Kwanini nawahusisha Mkuu wa Wilaya na OCD Lindi kwenye kifo cha mtoto wangu...

Kwanini nawahusisha Mkuu wa Wilaya na OCD Lindi kwenye kifo cha mtoto wangu...

Mkuu hujafanya hata upelelezi huru? Ungeenda mpaka shuleni kiujanja, tafuta wanafunzi wenzake. ..

Zungumza nao, walau watakupa picha ya juu juu.

Pole sana. Nimesikitika sana. Mungu wa Mbinguni akawe mfariji wako.
Kiukweli inauma, fikiria mimba, anazaliwa (mziki wa kulea) anafikia hatua anajielewa na hapo sio kwamba malezi yamesimama. Haya anaanza shule anafanikiwa kufika hadi level aliyokuwa nayo hadi umauti.

Hatupingi kifo, walakini unaibuka kwenye mzunguko wa kifo chenyewe kilivyotokea, inahuzunisha.
 
Pole sana mkuu kama mzazi inasikitisha sana, tatizo humu mmevamiwa na dot. Com,na vi tiss uchwara ambavyo vinajifanya ni semi God's, nchi imepoteza heshima na adabu yake, iam afraid hii case ina kila dalili itakua ni cold case soon, kama mzazi uamua mwenyewe how to revenge ushenzi na unyama huu, kumbuka kifo cha dada Akwilina, eti risasi imeenda juu na wakati wa kurudi ndio ikamuua ,huu ni uongo wa kinyama, kama upo nje ya royal families sahau haki yako, u need to push back mwenyewe, samahani kwa hili ila ndio ukweli wenyewe, unafiki sio mwema pole sana
Mkuu asante kwa mchango huu makini..matatizo yote yanayotokea Tanzania kwa mtu mmoja mmoja, familia nk ambayo yanagusa mamlaka chimbuko lake ni udhaifu wa wenye mamlaka nchi inaongozwa na WATOTO..watoto kwa maana kwamba hawana sifa na uwezo wa kutekeleza majukumu ya uongozi..tunakoelekea nchi itaangukia shimoni..sidhani mtu mzima anaweza kufanya haya yaliyofanyika, awe DC, OCD, Mkuu wa shule na hao wengine!
 
Hii imenikumbusha mtoto wa Mwinyi, aligonga MTU akaua, akakimbilia ikulu, magogoni!
Polisi waliufyata hakuna kilichofanyika, siku ya msiba, Alikuja mke mdogo wa Mwinyi kutoa rambirambi.
 
hamna cha uroyal family wala nini awa watu ukiwafuata fuata haki unapata mimi nakwambia...ile meseji yake ya mwanzo wengi tulizani masikhala nikiwemo mimi.

amuandikie barua mh. Rais nakuhakikishia hili jambo litaleta mkanganyiko na watafunguliana mashitaka. kwenye hiyo barua iwe ya malalamiko tu isiwe ya madai...
Yes mkuu but why kila kitu tulalamike kwa president?,wapi taasisi zetu za kusaidia utawala bora?,kwangu President Madiba ni ICON maana baada ya kuliona hili akaunda taasisi imara zenye kujitegemea kutoka kwa executive's, hapa tungekua na IPID huyu mzazi angeenda kwao kufungua docket (hawa wana uwezo wa kuwapeleleza police and to open docket, kuwafungulia mashitaka na kuwa arrest),kwetu hapa nani ana uwezo wa ku arrest OCD?,Pia nchi ingekuwa na PP mzazi huyu angelalamika kwake kuhusu DC,na elewa PP ana mamlaka ya ki judge, uamuzi wake ni binding,hii ni cold case kama yule msichana aliyeuliwa kinyama pale Arusha few years ago na wengi humu wameshasahau
 
Hiki nini tena huko Lindi???!!!?????
Mleta mada weka wazi habari yote kama ilivyo ili umma wote ujue nini hasa kimetokea, na ili upate msaada au ushauri unaostahili. Hakuna sababu ya kuficha ficha mambo ktk vifo au mauaji.
wa kuwadodosa kwa kina hao waliosundikiza msiba kutoka huko Lindi??? Kwenye msafara wa kuleta maiti kwa wazazi wa marehemu, Je, wawakilishi/walimu kutoka Shuleni alikosoma mwanao walikuwepo kwenye msafara?Je, Walitoa neno gani ama salamu za rambirambi??
N
Kuanza nianze kwa kuwashukuru wana Jamii Forums mlio nitafuta pm kwa kunipa pole katika msiba ule mzito. Nawashukuru pia wale mlio kuja pm kunikebehi yakuwa nilikuwa nawasinzigizia nilio wataja kwa kuwahusisha na Mauaji ya A WAPI?
NANI ARIRUHUSU MTOTO ATOKE NJE YA SHULE MPAKA AKAGONGWA?

KUNA UHUSIANO GANI KATI YA MARELIA ILIYOTAJWA NA DC NA KOVU LIRE LA AJALI?
Nakuelewa,inawezekana kabisa we ni muoga sana.ila ndugu uoga unatoka wapi mbele ya maiti ya binti yako,mtu anapata wapi nguvu ya kukukaripia huku umepoteza binti?.Hakuna atakayeniambia kitu kama binti yangu kalala na sababu sizielewi,narudia tena hakuna we ni mjinga period
 
Mpelekee mwalimu wako huu upuuzi uliouandika ili ajione ni jinsi gani alipoteza muda kumfundisha mpumbavu
Sasa wewe unaona na haki kabisa, kwenda Bar kunywa pombe (kinyume cha sheria na unaijua hii),your above the limit na unaamua kuendesha gari you knock someone dead, halafu unataka kuniambia umeua bila ya kukusudia?,ewe Tanzania yangu why usiwe kama New Zealand ,upuuzi huu haupo
 
Kifo cha mwanao chataka kufanana na cha yule msanii mohbad rapper wa nigeria....

Sema mzee wa mohbad ilisemekana alipewa maokoto,ila wadau walishinikiza adi maiti ilifukuliwa kwa ajili ya vpimo....adi leo sijajua ule mjadala uliishia wapi sababu uliwahusisha watu wazito wenye kujuana na raisi..

Vifo vya namna hyo vinamaumivu ya namna yake....
 
Najaribu kuvaa viatu vyako kama mzazi ni huzuni kubwa sana, kuna wengi wanakejeli kwa sababu hawajawahi kufiwa tena na binti pekee! Mungu akutetee kwa kweli.
 
Ndugu mimi kama Baba nilipofika hosptali nililipia pesa pale mochwari Temeke ili niuone mwili wa mwanangu kabla ya kuoshwa nilipo ingia ndani yule kijana wa mochwari alinivuruga kichwa alipoanza kunionesha miili ya maiti wengine nilipofkkia wa mwanangu niliona matone ya Damu kwenye shuka na mdomoni.

Yule kijana wa mochwari temeke kwa sauti ya ukali akanitaka nimvute mtto kutoka kwenye friza tumweke kwenye limeza la chuma mlio wai ingia mochwari mnanielewa kuna meza kama la wauza samaki wabichi mle ndani.

Basi baada ya hapo ndugu wakaingia kuosha mwili waliosha vizuri sikuambiwa na wale walio osha mwili nimekuja kuambiwa walimkuta na kovu mguuni baada ya kuwa amezikwa

Nieleweni jaman mimi nilimgomea Dc kupitia simu ya Ocd hata mkitaka ushahidi tumaweza kuupata mkasikia sauti za mazungumzo yangu na yule bwana

Baada ya kurudiwa akili nikawa sawa nilimtafuta Ocd na kumwomba aniunganishe na Mkuu wa Wilaya yule bwana Ocd kwa sauti ya kufoka mithili anamfokea mkewe nyumbani kwake aliniambia hanipi no ya Dc kama nataka kuchunguza mwili nichunguzie huko huko temeke.

Sasa utachunguza mwili ambao haukuwa na nyarraka yoyote,na je utaanzia wapi ndo nilkuwa sielewi

Ndugu zangu nasema mnaweza niona poyoyo nakubali kabisa kiukweli nilipatwa na tukio zito sanaa
Sikuwaza kabisa zaidi.

Naendelea kushukuru michango yenu ndugu

Nimeisha anza kufanyia kazi ushauri wenu

Mathalani kuwasiliana na ofisi ya IGP,ofisi ya malalamiko Dodoma lakini pia nipo katika hatua ya kufungua malalamiko ofisi ya Rais.
"He who claims must prove".
Kwenye maelezo yako hayatoshelezi kuthibitisha tuhuma kwa hawa watu unaowatuhumu, yaani OCD, Mkuu wa Wilaya, Mganga Mfawidhi wa Wilaya, n.k.
Kuna vitu vingi umeamua makusudi kuvificha, hutaki kuvieleza hapa.
Mpaka sasa hujaeleza mahali popote pale kama uliwahi kufanya mawasiliano na Uongozi wa Shule ambako mwanao alikuwa anasoma, WHY???????
Mtoto wako alipoenda kuripoti Shuleni alikosoma maana yake ni kwamba wewe mzazi wa kiume pamoja na mkeo mlimkabidhi mtoto huyo kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Lindi pamoja na Uongozi wote wa Shule hiyo ili kusudi mtoti huyo awe chini ya uangalizi wao. Sasa ulipopata taarifa za msiba zenye utata mwingi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya, Je, ni kwa nini wewe kama mzazi haukujaribu kufanya mawasiliano kwa Uongozi wa Shule ambako mwanao alikuwa anasona ambao ndio haswa uliwakabidhi mtoto wako ili awe chini ya uangalizi wao/ wamlee???????!??!!!??? Kwa nini hasa unakwepa kutujuza taarifa za mtoto wako ulizopata kutoka kwa Uongozi wa Shule?????Kwa sababu kwa kesi yako hii, Mtuhumiwa Namba Moja wa Mauaji na kifo cha Mwanao ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Lindi, wala siyo OCD, DC au Mganga Mfawidhi wa Wilaya, kwa sababu mtoto wako haukuwakabidhi hao ili wamlee Bali ulimkabidhi kwa Uongozi wa Shule.
Jinsi ulivyoli-handle suala hili tayari umesababisha ushahidi mwingi wa muhimu kupotea, till the moment you're about to lose all "water-tight evidences.". Kitaaluma Mimi pia ni Mtafiti na Mchunguzi (A Researcher &An Investigation Expert), lakini ninapata tabu sana kulielewa vyema hili suala lako.
 
Kulipiza kisasi ni haki.....

jamaa zangu wakirustu wengi wenu mnawaona waislamu ni magaidi.....ule si ugaidi ni ile hali ya mtu kujawa na ujasiri wa kudai haki yake au kulipiza kisasi....sema ndo hvyo tu propaganda ni nyingi.

Nchi iliojaa siasa kuna uhuru wa bendara sio wa haki...
 
Ndugu mimi kama Baba nilipofika hosptali nililipia pesa pale mochwari Temeke ili niuone mwili wa mwanangu kabla ya kuoshwa nilipo ingia ndani yule kijana wa mochwari alinivuruga kichwa alipoanza kunionesha miili ya maiti wengine nilipofkkia wa mwanangu niliona matone ya Damu kwenye shuka na mdomoni.

Yule kijana wa mochwari temeke kwa sauti ya ukali akanitaka nimvute mtto kutoka kwenye friza tumweke kwenye limeza la chuma mlio wai ingia mochwari mnanielewa kuna meza kama la wauza samaki wabichi mle ndani.

Basi baada ya hapo ndugu wakaingia kuosha mwili waliosha vizuri sikuambiwa na wale walio osha mwili nimekuja kuambiwa walimkuta na kovu mguuni baada ya kuwa amezikwa

Nieleweni jaman mimi nilimgomea Dc kupitia simu ya Ocd hata mkitaka ushahidi tumaweza kuupata mkasikia sauti za mazungumzo yangu na yule bwana

Baada ya kurudiwa akili nikawa sawa nilimtafuta Ocd na kumwomba aniunganishe na Mkuu wa Wilaya yule bwana Ocd kwa sauti ya kufoka mithili anamfokea mkewe nyumbani kwake aliniambia hanipi no ya Dc kama nataka kuchunguza mwili nichunguzie huko huko temeke.

Sasa utachunguza mwili ambao haukuwa na nyarraka yoyote,na je utaanzia wapi ndo nilkuwa sielewi

Ndugu zangu nasema mnaweza niona poyoyo nakubali kabisa kiukweli nilipatwa na tukio zito sanaa
Sikuwaza kabisa zaidi.

Naendelea kushukuru michango yenu ndugu

Nimeisha anza kufanyia kazi ushauri wenu

Mathalani kuwasiliana na ofisi ya IGP,ofisi ya malalamiko Dodoma lakini pia nipo katika hatua ya kufungua malalamiko ofisi ya Rais.

Pole sana kaka.

Hii nchi hiii
 
Mkuu ni kuulize mlikubali kuzika? Kama mlikubali kuzika bila uchunguzi basi umetupotezea muda sana na akili zetu tuliotoa ushauri! Nauliza tena mlikubali kuzika? Kama mmekubali basi case closed

Yes mkuu but why kila kitu tulalamike kwa president?,wapi taasisi zetu za kusaidia utawala bora?,kwangu President Madiba ni ICON maana baada ya kuliona hili akaunda taasisi imara zenye kujitegemea kutoka kwa executive's, hapa tungekua na IPID huyu mzazi angeenda kwao kufungua docket (hawa wana uwezo wa kuwapeleleza police and to open docket, kuwafungulia mashitaka na kuwa arrest),kwetu hapa nani ana uwezo wa ku arrest OCD?,Pia nchi ingekuwa na PP mzazi huyu angelalamika kwake kuhusu DC,na elewa PP ana mamlaka ya ki judge, uamuzi wake ni binding,hii ni cold case kama yule msichana aliyeuliwa kinyama pale Arusha few years ago na wengi humu wameshasahau
kutokana na kanchi huyo pekee ndie anae ogopeka kwa sasa. akienda mahakamani atapigwa dana dana mpaka miaka itakatika. ila akitumia mbinu ya kumuandikia moja kwa moja Raia yeye Mh Rais ataamua saaa kama atawashitaki watu wake ama lah.

na kingine atakuwa ameji defense maana kesi Rais anaweza asiijue ila Rais akiijua itakuwa ngumu kwao kumfanyia kitu kibaya. hii nchi yetu kuna mambo usipo yaelewa unaishia kati kati....😭😭😭😭​
 
Ni kipi sijakiandika ndugu?
Umesema mama ya Mtoto kupigiwa simu, mama ya Mtoto kunyangwanywa simu, mama kuelezwa Mtoto kafariki, Mama mkubwa kutaarifiwa, ndugu wengine kutaarifiwa kwamba wapokee Mwili wa Marehemu, Mwili kuletwa Usiku toka Lindi au Mtwara, Mwili kuwasili Nyumbani, ndugu kuzozana na Kyaruzi, mwishowe Mwili kupelekwa mortuary. Na kesho yake kwenda kutayarisha mwili wa marehemu, na mwishowe Mazishi.

Sasa ndani ya familia hamkuwa na vikao vyenu, kabla na baada ya kupata Mwili , watu wengine kuwaulizia huko shuleni nini hasa kilitokea, je cheti cha Mazishi hakijaandika sababu ya kifo.
Na pia kwanini mlizika kesho yake na Mwili ulifika Usiku , na taarifa zaidi baada ya Mazishi zinasemaje. Za njia za pembeni na njia za kiserekali
 
Ndugu niliutafuta ule uzi ili nitoe update sikuuona ten nikajua umefutwa na kuna kundi liliniandama sana kupitia pm nakaisi nmekosea kuleta ile habari hap..
Wlkinanani hao walikuandama pm leta ushahidi apa....wengi apa hatufahamiani leta ushahidi apa..

Usiwe muogo mkuu....ooh ayaaah
 
JE, KAMA MTOTO HAKUGONGWA NA WAKUBWA KWANINI ALIYEMGONGA HAKUKAMATWA?
Pole kwenu, na sisi sote kumpoteza kijana.

Katika nchi yenye utawala bora na watu wenye upeo wa kujitambua, mambo kama haya kamwe hayawezi kuruhusiwa kufanyika.

Hao viongozi walio tumia nafasi zao, vyeo vyao kufanya mambo tofauti na taratibu wasingetakiwa kuwa wanaendelea kushikilia nafasi hizo.

Nanyi wazazi na ndugu, mliwapa mwanya wa kuwanyima haki zenu, pengine kwa kukosa uelewa wa taratibu zinazohusiana na matukio ya namna hiyo.
Lakini pia, niseme, jambo kubwa la aina hiyo linapo tokea mara nyingi humfanya mtu kusahau lipi la kufanya.

Mlikabidhiwa mwili wa mtoto wenu kinyume kabisa ya taratibu. Lakini pia inabidi kusema ukweli hapa, hakuna mtu yeyote anaye jiandaa kukabiliana na aina hii ya tukio.

Poleni sana.
 
Back
Top Bottom