Kwanini naunga mkono Urusi kuchukua hatua za kijeshi Ukraine?

Sema "... Waafrika kuungana na Putin ...". Putin hawakilishi matakwa ya Mrusi. Warusi hawamuungi mkono; hawataki vita na ndugu zao wa Ukraina. Fuatilia vizuri.
 
Mkuu Yerricko hizo logic za wapi? Ili dunia iwe salama kunatakiwa kuwa na mkubwa mmoja tu. Siyo wawili wala watatu, wala wanne. Mbona unaongea kinyumenyume?
Sasa akiwa mkubwa mmoja si ataendesha dunia kama familia yake, wenye mawazo mbadala watatokea wapi.

Sawa na kusema leo vyama vyote vya upinzani vifutwe ibaki CCM pekee, si wataongoza nchi kama gari bovu.

Kuruhusu mtu mmoja kuwa nguvu pekee sawa na kumpa mamlaka ya kidikiteta
 
Vijana wengi humu wanasikiliza BBC, CNN na vyombo vingine vya magharibi hawajishughushi kabisa kupata habari au kusoma historia ya dunia kuanzia vita ya pili ya dunia hadi vita baridi vilivyopelekea Umoja wa Urusi kusambaratika...

Wengi wao hata ukiwauliza kwa nini NK na SK zilitengana hawajui, ila wanaishi kwa propaganda za Marekani tu.
 
Pumba tupu.
 
Yericko hili bandiko lako umeonekana una bias Sana hivyo wasomaji wengi wamekupuuza Sana. Kuanzia leo mavitabu na matakataka yako sitoyasoma tena umeonekana na ushabiki una mawazo ambayo hayabalance poor you
Hata mimi jana nimechoma mavitabu yake
 
Desmond tutu alipata kusema unapokuona tembo amekanyaga panya na wewe ukawa viguvugu, panya hatokuelewa
Hakuna kitu kinaitwa vuguvugu hata Mungu alisema atawatapika.
Kuna pande mbili, either uwe upande wa Russia na anayofanya ama uwe upande wa magharibi chini ya marekani
 
Rubbish, huwa nakuunga mkono mambo mengi lakini sikuungi kwa ujinga huu wa kuua watu wasio na hatia, kama mrusi ana nguvu kwanini asiende kuvamia Marekani?
Labda ni mali ya Putin msamehe,Udogo wa macho sio udogo wa ubongo.Lakini mpe hesabu ya kutambua thamani ya binadamu hajui hadi kesho.
 
Rubbish, huwa nakuunga mkono mambo mengi lakini sikuungi kwa ujinga huu wa kuua watu wasio na hatia, kama mrusi ana nguvu kwanini asiende kuvamia Marekani?
Kabla ya kukimbilia na mihemuko je umesoma alichoandika Yericko? hoja hujibiwa kwa hoja na sio kusema tu rubbish, atavamiaje Marekani kwa ugomvi upi au hujasoma majiombo ambayo watu wake wamekuwa wakiuawa na Ukraine lakini akina bwana mkubwa wamekaa kimya. je hushangia kwanini iwe Ukraine tu ndio ishadidiwe na si kwa Palestine,Syria na nchi nyingine lakini kwa Ukraine tu ni kama dunia imesimama?
 
Mauaji anayofanya Marekani ndiyo yanayohalalisha mauaji anayofanya Putin?
Urusi ametetea haki gani za Waafrika na Tanzania na dhidi ya nani?
 
Taifa hili lina nakisi kubwa sana ya waandishi kama hadi vitabu vya Yericko vinaweza kupata wasomaji.
Yericko hili bandiko lako umeonekana una bias Sana hivyo wasomaji wengi wamekupuuza Sana. Kuanzia leo mavitabu na matakataka yako sitoyasoma tena umeonekana na ushabiki una mawazo ambayo hayabalance poor you
 
Htr kushangilia mauaji.. Pia kuunga mkono Putin (MTU mmoja) mwenye maamuzi ya peke yake ni zaidi ya htr maana hatujui kesho atasemaje au ankja na lipi.. Hizo silaha zikiwa chini ya MTU asiye aminika ni HOMA ya dunia
 
Hongera umekariri vema propaganda ya Putin!!
Ila ni dhahiri huelewi unachoandika. Unarejea mkataba wa Minsk ya 2015, ingawa huwahi kuisoma! Mle Ukraine inaitwa Ukraine si "ukanda wa Urusi" jinsi unavyodai. - Yale mauaji ya watu wenye lugha ya kirusi katika mashariki ya Ukraine hayakutokea, isipokuwa kiasi pande zote mbili wakati ya kufyatuliana kwa makombora kati ya waasi na jeshi. Yote mengine ni uwongo.
Leo hii Putin anashambulia jiji la Charkiv. Idadi kubwa ya wakazi wake ni wasemaji wa Kirusi, hawajui nkuongea Kiukraine (kama watu wengi kwenye mashariki ya Ukraine). Watu haohao wanjisikia raia wa Ukraine, hawateswi ila sasa wanateswa na jeshi la Urusi na wenyewe wanatetea mji wao dhidi ya vikosi vya Putin, hata wakiwa tu na vyupa vya petroli dhidi ya bombombu na vifaru.
 
Htr kushangilia mauaji.. Pia kuunga mkono Putin (MTU mmoja) mwenye maamuzi ya peke yake ni zaidi ya htr maana hatujui kesho atasemaje au ankja na lipi.. Hizo silaha zikiwa chini ya MTU asiye aminika ni HOMA ya dunia
Ulileta andiko lolote kuilaani marekani kuivamia middle East? Ukraine wapigwe tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…