Kwanini namuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan?

Kwanini namuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan?

Sio najisifu ila kwa miaka 47 hadi sasa nimemsliza hati za kusafiri 4. Wewe Je?
Hiyo wadanganye wengine sio mimi.

Ila naona sasa umepata ajira ile taasisi ya kusajili makampuni una pata pata muda wa kuingia JF maana pale kwenye law firm walikua wanakubana sana.
 
Hiyo wadanganye wengine sio mimi.

Ila naona sasa umepata ajira ile taasisi ya kusajili makampuni una pata pata muda wa kuingia JF maana pale kwenye law firm walikua wanakubana sana.
Itabidi siku nikulipie ticket na visa ukatoe ushamba ndugu yangu. Ukitoka kidogo nje ya Tz, akili itafunguka
 
Wabongo sijui tukoje yani huwa tunamkubali kiongozi mazima au kumkataa mazima, mtu akishakwambi anamkubali kiongozi fulani basi hukuti tena akimkosoa anakubali kila jambo kutoka kwa kiongoz huyo na humtetea kwa yale yote yenye kumkosoa huyo kiongozi.

Yani unakuta mtu kavutiwa na sera fulani kutoka kwa huyo kiongozi basi tena ndio anamuunga mkono kwa kila jambo ameshakuwa kiongozi bora na kila anachofanya ni sahihi.
 
Kumekuwa na maneno maneno humu kuwa mimi na wenzangu tunaomuunga mkono Rais Samia basi kama sio Waislamu basi ni Wazanzibar na kama hauko kote huko basi wewe ni chawa wake.

Hizi ni siasa za majitaka ambazo kusema kweli zimeegemea kwenye vihoja badala ya hoja.

Kwa upande wangu Mimi Lord Denning, mimi sio wa asili wa Zanzibar wala sio muislamu. Ni mkristo mkatoliki na kusema kweli simjui Rais Samia, Sijawahi onana nae na wala hanijui.

Katika uzoefu wangu wa kufuatilia siasa za dunia ikiwemo Afrika na Tanzania naweza kusema Mimi Lord Denning naweza kuwa mmoja wa watu wachache sana wanaoifahamu dunia na siasa zake. Kwa umri wangu wa miaka 47 sasa nimeenda nchi nyingi, karibu mabara yote. Na kote huko nilikofika nimekuwa nikijifunza sana historia ya sehemu husika, siasa zake, maisha ya watu na uchumi wao

Kwa upande wa marais wa Tanzania nimebahatika kuwepo kipindi cha Nyerere ingawa nilikuwa mdogo, kipindi cha Mwinyi nikiwa na akili, kipindi cha mkapa hadi saivi nikiwa mtu mzima na akili zangu.

Nilimkubali sana Mkapa na sera zake za kiuchumi. Nikamkubali sana Kikwete maana nae kwenye uchumi alienda sawa pamoja na kuyumba maeneo kadhaa na nikatofautiana na Magufuli hasa kwenye sera zake za kiuchumi za state capture na sasa namuunga mkono Samia kwa sababu so far nimemsoma na kumuelewa kuwa anaenda vizuri sana kwenye sera za kiuchumi.

Kwanini namuunga mkono Rais Samia?

1. Wanasiasa wengi wa nchi yetu ukiondoa Mkapa walikuwa wanaogopa kufanya maamuzi positive kweli kiuchumi kwa kuogopa siasa ila Samia hayuko hivyo. Kwa nilivyomsoma Samia, anajua sana geopolitics, anapenda vitu vizuri, ni mkisasa kweli. Kwa sasa dunia ilipo na inapokwenda fursa ziko kwenye maeneo hayo. Moja ni kwa namna gani unavyojiweka na kujitangaza vizuri na pili ni namna gani unavyojiweka kisasa. Kwa maamuzi ya kuboresha sekta nyeti za kiuchumi ikiwemo bandari, utalii tena bila kujali siasa, kusema kweli amenivutia sana.

2. Tanzania kuna wajinga wengi sana na ujinga wao umewafanya kuwa masikini sana. Katika kuwaondoa kwenye ujinga wao ni lazima uwaonyeshe kweli kuwa wanatakiwa kuondoka katika imani na mazoea ya kijinga. Kwenye hili kusema ukweli wa Mungu wangu Samia anafanya vizuri.

Mabadiliko yanayofanyika katika uendeshaji wa uchumi wetu ili kutufanya tuendeshe uchumi katika mazingira yenye ushindani ili kupata matokeo mazuri kweli yamenifanya nijitokeze wazi kumuunga mkono huyu Mama.

Tanzania shida kubwa iliyopo ni watu kutopenda ushindani. Na ndo mana ubora katika mashirika ya Umma umekuwa finyu sana. Kutufanya tuondokane na mentality hii inanifanya kumuona Rais Samia kama Rais bora zaidi kuwa nae katika kipindi hiki.

Mwisho napenda kumaliza kwa kusema uongozi na maendeleo ya kweli ni matokeo ya kutumia akili vizuri. Sio rasilimali wala sio utajiri ulio nao kama Taifa. Kuna sehemu Tanzania tunatakiwa kufika ila ili tufike lazima tutumie kweli akili zetu vizuri hasa katika kujua Dunia ipo wapi, inaenda wapi na itakuwa wapi katika siku nyingi zijazo.

Ili tufike huko lazima Watanzania tutumie akili zetu vizuri. Tuifanye nchi yetu kuwa sehemu ya mjadala wa dunia kama sehemu nzuri ya kuja, kuwekeza na kuishi ikiwemo kufanya starehe. Na ili tutimize hili lazima tuite watu wenye akili tofauti, wabadirishe fikra zetu, na watufanye tuwaze vizuri. Ni lazima tubadiri mfumo wa elimu yetu ili kutufanya tuende kama dunia inavyoenda ili tusiachwe nyuma.


Asanteni
Lord Denning
Kilimanjaro
Nidhahili umemkubali Samia kupitia point moja tu ya namba anavyojitahidi kufanya uchumi wetu uwe vizur lakini umesahau matatizo yake mengine mengi ambayo kupitia hayo ndio yanawakera sana watu mpaka wanaona hafahi kuwa rais Wala Hana capabilities tosherevu za kuwa raisi mfano hawezi kuwawajibisha mafisadi na wanadhilifu wa Mali na pesa uma, hawezi kufanya followup kwa subordinate wake na kuchukua hatuna stahiki kwa mazembe nabaya kuliko yote anabariki upigaji kwa Kila kiongozi katika eneo lake ( Kila mtu ale kwa elefu wa namba yake) ayo ni matusi kwa masikini na watu wenye Hali ya chini katika nchi hii .Huwezi sema waziwazi huo upuuzi na ukabaki salama .Nchi inashida watu nimasikini sana afu wapole sasa watanzania afu hujali Hali zao wewe unasema tu watu wale kwenye maeneo Yao? Huoo ni upuuzi na ningekua na uwezo ningeipindua hii nchi kama niger tu
 
Mkataba una shida gani?
Wewe kumbe ni mpumbavu nilikua nakuchukulia unaakili Wenda unakitu tukutazame kumbe ni mpuuzi mmoja uliejiandaa kubishana sio kuelewa.Haiwezekani Kila mtu akuambie mkataba unashida wewe useme ukataba unashida gan?
 
Wewe kumbe ni mpumbavu nilikua nakuchukulia unaakili Wenda unakitu tukutazame kumbe ni mpuuzi mmoja uliejiandaa kubishana sio kuelewa.Haiwezekani Kila mtu akuambie mkataba unashida wewe useme ukataba unashida gan?
Matusi ya nini? Sema wewe shida yake?
 
Back
Top Bottom