Kwanini Mwl Nyerere hakuweka ukweli hadharani juu ya kifo cha Kassim Hanga? Mbona CCM huwa hawataki ukweli kuhusu mauaji ya Kassim Hanga kuwa wazi?

Siku ya mwisho kasimu kuonekana ilikuwa hapo bustani ya mnazi mmoja mbele ya kibarua bar kakangu Mohamed said alikuwapo,Nyerere alimrudisha Zanzibar na karume akafanya yake,tunapoishi mambo ya vifo yanawafaa wengine tu.
Aliwarudisha Zanzibar Hanga na Othman Sharif. Alitoa sababu zake kwenye mkutano wa hadhara hapa Dar (kuna picha ipo humu kwenye mitandao)
 
Shukrani nyingi sana poti.
 
Mbona hii inafahamika, aliuawa na serikali ya Karume bila kesi kwa tuhuma za kutaka kumpindua. Karume alimwaga damu za watu wengi mno, mwisho wa siku ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga.
 
Rais wa JMT ana mamlaka makubwa kuliko rais wa SMZ.

Ishu ya kiongozi wa serikali kuuwawa unalinganisha na matukio ya kuvunja mlango?
Ndio nakuonyesha kua kuna ngazi za kufuata huwezi ukaacha kumtaja kiongozi wa nchi /serikali husika, kumbuka ile ni nchi kamili ina Rais kamili kama ulikua hujui au labda huelewi majukumu yake wewe. Halafu viongozi wa selikali za vitaa hawashughuliki na kesi za kuvunja milango pekee hata za mauwaji pia kama ulikua hufahamu.
Mgawanyo wa majukumu wa viongozi wa serikali unamaana yake
 
Daaa!! weye jamaa sasa haya yooote uliyajuaje mkuu!! au na wewe ulikuwa mmoja wao, make ulivo yapangilia???heee!!...km ni kweli baasi siasa ni mchezo mchafu!
 
Swali, je kuua mtu ni kwa maslahi ya nchi au viongozi?

Ukiangalia kwa makini hakuna taifa linalotaka watu wake wafe, bali ni insecurities za viongozi zinazosababisha maafa.

Tuwe wazalendo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…