilishauzwa iko chini ya watu binafsi, inasemekana kina hao hao mleta mada aliowataja. Hata assets wanazotumia kwa sasa kama basi ni lile lile la Singida united wame re-rebland tu.

Singida united ilikuwa timu ya Mwigulu, Mo alikuwa anasaidia tu. Ndio maana Mwigulu alikuwa anaamua tu kufanya anachotaka, kuna siku alimtoa Faisal Salum kama zawadi kwenda yanga, the fall of Mwigulu Nchemba ikawa the fall of Singida united hauwezi hata kurelate?
 
Kinachonikera sio suala la yeye kumiliki timu.

Ila ni jinsi DTB ilivyotumia rushwa kwa kuhonga marefa na baadhi ya timu zisizojielewa ili ipande ligi kuu.

Kuna haja ya ligi daraja la kwanza kumulikwa kwa ukaribu.
Kama hupeleki ushahidi TAKUKURU basi utaendelea kukereka tu
 
Si kweli, Singida United ilikuwa ya MO, Hata ilo basi walipewa na MO,... MO aliporudi Simba akaitelekeza Singida United, Ndio chanzo cha anguko lake....
 
Wamiliki wa hiyo Benk unawajua?. Kazi ya mke wa Mwigullu unaijua?.
Kwa taarifa yako, Baada ya Singida utd kushuka daraja. Mwigulu ndio alieinunua Mawenzi Market ya Morogoro na kuihamishia Singida na sasa ndio imebadilishwa jina ndio hiyo inaitwa DTB. Inshu nyingine ya uendeshaji wa timu anajua kamkabidhi nani.
 
Naunga hoja mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…