Kwanini Mwigulu akiwa na cheo Serikalini lazima awe na timu ligi kuu?

Kwanini Mwigulu akiwa na cheo Serikalini lazima awe na timu ligi kuu?

Wamiliki wa hiyo Benk unawajua?. Kazi ya mke wa Mwigullu unaijua?.
Kwa taarifa yako, Baada ya Singida utd kushuka daraja. Mwigulu ndio alieinunua Mawenzi Market ya Morogoro na kuihamishia Singida na sasa ndio imebadilishwa jina ndio hiyo inaitwa DTB. Inshu nyingine ya uendeshaji wa timu anajua kamkabidhi nani.
Benki ya DTB ni ya wahindi naijua toka miaka ya 2000 huko... Mwigulu hana hela ya kumiliki timu,.... MO mwenyewe African Lyon ilimshinda, Unadhani kumiliki timu mchezo?
 
Ccm ina wenyewe
Hakikisha unapata pesa ili maisha ya familia yako yawe mazuri, huku kuhoji hoji na kulalamika haitakusaidia kitu maana walioshika mpini ndio hao kwa sasa
Umenena la maana, hakuna mwanaharakati tajiri
 
Hiyo haimilikiwa na bank, ilishauzwa iko chini ya watu binafsi, inasemekana kina hao hao mleta mada aliowataja. Hata assets wanazotumia kwa sasa kama basi ni lile lile la singida united wame re-rebland tu.

View attachment 2228771
Songida united ilikuwa timu ya mwigulu, mo alikuwa anasaidia tu. Ndio maana mwigulu alikuwa anaamua tu kufanya anachotaka, kuna siku alimtoa faisal salum kama zawadi kwenda yanga, the fall of mwigulu mchemba ikawa the fall of singida united hauwezi hata kurelate?
Ahsante mkuu kwa kuleta ushahidi mzuri
 
Kipindi akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Nchi, alikuwa anamiliki timu ya Singida Utd ya pale mkoani Singida. Akajaza wachezaji wa kigeni kibao kama vile Michel Rusheshagonga, Shafik Batambuze, Tafazwa Kutinyu nk

Wadhamini nao wakajitokeza wa kutosha mpaka jezi ikawa imechafuka kwa matangazo ya wadhamini.

Miaka michache baadae akatumbuliwa na hayati Magufuli, hatimae na mrija wa pesa ukapungua, wadhamini wakajitoa Singida ikashuka na kusahaulika ligi kuu bara.

Aliporudishwa kwenye Baraza la Mawaziri enzi ya Magufuli, akakaa kwa adabu bila kujihusisha na umiliki wa timu.

Baada ya kifo cha hayati Magufuli, Mama Samia akawa Rais na kumchagua Mwigulu kuwa Waziri wa Fedha. Ndani ya mwaka mmoja tu, tayari timu yake mpya aliyoinunua ya DTB imepanda daraja huku baadhi ya wachezaji waliopandisha timu hiyo wakiwa ni wale wale waliotumika enzi ya Singida Utd.

Japo amekuwa akikanusha kuwa yeye sio mmiliki, lakini ukweli siku zote haujifichi. DTB ina mastaa kibao kama Juma Abdul, Amis Tambwe, David Mwantika, Nicholaus Gyan, Tafazwa Kutinyu, na wengineo wengi.

Hizi fedha huwa anatoa wapi? Ni kwanini huwa ana miliki akiwa na cheo tu serikalini?
Hata PM anamiliki Namungo
 
Imani yako baki nayo ila mimi namjua alieinunua timu ya Mawenzi Market na mgao nimeupata kwa kuwa nilikuwa mwanachama wa timu.
Mkuu...kama Mwigulu aliinunua Mawenzi Market, akaibadilisha jina., kwa nini iitwe DTB( Diamond Trust Bank) DTB tumeifuatilia toka inaanza ligi, viongozi wake ni kutoka benki ya DTB. .
 
Si kweli, Singida United ilikuwa ya MO, Hata ilo basi walipewa na MO,... MO aliporudi Simba akaitelekeza Singida United, Ndio chanzo cha anguko lake....
Timu ambayo imewahi kumilikiwa na Mo befire simba ni African lion, Hiyo singida haijawqhi kumilikiwa na Mo hata kwenye udhamini tu hakuwepo. Hii singida ni ya juzi tu wakati mo tayari muda mrefu yupo simba. Kwa hiyo unaamini Mo anaimiliki singida na hakuna hata bidhaa yake moja kwenye sponsorship. Sungida ilikuwa na wadhamini wengi ila sio Mo. Nakataa.

SING12-600x514.jpg
 
Hiyo haimilikiwa na bank, ilishauzwa iko chini ya watu binafsi, inasemekana kina hao hao mleta mada aliowataja. Hata assets wanazotumia kwa sasa kama basi ni lile lile la singida united wame re-rebland tu.

View attachment 2228771
Songida united ilikuwa timu ya mwigulu, mo alikuwa anasaidia tu. Ndio maana mwigulu alikuwa anaamua tu kufanya anachotaka, kuna siku alimtoa faisal salum kama zawadi kwenda yanga, the fall of mwigulu mchemba ikawa the fall of singida united hauwezi hata kurelate?
Basi lao kila siku naliona limepaki kwenye petrol station Kinyerezi
 
Benki ya DTB ni ya wahindi naijua toka miaka ya 2000 huko... Mwigulu hana hela ya kumiliki timu,.... MO mwenyewe African Lyon ilimshinda, Unadhani kumiliki timu mchezo?
Acha kukaza fuvu wahindi walishamuuzia Mwigulu. Mimi nina washkaji wafanyakazi na wachezaji wa hiyo timu kabla haijauzwa.
Mwigulu hana hela lakini ana back-up ya wadau kusaidia uendeshaji wa timu. Nayajua haya kupitia mheshimiwa fulani jinsi alivyokua anawatumia wafanyabiashara kuisaidia timu fulani premier league.
 
Sisi singida big star fc tutamfunga yoyote ataekuja mbele yetu isipokuwa Yanga
 
Hii si inamilikiwa na benki ya DIAMOND TRUST?..... Sidhani kama anahusika nayo.....Hata Singida United , Mwigulu hakuwa mmiliki wake.. Walikuwepo wakina Yusufu na Mo nao waliisaidia kupanda daraja...Mo alivyopata dili la kuinunua Simba, Ndio akaitelekeza Singida United...Si tuliokuwa Singida tunaelewa kilichokuwa kinaendelea pale Singida United.
Baada ya DTB leo kubadili jiba na kujiita Singida Big Star bado una hoja zako hizi?
 
Back
Top Bottom