Kwanini nawahusisha Mkuu wa Wilaya na OCD Lindi kwenye kifo cha mtoto wangu...

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya inahusikaje kwanza na vifo vya wanafunzi kama ni natural death?

Na nyie mmeshangaza sana kupokea mwili na kuzika katika mazingira yote yale,huwa hamuoni hata kwenye taarifa za habari wengine wanachofanya?

Chachamaeni uchunguzi ufanyike!
 
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya inahusikaje kwanza na vifo vya wanafunzi kama ni natural death?
wote tunajiuliza hivyo... hii kesi ina maswali mengi kuliko majibu... kuna maiti ngapi zipo hospitalini kwa kuwa tu zinadaiwa hivyo haziwezi kuachwa zikazikwe hadi ndugu walipe gharama za matibabu😭😭

kwa wema gani walio kuwa nao huyo OCD pamoja na MKUU wa wilaya...? wamsaidie mtu wasio mjua kweli...?

kuna kitu kimejificha...ila amini ipo siku ukweli utajidhihirisha tu...!
 
Ndugu mwili uliletwa na mitutu ya Bunduki kwangu mimi sikuwepo kwangu kabisa nilifika kumekucha mait imeisha pelekwa Temeke ndugu yangu uchungu nilio kuwa nao

Nilitaka nilete update uwezi amini hata maoni kwenye ule uzi sikuyaona zaidi niliishia tu kukutana na kashifa na kejeri pm nikazima simu nimekuja kuingia leo jf baada ya mazishi

Ndugu tambua binti yangu alikuwa bin pekeee sikuwa na mtoto mwingine yaani hapa sina mtoto tena.chukua picha hiyo
Mkuu nimekuelewa pole sana utapata mwingine Mungu ni mwema!
Ngoja tuendelee kupaza sauti hata baada ya uzi huu leta mwingine hadi Rais achukue hatua kuruhusu uchunguzi
 
kutokana na kanchi huyo pekee ndie anae ogopeka kwa sasa. akienda mahakamani atapigwa dana dana mpaka miaka itakatika. ila akitumia mbinu ya kumuandikia moja kwa moja Raia yeye Mh Rais ataamua saaa kama atawashitaki watu wake ama lah.

na kingine atakuwa ameji defense maana kesi Rais anaweza asiijue ila Rais akiijua itakuwa ngumu kwao kumfanyia kitu kibaya. hii nchi yetu kuna mambo usipo yaelewa unaishia kati kati....😭😭😭😭​
Ukweli mchungu mkuu, upo right maana ni wachache wanaofaidi pie ya nchi
 
Duh hii mambo ni ngumu sana sijui umepataje ujasiri wa kuandika ilihali umekosa ujasiri wa kwenda kurepoti ila pole sana ndugu
 
Ulichosema kipo sahihi kabisa. Ni ukweli mchungu watanzania tumekuwa keyboard warriors wazuri lakini linapokuja swala la vitendo tumekuwa mithili ya mbuni kuficha vichwa vyetu kwenye shimo kwa matumaini kuwa hata mwili hauonekani pia.

Kwa dalili zilzipo hapo mahali hatutofika kamwe na walio madarakani wataendelea kufanya watakavyo wakijua tutaishia kubwabwaja, yakizidi sana kunazuliwa tukio moja la kipumbavu attention inahamia huko na ya msingi yanasahaulika.

Najisikitikia kuwa Mtanzania.
Uafrika hasa utanzania ni laana.
 
Pole sana, bila shaka uchunguzi wa kina unatakiwa. Mashaka ni mengi kuliko majibu.
 
Kwani hii Ishu haikuishaga tu mtoa mada..Ina maana dokezo la kwanza lile haukupata muafaka
Baada ya Mkuu wa mkoa kumfajya vibaya mtoto wa kike, bafo kuna mtu ana wasi wasi na ujinga wa hawa wakuu wa wilaya na mikoa?
Kiufupi madaraka makubwa yanawapa kiburi sana
 
Kuanza nianze kwa kuwashukuru wana Jamii Forums mlio nitafuta PM kwa kunipa pole katika msiba ule mzito. Nawashukuru pia wale mlio kuja PM kunikebehi yakuwa nilikuwa nawasinzigizia nilio wataja kwa kuwahusisha na Mauaji ya mtoto wangu.

Ilianzia hapa: Mh. Rais, Mkuu wa Wilaya na OCD Lindi 'wamemuua' ANGEL KESSY Mwanafunzi wa PCB

Naomba nieleze kilichojitekeza na ili niweze eleweka vizuri. Kisa kilikuwa hivi:
Mtoto aliripoti shule ya Lindi girls akiwa mzima wa afya pasi na shida yoyote kiafya akitoka shule aliyokuwa amepangiwa Iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani kombi ya PCB.

Baada ya kuripoti amesoma pale wiki mbili akielekea wiki ya 3 tunapewa taarifa yakuwa mtoto amezidiwa tarehe 16 saa nne kamili kupitia simu ya Mama yake. Tarehe hiyo hiyo 16/11/2023 kwa simu ya mtu aliyejitambulisha ya kuwa ni mwalimu, mama mzazi wa marehemu alitokea Mbagala kuelekea shule majira ya saa tano kamili na alifika shule pale saa kumi na mbili kamili.

Mama mzazi alipofika cha kwanza alikutana na watu wafatao;-
1. Mkuu wa Wilaya ya Lindi.
2 OCD kituo cha polisi Lindi.
3. Mganga Mfawidhi wa Wilaya.
4. Walimu wawili.

Kutokana na uwepo wa watu hao kwenye eneo ilo kulipelekea Mama mzazi wa Marehemu kuingia na hofu kubwa kuwa yawezekana mtoto wake ameishaFARIKI. Ili mambo yaweze kwenda sawa, jopo ilo hapo likiongozwa na DC liliona ni busara kwanza kumnyang'anya simu ya Mkononi Mama yule kitendo kile kilimtia hofu zaidi.

Baada ya kumnyang'anya simu walimwingiza ndani na kumwonesha mtoto wake akiwa TAYARI KWENYE JENEZA. Mama mzazi wa marehemu kiukweli alipatwa na mshutuko mkubwa sana watu wale wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya na OCD walimtaka mama yule ataje no za simu za ndugu wa karibu.

Mama wa marehemu alitaja no ya kwanza ni ya Dada yake mkubwa ya pili alitaja no za simu za mme wake na mtoto wa Dada yake.

Ili kutimiza kile walichokuwa wamekipanga yafatayo yalifanyika:
Kwanza DC kupitia simu ya OCD alipiga simu kwa Dada mkubwa wa mzazi wa marehemu kumpatia taarifa yule dada mtu alipokea taarifa na kuanza safari kutoka Bukoba kuja DSM.

Aliyepigiwa akiwa wa Pili ni Baba wa Marehemu huyu alipigiwa simu ya kupewa taarifa lakini pia akubali mwili uletwe usiku usiku kwa gari la serikali na JENEZA tayari liliishanunuliwa.

Simu nyingine ilikwenda kwa Kaka wa Marehemu; yeye alipewa taarifa ya msiba na kuombwa pia akubali mwili uletwe DSM usiku usiku. Kwa upande wa Kaka wa marehemu yeye alipinga mwili usiletwe DSM mpaka ufanyiwe uchunguzi.

Kwa kuwa mama wa marehemu alikuwa kazingirwa na kundi hilo likiongozwa na DC huku akiwa amenyang'anywa simu, kila tulipopiga simu yake, ilipokelewa na Mwalimu aliyedai kuwa MAMA WA MAREHEMU AMEZIMIA.

Kwa maana hii, aliyeridhia pasipo kufikiria kwa kina mwili uletwe alikuwa mtu mmoja tu. Kweli majira ya Saa TISA usiku mwili ulifikishwa nyumbani kwao Kongowe Mzinga DSM. Baada kufikishwa mwili waliingia ndani wanawake wawili na wanaume wawili wakajitambulisha vizuri. Wakiwa ndani ukatokea mzozo kidogo ndugu wa marehemu wakataka kujua nini kilichomuua mtoto wao.

Ndipo alipojitokeza Askari Polisi aliyevalia kiraia, akajitambulisha kuwa yeye ni Afande Kyaruzi, akatoa maneno yalikuwa na vitisho ndani yake. Mwisho magari yale mawili yaliwabeba Baba wakubwa wa marehemu baadhi ya ndugu mpaka hospatli ya Temeke kwa ajili kuhifadhi mwili.

Mwili ulihifadhiwa pale, hakuna nyaraka yoyote iliyotolewa kutoka shuleni na hospitali ya Lindi iliyoonesha mtoto aliumwa nini? Na walimpa dawa gani?

Zaidi, wale walimu na afande Kyaruzi waliacha stakabadhi inayoonesha Mkuu wa Wilaya na jopo lake walilipa shiilingi Laki moja ya kumuhifadhi mtoto hosptalini tu na walilipa mwili uhifadhiwe saa 24, jambo lililoonesha kuwa hata malipo yalifanyika tarehe 15/11/2023.

Ila sisi wanafamilia tulipewa taarifa tarehe 16.

Kilichotushangaza zaidi:

Ndugu wa marehemu walipoenda kuosha mwili walikuta mwili wa marehemu ukiwa na kovu kubwa sana maeneo ya miguuni na lilikuwa limeshonwa na nyuzi kumi na mbili. Kovu lile liliashiria marehemu alikuwa amegongwa.

Changamoto walioosha mwili hawakuwa tayari kutoa taarifa kuwa wamekuta mwili una kovu jambo hilo lilipelekea kuendelea na ratiba ya mazishi na tulimzika mtoto wetu tarehe 18/11/2023.

Marehemu (mtoto wangu) alikuwa anaitwa ANGEL NINSIMA KESSY na alikuwa MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO (PCB) LINDI GIRLS.

KWANINI TUNAMTUHUMU MKUU WA WILAYA, OCD NA MGANGA MFAWIDHI?

1. Kwanini msiba ule haukutolewa taarifa ya kifo na Uongozi wa Shule badala yake awe DC kupitia simu ya OCD?

2. Kwanini Mkuu wa Wilaya na jopo lake hawakutoa taarifa ya mtoto aliumwa nini? Je, alipokelewa hosptali na kupimwa na kupewa dawa gani?

3. Kwanini Mkuu wa Wilaya alikuwa akipiga simu na kuomba sana mwili upokelewe Usiku ule ule pasipo kukubali ifanyike postmotamu?

4. Kwanini DC alipofikisha mwili Temeke hosptali hawakuteua mtu hata mmoja kufika hapo msibani kuleta hata salamu za shule kwa niaba ya shule na wanafunzi wenzie na marehemu?

5. Kama mtoto alikufa kifo cha kawaida, Polisi walisindikiza Mwili wa marehemu kwa cheo gani alichokuwa nacho marehemu?

6. Kwanini DC baada ya kufikisha mwili Dar alizuia mawasiliano baina yake na ndugu wa marehemu akaelekeza mawasiliano yote yafanyike kati ya ndugu wa marehemu na OCD tu?

Tunahoji mengi katika hili.

Nimalizie kwa kufikisha masikitiko yangu makubwa kwa waandishi wa habari hasa ITV NA VYOMBO VINGINE Maana tuliwatafuta tukihitaji msaada wao ili taarifa hii iweze fika mbali kwa ajili ya kufichua uovu wa namna hii lakini hawakuwa tayari.

Ombi langu nalipeleka kwa Mawaziri wa Afya na TAMISEMI, jambo hili lichunguzwe,

Napeleka ombi kwa mkuu wa Odara ya Usalama wa Taifa, tafadhali fanya jambo hapa.

Napeleka ombi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) tafadhali OCD na Afande Kyaruzi wawajibishwe.

Napeleka ombi langu kwa Waziri wa Elimu shule ya Lindi Girls ni ya Serikali; uzembe uliojitokeza hasa kwa watumishi wa shule ni mkubwa mpaka mwanangu anaaga dunia.

Mwisho kwa Mh Rais, kwa mamlaka yake jamani ni huzuni kumpoteza mtoto wa kidato cha tano mkondo PCB, tuliisha invest vingi jamani.

Naomba niliowataja wawajibishwe kwa manufaa ya Umma.

Ujumbe huu umfikie pia Joyce Mhavile: ITV kuna changamoto kubwa wanahabari wako wana-cover stori inayowapa bahasha.

WASI WASI

JE, KAMA MTOTO HAKUGONGWA NA WAKUBWA KWANINI ALIYEMGONGA HAKUKAMATWA?

JE, MTOTO ALIGONGWA AKITOKEA WAPI KWENDA WAPI?

NANI ARIRUHUSU MTOTO ATOKE NJE YA SHULE MPAKA AKAGONGWA?

KUNA UHUSIANO GANI KATI YA “MARELIA” ILIYOTAJWA NA DC NA KOVU LIRE LA AJALI?
Hivi suala hili liliishia wapi?
Mhusika utupatie feedback
 
Huyu DC yeye ndie msimamizi wa haki na kuzuia dhuluma ktk wilaya yake.
Lakini tunaona huyu DC ndie dhulumati mkubwa wa haki za raia!
Mama SSH please anza na huyu mtu anaekuchafua na uchunguzi ufanyike.
 
Duuh ya lini hii?
 
dah aiseeeee haya mambo yanaumiza sana.....

Hii dunia si mahali salama....
 
Back
Top Bottom