Kwanini naunga mkono Urusi kuchukua hatua za kijeshi Ukraine?

Inaonekana hufahamu mambo mengi katika mzozo huu.
Hujui vizuri siasa za USA na Russia.
Ungekua unajua Cuban missile crisis usingesema hayo unayosema.
 
hao watu wanaishi kule mashariki, km nia ya urusi ilikuwa ni kuwalinda andepeleka majeshi kuwalinda kulekule kwe ,majimbo ambayo urusi imeshayatambua kuwa ni huru na si kuvamia nchi yote, utakua umetumia hisia tu
 
Yericko hili bandiko lako umeonekana una bias Sana hivyo wasomaji wengi wamekupuuza Sana. Kuanzia leo mavitabu na matakataka yako sitoyasoma tena umeonekana na ushabiki una mawazo ambayo hayabalance poor you
 
I second u[emoji106]
 
Rubbish, huwa nakuunga mkono mambo mengi lakini sikuungi kwa ujinga huu wa kuua watu wasio na hatia, kama mrusi ana nguvu kwanini asiende kuvamia Marekani?
Marekani anapoua mbona kelele si nyingi?...Iraq, Libya, Syria, Afghanistan, Vietnam, etc? Hujiulizi kwa nini? Siungi mkono mauaji ya raia. Lakini hii vita imetafutwa na NATO na hasa Marekani.
 
Kama kweli wewe ni mfuatiliaji wa habari za kimataifa lazima uwe umesikia mijadala mingi tu iliyofanyika na inayoendelea kuhusu uongo na uovu uliofanywa na marekani na washirika wake huko Iraq, Afghanistan, Libya, n.k. ripoti zimetolewa na taasisi rasmi za US, UK, NGOs na wengine kuhusu ghilba zilizofanyika kuanzisha vita ya Iraq. Tony Blair na George Bush wametajwa kama war criminals.

Malalamiko kuhusu Saudi Arabia na Iran kwenye vita ya Yemen yanasikika kila mara. Vita za Syria na Ethiopia zinazungumzwa. Hakuna ujinga unaopita hapa duniani, watu wote wakakaa kimya. Wapo watakaoliamsha. Uzuri wa Marekani na Ulaya viongozi wao wanakosolewa hadharani tena kwenye media za kimataifa. Mambo yao yanachambuliwa hadharani. Hata uongo wa CIA au jeshi kama pale walipoua familia kwa drone kule Afghanistan CNN walichunguza na kuripoti kimataifa na baadaye Pentagon na State Department wakakiri kosa na kuahidi kulipa kifuta machozi.

Huko Urusi hakuna mwenye jeuri ya kumuhoji Putin kitu. Na anayemkosoa ajiandae kupakazwa au kulishwa polonium na watu wasiojulikana. Hao Warusi anaodai kuwalinda hashauriani nao chochote kwa sababu anajua hakuna ukweli zaidi ya yeye kutaka kuimarisha utawala wake mrefu wa kidikteta huko Urusi. Hayuko tayari kuona demokrasia ikistawi jirani yake halafu wananchi wake wakaanza kumhoji na kukimbia nchi.
 
Rubbish, huwa nakuunga mkono mambo mengi lakini sikuungi kwa ujinga huu wa kuua watu wasio na hatia, kama mrusi ana nguvu kwanini asiende kuvamia Marekani?
Halafu eti unaweka stand by nuclear weapons kuweza kutumika FOR WHAT!!!!!???? Rubbish,hivi huyo Putin anaakili sawa sawa hajatosheka tu alivyoimega Ukraine na kuunda vikundi vya waasi??
 
Umechambua vizuri sana Yericko. Ongeza na hoja ya Muhoozi Kainerugaba, si ya kupuuzwa.
Ubabe wa NATO na Marekani nao ni wa kihalifu. Nakumbuka ukatili na uhalifu walioufanya Libya na kwingeneko duniani. They have no moral stance and/or authority!
 
Marekani hataki mrusi aweke silaha cuba lakini anataka kumzunguka mrusi akiweka silaha nchi jirani na urusi, hii vita imetengenezwa na nato
 
Unazungumziaje matendo ya Marekani mnaemuita mama wa demokrasia kuvamia Syria, Iraq,Libya...?
 
Kwanini sisi hatuhesabiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…