Sasa wewe tufanye ni msomi. Niambie nchi imeuzwaje?
Usikimbie!
Imeuzwa kupitia mkataba wa 25.10.2022 mkataba ambao uliridhiwa na Bunge 10.06.2023. Ndani ya mkataba huo mwarabu anapewa haki za kipekee za kumiliki njia kuu za uzalishaji mali hususani bandari, maeneo ya biashara na ardhi.
Mkataba huo unampa mamlaka ya kuendelea, kujenga, kuendesha na kuendeleza bandari zote za Tanganyika, shughuli za kuratibu mizigo (logistics centers ambazo sasa zinafanywa na clearing and forward agents), special economic zones (hata mlima Kilimanjaro unaingia hapa, mbuga za wa nyama na madini zinaingaia hapa), trade center kama Kariakoo, Mwanza, Arusha unduma, strategic infrastructure kama SGR, Barabara na madaraja, trade corridors kama maeneo ya Hororiri, Sirari, Tunduma)!
Lakini pia amepewa haki za kumiliki ardhi aitakayo na serikali italazimika kuwapa ardhi hiyo hata kama INA watu basi serikali itapaswa kuwafukuza watu hao ili mwarabu akae. Na akiimiliki ardhi akaanza kujichimbia madini yaliyoko ardhini hatupaswi kumuuliza).
Hayo yote amekabidhi kuanzia tarehe tajwa hadi mwisho wa dunia.
Lakini katika hayo yote mgao wa Tanzania hauwekwi wazi.
Hebu sasa na wewe tuambie, kwa nini unashikilia hoja kuwa nchi haijauzwa?