Kwanini nawahusisha Mkuu wa Wilaya na OCD Lindi kwenye kifo cha mtoto wangu...

Kwanini nawahusisha Mkuu wa Wilaya na OCD Lindi kwenye kifo cha mtoto wangu...

Pole sana ndugu,

Naamini Kuna vitu umechagua kutoviandika hapo Ili kutovuruga ushahidi wa case na tukio.

Mungu akusaidie kupata UKWELI na HAKI.
 
''ifike mahali'' ni msemo uliozoeleka sana Bongo. Hiyo mahali haitafika bila raia kujitambua na kutambua haki zao na kuzidai ka nguvu. Wewe endelea kusubiri ifike mahali lakini haitafika mahali.
Ulichosema kipo sahihi kabisa. Ni ukweli mchungu watanzania tumekuwa keyboard warriors wazuri lakini linapokuja swala la vitendo tumekuwa mithili ya mbuni kuficha vichwa vyetu kwenye shimo kwa matumaini kuwa hata mwili hauonekani pia.

Kwa dalili zilzipo hapo mahali hatutofika kamwe na walio madarakani wataendelea kufanya watakavyo wakijua tutaishia kubwabwaja, yakizidi sana kunazuliwa tukio moja la kipumbavu attention inahamia huko na ya msingi yanasahaulika.

Najisikitikia kuwa Mtanzania.
 
Kuanza nianze kwa kuwashukuru wana jamii forum mlio nitafuta pm kwa kunipa pole katika msiba ule mzito,

Nawashukuru pia wale mlio kuja pm kunikebei yakuwa nilikuwa nawasinzigizia nilio wataja kwa kuwausisha na Mauaji ya mtoto wangu

I?
Duh! Pole sana Mkuu!
 
Huyu alishapewa ushauri hapa toka mwanzo kuwa wasikubali kuzika sasa kama wamekubali kuzika kwakweli ametuangusha sana sana
Ndugu ushauri sikuuona kamwe zaidi niliona matusi yenu na kebei
 
Kuanza nianze kwa kuwashukuru wana jamii forum mlio nitafuta pm kwa kunipa pole katika msiba ule mzito,

Nawashukuru pia wale mlio kuja pm kunikebei yakuwa nilikuwa nawasinzigizia nilio wataja kwa kuwausisha na Mauaji ya mtoto wangu
HULE MPAKA AKAGONGWA?

KUNA UHUSIANO GANI KATI YA MARELIA ILIYOTAJWA NA DC NA KOVU LIRE LA AJALI?
Haijaingia akilini kwa nini watu wote hawo wamuue mtoto wa shule? Kwa nini unadhani JF ina uwezo au sababu zaidi kukusaidia kuliko Diwani wako au IGP?
 
Jibu maswali ya huyo member ni muhimu sana, na mm swali langu ni moja kuona kidonda mguuni inaaashiria vipi kwamba mtoto aligongwa?
Ndugu mimi kama Baba nilipofika hosptali nililipia pesa pale mochwari Temeke ili niuone mwili wa mwanangu kabla ya kuoshwa nilipo ingia ndani yule kijana wa mochwari alinivuruga kichwa alipoanza kunionesha miili ya maiti wengine nilipofkkia wa mwanangu niliona matone ya Damu kwenye shuka na mdomoni.

Yule kijana wa mochwari temeke kwa sauti ya ukali akanitaka nimvute mtto kutoka kwenye friza tumweke kwenye limeza la chuma mlio wai ingia mochwari mnanielewa kuna meza kama la wauza samaki wabichi mle ndani.

Basi baada ya hapo ndugu wakaingia kuosha mwili waliosha vizuri sikuambiwa na wale walio osha mwili nimekuja kuambiwa walimkuta na kovu mguuni baada ya kuwa amezikwa

Nieleweni jaman mimi nilimgomea Dc kupitia simu ya Ocd hata mkitaka ushahidi tumaweza kuupata mkasikia sauti za mazungumzo yangu na yule bwana

Baada ya kurudiwa akili nikawa sawa nilimtafuta Ocd na kumwomba aniunganishe na Mkuu wa Wilaya yule bwana Ocd kwa sauti ya kufoka mithili anamfokea mkewe nyumbani kwake aliniambia hanipi no ya Dc kama nataka kuchunguza mwili nichunguzie huko huko temeke.

Sasa utachunguza mwili ambao haukuwa na nyarraka yoyote,na je utaanzia wapi ndo nilkuwa sielewi

Ndugu zangu nasema mnaweza niona poyoyo nakubali kabisa kiukweli nilipatwa na tukio zito sanaa
Sikuwaza kabisa zaidi.

Naendelea kushukuru michango yenu ndugu

Nimeisha anza kufanyia kazi ushauri wenu

Mathalani kuwasiliana na ofisi ya IGP,ofisi ya malalamiko Dodoma lakini pia nipo katika hatua ya kufungua malalamiko ofisi ya Rais.
 
Ujumbe huu umfikie pia Joyce Mhavile,ITV kuna changamoto kubwa wanahabar wako wanacover stori inayowapa bahasha
Hapa ndio andiko lako limeonyesha ulivyo, yaani ulitaka waje for free kufanya kazi yako? mhavile anajua waandishi wake hawalipi hela ya maana na wanategemea hizo bahasha na wala sio dhambi wala Rushwa.

Mwisho pole sana kwa Kumpoteza binti yako, Ulichokosea ni kukubali kumzika bila uchunguzi kwa sasa ni kama umechelewa
 
Ukiwa kama baba wa mtoto naomba nikiri wazi kwamba hukutekeleza majukumu Yako vilivyo Toka umepata taarifa za msiba na mpaka dogo anazikwa...
Jamaa amenidisapoint sana alikuja hapa mwili ukiwa lindi na tulimshauri asikubali mwili kuzikwa!

Maana kuja kufukuliwa ni process kubwa mpaka wakubwa waone aibu lakini angegoma mwili kuzikwa ingemsaidia zaidi…
 
Ndugu ushauri sikuuona kamwe zaidi niliona matusi yenu na kebei
Mkuu acha uongo karudie kusoma ule uzi ushauri huo ulipewa na kama kuna mtu alikejeli basi ni mmoja! Kasome tena ule uzi! Sasa hata kama ukuona huo ushauri ulikubali vipi kuzika katika hali ulio eleza? Mgegoma na mkawasusia mwili shida mnafikiri habari mpaka wafatwe ITV …ungeweza ku update hata hapa Jf ingesaidia msingekubali kuzika maana sasa hivi itahitajika nguvu na ushawishi mkubwq mpaka mwili urudiwe tena kufukuliwa na ufqnyike uchunguzi!

Lakini usichoke tuendelee kupambana mkuu!
 
Yaliyonifika yakikufika utaelewa! Sikuombei maana si mema
Ila asante ubarikiwe sana
Mimi naona amekuuliza vizuri ili aweze kutoa ushauri au kukusaidia. Hakuna anayeona yaliokupata ni madogo. Lakini taarifa inakati Kati mtu unashindwa kutoa ushauri. Au kukusaidia. Inawezekana umeikata Kwa sababu za msingi, lakini ikampa shida MTU wa nje ya mzunguko wa taarifa yako.
 
Haijaingia akilini kwa nini watu wote hawo wamuue mtoto wa shule? Kwa nini unadhani JF ina uwezo au sababu zaidi kukusaidia kuliko Diwani wako au IGP?
Ndugu sijaomba jamii forum inipe msaada naomb kama unasoma na uelewi basi kaa pale maoni mengine yanazidisha uchungu
Maoni yako nayaweka medhani kwa bwana asshughulike nawe apendavyo
 
Mkuu acha uongo karudie kusoma ule uzi ushauri huo ulipewa na kama kuna mtu alikejeli basi ni mmoja! Kasome tena ule uzi! Sasa hata kama ukuona huo ushauri ulikubali vipi kuzika katika hali ulio eleza? Mgegoma na mkawasusia mwili shida mnafikiri habari mpaka wafatwe ITV …ungeweza ku update hata hapa Jf ingesaidia msingekubali kuzika maana sasa hivi itahitajika nguvu na ushawishi mkubwq mpaka mwili urudiwe tena kufukuliwa na ufqnyike uchunguzi!

Lakini usichoke tuendelee kupambana mkuu!
Ndugu niliutafuta ule uzi ili nitoe update sikuuona ten nikajua umefutwa na kuna kundi liliniandama sana kupitia pm nakaisi nmekosea kuleta ile habari hap..
 
Mimi naona amekuuliza vizuri ili aweze kutoa ushauri au kukusaidia. Hakuna anayeona yaliokupata ni madogo. Lakini taarifa inakati Kati mtu unashindwa kutoa ushauri. Au kukusaidia. Inawezekana umeikata Kwa sababu za msingi, lakini ikampa shida MTU wa nje ya mzunguko wa taarifa yako.
Ni kipi sijakiandika ndugu?
 
Jamaa amenidisapoint sana alikuja hapa mwili ukiwa lindi na tulimshauri asikubali mwili kuzikwa! Maana kuja kufukuliwa ni process kubwa mpaka wakubwa waone aibu lakini angegoma mwili kuzikwa ingemsaidia zaidi…
Ndugu mwili uliletwa na mitutu ya Bunduki kwangu mimi sikuwepo kwangu kabisa nilifika kumekucha mait imeisha pelekwa Temeke ndugu yangu uchungu nilio kuwa nao

Nilitaka nilete update uwezi amini hata maoni kwenye ule uzi sikuyaona zaidi niliishia tu kukutana na kashifa na kejeri pm nikazima simu nimekuja kuingia leo jf baada ya mazishi

Ndugu tambua binti yangu alikuwa bin pekeee sikuwa na mtoto mwingine yaani hapa sina mtoto tena.chukua picha hiyo
 
Back
Top Bottom