Kwanini Nchi nyingi zenye asili ya Uislam zinakumbwa na Vita sana?

Ufitini wa nchi za magharibi ndio chanzo kikuu... Wao ndio wana sponsor rebel groups
 
Doctrine ya uislam ni kwamba muislam ni ndugu kwa muislam!

Nikiwa bado mdogo hivi nikiingiz msikitini wakati wa kuswali unapiga mstari huku vidole vya mwisho miguuni vile vidogo vya mwisho vinagusana na vya mwenzako kuonesha jamaa!!

Sasa basi,utajiri uliopo nchi tajiri za kiislam ungeeenea kwa waislam wenzao bila shida yoyote na kustawi kote sana hasa kijamaa zaidi na ustawi was maisha!!

Marekani akihofia hayo yote na nchi za kibepari duniani wakaanzisha ugaidi hapo September 11 na vikundi hivyo vikazaliwa kama donda ndugu Kote duniani!!

Kanuni ni rahisi sana;-

Uislam:-ujamaa

Ukristo:-ubepari

Sisi tulioamua kuwa huru tupo mixed!!

Kwa hiyo Russia 🇷🇺 Venezuela 🇻🇪 na Cuba 🇨🇺 ni wasilam?
 
Maneno haya aliyotamka Yesu, hakuna mwanadamu yeyote wala malaika wala kerubi wala serafi awezaye kujitamkia, isipokuwa Mungu tu.

Kimsingi Yesu alikuwa akisema: unavyoniona Mimi hapa, ndiye Mungu hasa niliye katika sura na umbile la kibinadamu.

Kabla ya maneno haya kutamkwa, Tomaso alikuwa amemuuliza Yesu swali: ^Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia?^ (aya ya 5).

Jibu la Yesu linaonesha uhusiano Wake na Baba ukoje: Mimi ndiye njia, kweli na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya Mimi.

Siyo tu kwamba Yesu ni njia na kweli ya kutufikisha kwa Baba, bali hapa anatamka kwamba Yeye ndiye uzima kwa vile ndiye Muumbaji! (Mwanzo 2:7).

Isingeleta mantiki yoyote hata kidogo kudai hivyo kwamba Yeye ni njia, kweli na uzima iwapo angekuwa Mtume tu wa Mungu!

Akaongeza: ^Kama mngalinijua Mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.^

Pamoja na maneno hayo ya Kristu, yasiyokuwa na chembe ya mashaka yoyote kwamba Yeye ni nani, bado Filipo akarudia swali la msisitizo:

^Bwana, utuoneshe Baba, yatutosha!^

Ni kama vile alikuwa akimwambia Yesu: ^Bwana, iwapo unazungumzia kumjua au kumwona Mungu kupitia matendo Yako, hilo mbona tunalifahamu vizuri sana. Tunachotaka sisi ni kumwona Mungu kabisa jinsi alivyo, yukoje, Yeye ni nani!^

Hii ni kweli, hasa ikizingatiwa kwamba wanafunzi hao walikuwa pamoja na Kristu muda wote, walijua historia Yake na kwamba watu wengine wote walimtambua kama nabii wa Mungu.

Maswali ya Tomaso na Filipo yasingeleta maana yoyote iwapo walikuwa tu wakiuliza kuhusu utendaji wa Mungu.

Kwamba walitaka kuoneshwa matendo ya Mungu kupitia Yesu, wakati walikuwa wameshuhudia muda wote huduma Zake mbalimbali za huruma na upendo pamoja na miujiza Yake?

Ukweli ni kwamba maswali haya ya Tomaso na Filipo ni swali na lile la Musa alipomuuliza Mungu: ^Nakusihi unioneshe utukufu Wako^ (Kutoka 33:18), ambapo akajibiwa, ^Huwezi kuniona uso Wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi.^

Ni wazi kwamba Musa alitaka kumwona Mungu katika uhalisia Wake, vivyo hivyo na Tomaso na Filipo. Musa alioneshwa wema wa Mungu, huku wale wanafunzi wakioneshwa Kristo Mwenyewe!

^Filipo akamwambia, Bwana, utuoneshe Baba, yatutosha. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona Mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuoneshe Baba? Husadiki kwamba Mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani Yangu?^ (Yohana 14:8-10a).

Majibu yaleyale ambayo Yesu aliwaambia wanafunzi katika Yohana 14, ndiyo aliwaambia Wayahudi walitaka kujua hasa Yeye ni nani (Yohana 10:24-38):

^Hata lini utatuhangaisha nafsi zetu? Kama Wewe ndiye Kristo, utuambie waziwazi.^

Wayahudi walikuwa wakifahamu vyema unabii waliosoma katika Agano la Kale kumhusu Kristu. Mathalani:

Isaya 9:6 ^Maana kwa ajili yetu Mtoto amezaliwa, Tumepewa Mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani Mwake; Naye ataitwa jina Lake Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.^

Isaya 7:14 ^Kwa hiyo Bwana Mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa Mtoto mwanamume, Naye atamwita jina Lake Imanueli.^

Si ajabu Yesu alipowaambia Yeye ndiye, waliokota mawe ili kumpiga (kwa sababu Wayahudi wengi hawakuamini kwamba ndiye hasa alikuwa Masihi!)

Zingatia baadhi ya maneno aliyotamka Kristu hapa, yanayoonesha Yeye ni zaidi ya mwanadamu na malaika:

^Nami nawapa uzima wa milele^ (aya ya 28). Ni Mungu pekee ndiye awezaye kutupatia uhai au kuuondoa.

^Mimi na Baba tu umoja^ (aya ya 30). Ndiyo maana Yesu anaitwa Mwana pekee (the only begotten Son). Maneno ya Kiyunani ni monogenes, yenye maana ya mwenye asili ileile sawa Naye!

Kama unadhani Wayahudi hawakuelewa kile ambacho Yesu Kristu alikuwa akiwaambia juu ya uhusiano Wake na Baba, hebu zingatia maneno yao:

^Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu Wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.^ (aya ya 33).

Ni wazi hapa Yesu alikuwa akiwaambia kwamba Yeye ndiye Mungu hasa! Na wala siyo kwamba matendo Yake tu ndiyo yalikuwa sawa na yale ya Mungu!

^Ikiwa tunataka kusisitiza…yote ni uongo^

Ujio wa Yesu duniani katika sura na umbile la mwanadamu ni sawa kabisa na vile ambavyo Mungu aliwatokea manabii, mitume na watu Wake zamani katika maumbile mbalimbali kama vile malaika, nk. (Waamuzi 13:20-22; 6:11-23).

Mungu anaweza kujivika sura ya nafsi yoyote au kitu chochote. Kule jangwani, Mungu alimtokea Musa katika kichaka kilichokuwa kinawaka moto bila kuteketea (Kutoka 3:1-6).

Yesu ni Mungu katika umbile la kibinadamu. Asili Yake ya uungu ilisitirika katika ubinadamu. Katika umbile hili ndipo wanafunzi Wake waliweza kumwona Mungu.

Hawakuishia kuona matendo tu ya Mungu, bali walimwona Mungu Mwenyewe hasa!

^Hapo mwanzo alikuwepo Neno, Naye Neno alikuwa kwa Mungu, Naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwepo kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa Huyo; wala pasipo Yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. Ndani Yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.^ (Yohana 1:1-4).

Je, MUNGU aliwahi kuonekana katika umbo la mwanadamu kwa yeyote?

Mwenyezi Mungu alipozungumza na Mitume kama Musa, Ibrahimu na wengine, ambayo yameandikwa katika Biblia na Quran Tukufu, je, alionekana katika umbo la mwanadamu halisi?

Kwa uaminifu kabisa, haijalishi. MUNGU Mwenyezi anaweza kuonekana kama mbwa, paka, ng'ombe au mwamba akitaka.

Kwa hivyo haihusu kutowezekana kwa MUNGU kuifanya, lakini je, MUNGU Mwenyezi angejifanya?

Kwa mfano, je, sasa hivi MUNGU Mweza-Yote anamtokea mtu fulani au viumbe vingine, kama wanyama au wadudu na kuzungumza nao moja kwa moja?

Hakika hakuna lisilowezekana kwa MUNGU. Lakini angefanya hivyo?

Kwa kweli hangefanya hivyo (isipokuwa kwa makusudi kabisa anataka kuwadanganya watu fulani kama vile Biblia inavyofafanua kwa kina juu ya mada ya roho za uwongo za Biblia ambazo MUNGU Mwenyezi anazituma ili kuwadanganya watu wa uongo) kwa sababu hiyo ingefanya uumbaji mkuu wa MUNGU Mwenyezi kukosea.

Biblia yenyewe inajibu swali hili la msingi:

Kutoka 6:3

3. Nalimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, lakini kwa jina langu, BWANA, sikujidhihirisha kwao kabisa.

Hesabu 23:19

19 Mungu si mtu, aseme uongo; wala mwana wa Adamu, hata ajute; au amesema, na hatalitimiza?

MUNGU si mwanadamu wa damu na nyama (Hesabu 23:19).

Yuda 8:16

Usijaribu kuyafunga makusudi ya Bwana, Mungu wetu; kwa maana Mungu si kama mwanadamu, kutishwa, wala si kama mwanadamu ili avutwe kwa kusihi.

Kwa hivyo ikiwa MUNGU Mwenyezi si mwanadamu, basi asingeonekana kama mwanadamu kwa yeyote. Anaweza kuonekana kama Nuru katika mwonekano wa mwanamume, pengine, lakini hangeonekana kama mtu wa nyama na damu. Hii inathibitishwa zaidi hapa:

Luka 1:11-12

Malaika wa Bwana akamtokea, amesimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia. Zekaria alipomwona alifadhaika, na hofu ikamwangukia.

Kutoka 3:2

2. Huko malaika wa Bwana akamtokea katika miali ya moto kutoka ndani ya kijiti. Musa aliona kwamba kile kijiti kilikuwa kinawaka moto hakikuteketea.

GOD is not a flesh and blood man (Numbers 23:19).
 
Maneno haya aliyotamka Yesu, hakuna mwanadamu yeyote wala malaika wala kerubi wala serafi awezaye kujitamkia, isipokuwa Mungu tu.

Kimsingi Yesu alikuwa akisema: unavyoniona Mimi hapa, ndiye Mungu hasa niliye katika sura na umbile la kibinadamu.

Kabla ya maneno haya kutamkwa, Tomaso alikuwa amemuuliza Yesu swali: ^Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia?^ (aya ya 5).

Jibu la Yesu linaonesha uhusiano Wake na Baba ukoje: Mimi ndiye njia, kweli na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya Mimi.

Siyo tu kwamba Yesu ni njia na kweli ya kutufikisha kwa Baba, bali hapa anatamka kwamba Yeye ndiye uzima kwa vile ndiye Muumbaji! (Mwanzo 2:7).

Isingeleta mantiki yoyote hata kidogo kudai hivyo kwamba Yeye ni njia, kweli na uzima iwapo angekuwa Mtume tu wa Mungu!

Akaongeza: ^Kama mngalinijua Mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.^

Pamoja na maneno hayo ya Kristu, yasiyokuwa na chembe ya mashaka yoyote kwamba Yeye ni nani, bado Filipo akarudia swali la msisitizo:

^Bwana, utuoneshe Baba, yatutosha!^

Ni kama vile alikuwa akimwambia Yesu: ^Bwana, iwapo unazungumzia kumjua au kumwona Mungu kupitia matendo Yako, hilo mbona tunalifahamu vizuri sana. Tunachotaka sisi ni kumwona Mungu kabisa jinsi alivyo, yukoje, Yeye ni nani!^

Hii ni kweli, hasa ikizingatiwa kwamba wanafunzi hao walikuwa pamoja na Kristu muda wote, walijua historia Yake na kwamba watu wengine wote walimtambua kama nabii wa Mungu.

Maswali ya Tomaso na Filipo yasingeleta maana yoyote iwapo walikuwa tu wakiuliza kuhusu utendaji wa Mungu.

Kwamba walitaka kuoneshwa matendo ya Mungu kupitia Yesu, wakati walikuwa wameshuhudia muda wote huduma Zake mbalimbali za huruma na upendo pamoja na miujiza Yake?

Ukweli ni kwamba maswali haya ya Tomaso na Filipo ni swali na lile la Musa alipomuuliza Mungu: ^Nakusihi unioneshe utukufu Wako^ (Kutoka 33:18), ambapo akajibiwa, ^Huwezi kuniona uso Wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi.^

Ni wazi kwamba Musa alitaka kumwona Mungu katika uhalisia Wake, vivyo hivyo na Tomaso na Filipo. Musa alioneshwa wema wa Mungu, huku wale wanafunzi wakioneshwa Kristo Mwenyewe!

^Filipo akamwambia, Bwana, utuoneshe Baba, yatutosha. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona Mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuoneshe Baba? Husadiki kwamba Mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani Yangu?^ (Yohana 14:8-10a).

Majibu yaleyale ambayo Yesu aliwaambia wanafunzi katika Yohana 14, ndiyo aliwaambia Wayahudi walitaka kujua hasa Yeye ni nani (Yohana 10:24-38):

^Hata lini utatuhangaisha nafsi zetu? Kama Wewe ndiye Kristo, utuambie waziwazi.^

Wayahudi walikuwa wakifahamu vyema unabii waliosoma katika Agano la Kale kumhusu Kristu. Mathalani:

Isaya 9:6 ^Maana kwa ajili yetu Mtoto amezaliwa, Tumepewa Mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani Mwake; Naye ataitwa jina Lake Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.^

Isaya 7:14 ^Kwa hiyo Bwana Mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa Mtoto mwanamume, Naye atamwita jina Lake Imanueli.^

Si ajabu Yesu alipowaambia Yeye ndiye, waliokota mawe ili kumpiga (kwa sababu Wayahudi wengi hawakuamini kwamba ndiye hasa alikuwa Masihi!)

Zingatia baadhi ya maneno aliyotamka Kristu hapa, yanayoonesha Yeye ni zaidi ya mwanadamu na malaika:

^Nami nawapa uzima wa milele^ (aya ya 28). Ni Mungu pekee ndiye awezaye kutupatia uhai au kuuondoa.

^Mimi na Baba tu umoja^ (aya ya 30). Ndiyo maana Yesu anaitwa Mwana pekee (the only begotten Son). Maneno ya Kiyunani ni monogenes, yenye maana ya mwenye asili ileile sawa Naye!

Kama unadhani Wayahudi hawakuelewa kile ambacho Yesu Kristu alikuwa akiwaambia juu ya uhusiano Wake na Baba, hebu zingatia maneno yao:

^Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu Wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.^ (aya ya 33).

Ni wazi hapa Yesu alikuwa akiwaambia kwamba Yeye ndiye Mungu hasa! Na wala siyo kwamba matendo Yake tu ndiyo yalikuwa sawa na yale ya Mungu!

^Ikiwa tunataka kusisitiza…yote ni uongo^

Ujio wa Yesu duniani katika sura na umbile la mwanadamu ni sawa kabisa na vile ambavyo Mungu aliwatokea manabii, mitume na watu Wake zamani katika maumbile mbalimbali kama vile malaika, nk. (Waamuzi 13:20-22; 6:11-23).

Mungu anaweza kujivika sura ya nafsi yoyote au kitu chochote. Kule jangwani, Mungu alimtokea Musa katika kichaka kilichokuwa kinawaka moto bila kuteketea (Kutoka 3:1-6).

Yesu ni Mungu katika umbile la kibinadamu. Asili Yake ya uungu ilisitirika katika ubinadamu. Katika umbile hili ndipo wanafunzi Wake waliweza kumwona Mungu.

Hawakuishia kuona matendo tu ya Mungu, bali walimwona Mungu Mwenyewe hasa!

^Hapo mwanzo alikuwepo Neno, Naye Neno alikuwa kwa Mungu, Naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwepo kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa Huyo; wala pasipo Yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. Ndani Yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.^ (Yohana 1:1-4).

Njia ya Yesu

Kwanza na kabla ya yote, lazima itambulike kuwa Yesu Kristo, mwana wa Mariamu, alikuwa ni wa mwisho katika orodha ya manabii wa Kiisraeli.

Aliishi kwa mujibu wa Torati, na sheria ya Musa, na aliwafundisha wafuasi zake wafanye hivyo hivyo.

Katika Mathayo 5:17-18, Yesu ameeleza: “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kuitimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.”

Kwa bahati mbaya, kiasi cha miaka mitano baada ya kuisha kwa uchungaji wa Yesu, Rabbi kijana kwa jina la Sauli wa Tarsus, aliyedai kuwa amemuona Yesu katika maono, alianza kubadilisha njia ya Yesu.

Paulo (jina lake kwa Kirumi) alikuwa na heshima kubwa kwa falsafa ya Kirumi na alizungumza kwa ufahari kwa kuwa na uraia wa Roman.

Imani yake ilikuwa ni kuwa wasio-Wayahudi walioingia Ukristo wasibebeshwe mzigo wa Torati kwa hali yoyote ile.

Mtunzi wa Matendo 13:39 anamnukuu Paulo akisema, “Na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa Torati ya Musa.”

Kimsingi ilikuwa ni kwa kupitia juhudi za Paulo ndipo kanisa lilipoanza kufuata mkondo wa tabia za wasio-Wayahudi. Paulo ameandika barua (nyaraka), nyingi za Agano Jipya zinazokubaliwa na kanisa zikiwa ni kama mafundisho rasmi ya kiitikadi na Kitabu kilichofunuliwa.

Nyaraka hizo hazikuilinda Injili ya Yesu wala hata kuiwakilisha;135F136 badala yake amegeuza mafundisho ya Kristo kuwa ya falsafa ya Kihelleniki (Graeco-Roman).

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya mafundisho aliyoyafuata nabii Yesu na kuyafundisha, lakini baadaye yaliachwa na Kanisa.

Hata hivyo, mengi miongoni mwa mafundisho hayo yalifufuliwa katika ujumbe wa mwisho wa Uislamu ulioletwa na Mtume Muhammad (SAW) na yakaendea kubakia kuwa ni sehemu ya msingi katika matendo ya dini ya Kiislamu hadi leo hii.

Kusujudu katika Sala

Yesu ameelezwa katika Yesu ameelezwa katika Injili kuwa amesujudu alipokuwa akisali.

Katika Mathayo 26:39, mtunzi anaeleza tukio lililotokea pale Yesu alipoenda na wanafunzi wake hadi Gethsemane:

“Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba, akasema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utavyo wewe.”
 
Maneno haya aliyotamka Yesu, hakuna mwanadamu yeyote wala malaika wala kerubi wala serafi awezaye kujitamkia, isipokuwa Mungu tu.

Kimsingi Yesu alikuwa akisema: unavyoniona Mimi hapa, ndiye Mungu hasa niliye katika sura na umbile la kibinadamu.

Kabla ya maneno haya kutamkwa, Tomaso alikuwa amemuuliza Yesu swali: ^Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia?^ (aya ya 5).

Jibu la Yesu linaonesha uhusiano Wake na Baba ukoje: Mimi ndiye njia, kweli na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya Mimi.

Siyo tu kwamba Yesu ni njia na kweli ya kutufikisha kwa Baba, bali hapa anatamka kwamba Yeye ndiye uzima kwa vile ndiye Muumbaji! (Mwanzo 2:7).

Isingeleta mantiki yoyote hata kidogo kudai hivyo kwamba Yeye ni njia, kweli na uzima iwapo angekuwa Mtume tu wa Mungu!

Akaongeza: ^Kama mngalinijua Mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.^

Pamoja na maneno hayo ya Kristu, yasiyokuwa na chembe ya mashaka yoyote kwamba Yeye ni nani, bado Filipo akarudia swali la msisitizo:

^Bwana, utuoneshe Baba, yatutosha!^

Ni kama vile alikuwa akimwambia Yesu: ^Bwana, iwapo unazungumzia kumjua au kumwona Mungu kupitia matendo Yako, hilo mbona tunalifahamu vizuri sana. Tunachotaka sisi ni kumwona Mungu kabisa jinsi alivyo, yukoje, Yeye ni nani!^

Hii ni kweli, hasa ikizingatiwa kwamba wanafunzi hao walikuwa pamoja na Kristu muda wote, walijua historia Yake na kwamba watu wengine wote walimtambua kama nabii wa Mungu.

Maswali ya Tomaso na Filipo yasingeleta maana yoyote iwapo walikuwa tu wakiuliza kuhusu utendaji wa Mungu.

Kwamba walitaka kuoneshwa matendo ya Mungu kupitia Yesu, wakati walikuwa wameshuhudia muda wote huduma Zake mbalimbali za huruma na upendo pamoja na miujiza Yake?

Ukweli ni kwamba maswali haya ya Tomaso na Filipo ni swali na lile la Musa alipomuuliza Mungu: ^Nakusihi unioneshe utukufu Wako^ (Kutoka 33:18), ambapo akajibiwa, ^Huwezi kuniona uso Wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi.^

Ni wazi kwamba Musa alitaka kumwona Mungu katika uhalisia Wake, vivyo hivyo na Tomaso na Filipo. Musa alioneshwa wema wa Mungu, huku wale wanafunzi wakioneshwa Kristo Mwenyewe!

^Filipo akamwambia, Bwana, utuoneshe Baba, yatutosha. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona Mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuoneshe Baba? Husadiki kwamba Mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani Yangu?^ (Yohana 14:8-10a).

Majibu yaleyale ambayo Yesu aliwaambia wanafunzi katika Yohana 14, ndiyo aliwaambia Wayahudi walitaka kujua hasa Yeye ni nani (Yohana 10:24-38):

^Hata lini utatuhangaisha nafsi zetu? Kama Wewe ndiye Kristo, utuambie waziwazi.^

Wayahudi walikuwa wakifahamu vyema unabii waliosoma katika Agano la Kale kumhusu Kristu. Mathalani:

Isaya 9:6 ^Maana kwa ajili yetu Mtoto amezaliwa, Tumepewa Mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani Mwake; Naye ataitwa jina Lake Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.^

Isaya 7:14 ^Kwa hiyo Bwana Mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa Mtoto mwanamume, Naye atamwita jina Lake Imanueli.^

Si ajabu Yesu alipowaambia Yeye ndiye, waliokota mawe ili kumpiga (kwa sababu Wayahudi wengi hawakuamini kwamba ndiye hasa alikuwa Masihi!)

Zingatia baadhi ya maneno aliyotamka Kristu hapa, yanayoonesha Yeye ni zaidi ya mwanadamu na malaika:

^Nami nawapa uzima wa milele^ (aya ya 28). Ni Mungu pekee ndiye awezaye kutupatia uhai au kuuondoa.

^Mimi na Baba tu umoja^ (aya ya 30). Ndiyo maana Yesu anaitwa Mwana pekee (the only begotten Son). Maneno ya Kiyunani ni monogenes, yenye maana ya mwenye asili ileile sawa Naye!

Kama unadhani Wayahudi hawakuelewa kile ambacho Yesu Kristu alikuwa akiwaambia juu ya uhusiano Wake na Baba, hebu zingatia maneno yao:

^Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu Wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.^ (aya ya 33).

Ni wazi hapa Yesu alikuwa akiwaambia kwamba Yeye ndiye Mungu hasa! Na wala siyo kwamba matendo Yake tu ndiyo yalikuwa sawa na yale ya Mungu!

^Ikiwa tunataka kusisitiza…yote ni uongo^

Ujio wa Yesu duniani katika sura na umbile la mwanadamu ni sawa kabisa na vile ambavyo Mungu aliwatokea manabii, mitume na watu Wake zamani katika maumbile mbalimbali kama vile malaika, nk. (Waamuzi 13:20-22; 6:11-23).

Mungu anaweza kujivika sura ya nafsi yoyote au kitu chochote. Kule jangwani, Mungu alimtokea Musa katika kichaka kilichokuwa kinawaka moto bila kuteketea (Kutoka 3:1-6).

Yesu ni Mungu katika umbile la kibinadamu. Asili Yake ya uungu ilisitirika katika ubinadamu. Katika umbile hili ndipo wanafunzi Wake waliweza kumwona Mungu.

Hawakuishia kuona matendo tu ya Mungu, bali walimwona Mungu Mwenyewe hasa!

^Hapo mwanzo alikuwepo Neno, Naye Neno alikuwa kwa Mungu, Naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwepo kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa Huyo; wala pasipo Yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. Ndani Yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.^ (Yohana 1:1-4).

Yesu anasemaje katika injili??

Yesu anasemaje katika Injili

Yohana 17:3 imeandikwa hivi –

uzima wa milele ndiyo huu wakujue Mungu wa pekee na Yesu uliyemtuma.

Katika Aya hii Yesu anasema kwamba ili kupata uzima lazima tumjue kwanza Mungu wa pekee na umjue Yesu Kristo aliyetumwa na Mungu, hapa Yesu hasemi lolote kuhusu yeye kuwa nafasi ya pili ya Mungu ila anakiri wazi yeye ametumwa na Mungu mmoja wa pekee.

Luka 2:40 imeandikwa hivi: -

Yule mtoto akakua akaongezeka nguvu amejaa hekima na neema ya Mungu ilikua juu yake.

Katika Aya hii tunaambiwa kwamba Yesu alijaa hekima na neema ya Mungu. Tahadhari ufikirie vizuri kwa makini sababu hapa inayonyesha kwamba bila ya Mungu kumpa neema Yesu asingelikuwa na hekima hii inaonyesha wazi Yesu ni kiumbe aliyeteuliwa na Mungu na hii ni kawaida yake Mwenyezi Mungu kwa Mitume na Manabii wake kuwapa neema na hekima.

Yohana 13:13 imeandikwa hivi: -

Nanyi mwaniita Mwalimu na Bwana nanyi mwasema vema maana ndivyo nilivyo.

Maneno hayo yatueleza wazi kwamba alikuwa anajua wazi kwamba yeye ni Mwalimu na Bwana ndiyo maana anawasifu wanafunzi wake, NANYI MWASEMA VEMA.

Mathayo 23:9 imeandikwa: -

Wala msimwite mtu Baba maana Baba yenu ni mmoja wa Mbinguni wala msiitwe Kiongozi maana Kiongozi wenu ni mmoja naye ndiye Yesu Kristo.

Hapa Yesu anaendelea kutuonyesha jinsi alivyo tofauti na Mungu, na yeye hayuko sawa na Mungu daima Mungu ni Baba lakini Yesu ni Kiongozi tu.

Ufunuo: 1:1-2 imeandikwa hivi: - Ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu awaonyeshe watu wake…Naye akatuma Malaika akamuonyeshe Mtumwa wake Yohana…

Wakati ufunuo unatolewa na Mungu na kupewa Yesu wakati huo Yesu ameshatoka Duniani yuko Mbinguni
(kwa mujibu wa bible), lakini bado inaonyesha Mungu ndiye mkubwa Yesu bado ni wakutumwa ili awaonyeshe watumwa kuhusu mambo yao yatakayokuja kama tulivyosoma.

Zipo Aya nyingi sana zinazoonyesha wazi kuwa Yesu alikuwa halijui kabisa fundisho la tatu na wala kuhusu kuwa yeye ni Mungu.
 
Siiamini hata nukta.

Ndio sababu tukaisoma Biblia na ukristo ili tuwaonyeshe imeandikwa kitu gani kinyume na mnavyopotoshwa na wasaka tonge wachungaji matapeli huko makanisani kwenu
 
Nchi nyingi zenye mlengo wa uislamu au majimbo mengi ya nchi yenye mlengo wa uislamu uwa ni kitovu cha ugaidi na maeneo hayo usifika kwa kuzalisha makundi mengi ya Kigaidi.

Sisemi tu kwa sababu nasema bali nasema kwa sababu zipo nadharia nyingi zinazoonesha kuwa ni kweli maeneo hayo ukumbwa na matukio ya kigaidi ama Vita.

Hata Tanzania miaka kadhaa ya nyuma kulikuwa na tetesi za matukio ya kigaidi maeneo ya Kibiti na jirani na maeneo hayo ambayo kwa wingi ukaliwa na watu wa Dini ya uislamu kitendo kilichopelekea Jeshi la Tanzania kuwekeza nguvu huko Kibiti na kutokomeza ugaidi huo ambao ulikuwa umeanza kumea katika maeneo hayo ya pwani ya Tanzania. Hata kijana mmoja wa kitanzania mwenye mlengo wa Dini ya kiislamu aliwahi kukamatwa Kenya akitumikia kikundi cha kigaidi cha Al-Shabab.

Ukiachilia mbali hayo, Duniani ukitamka neno ugaidi alafu ukasema tutajie dini yenye kuhusishwa na ugaidi moja kwa moja hata mtoto atakutajia Uislamu. Na hii ni kwa sababu Watu wote wanaokamatwa katika matukio hayo basi ujinasibu kama wanapigania Dini ama maslahi yao ya kidini. Ukiachilia mbali kupigania Dini au Maslahi ya Kidini. Nchi hizo hizo au maeneo hayo hayo yamekuwa yakikumbwa na Mapinduzi ya kijeshi na watu hao wakitaka kusimika dola la kiislamu.

Alikadharika maeneo hayo uwa yanakumbwa na vurugu za kivita za mara kwa mara.

Hapa Afrika ukitoa Congo DRC tu ambayo haina waislamu wengi, nchi nyingi zilizobaki zenye vita za mara kwa mara maeneo hayo yenye vita ukaliwa na waislamu kwa idadi kubwa.

Ukanda wote wa Sahel, yani kusini mwa mpaka wa jangwa la Sahara, nchi kama Sudan, Niger, Mali, Burkinafaso, Chad na nyinginezo na nchi zinazokumbwa na vikundi vya kigaidi mara kwa mara. Na ni nchi zenye uislamu mwingi na kama unavyoona zinapakana na nchi za waarabu wa kiafrika ambazo kwa asilimia 90 raia wa nchi hizo ni waislamu.
View attachment 2943395
Nigeria pia ni miongoni mwa nchi inayokumbwa na matukio ya kigaidi sana hususani Maeneo ya kaskazini ya nchi hiyo ambayo ukaliwa na waislamu wengi. Nchini Nigeria wakristo wengi wanapatikana Kusini katika majiji kama Lagos, na Abuja, na waislamu wengi upatikana maeneo ya Kaskazini mwa nchi ambayo mara nyingi majimbo ya Maeneo hayo uongozwa kwa Sheria za kiislamu, pia nadhani juzi kati katika mfungo wa ramadhani watu wa maeneo hayo walikamatwa kwa kutokufunga Mfungo wa Ramadhani na waliadhibiwa. Maeneo hayo hayo ndio kituo cha Kundi la Boko Haram na vikundi vingine vya namna hiyo.

Tukiama barani Afrika tukaamia bara la Asia ukanda ya Middle East (Mashariki ya Kati) ambapo ndiko uislamu umeanzia huko ndiko kuna vikundi vingi vya kigaidi, na karibia kila nchi ina vikundi vyake. Nadhani wengi mnavifahamu vikundi kama Hamas kilichoishambulia Israel na kuteka na kuua watu katika tamasha la mziki, na kupeleka vita ambayo imeigharimu ardhi ya Palestina ukanda wa Gaza. Vilevile haikupita miezi mingi kuna kikundi kutoka Yemen nacho kinaitwa Hauthi kikaanza kulipa mashambulizi kwa kupiga meli zinazopita ukanda wa bahari ya sham bila kujali kuwa anaepigwa ni raia wa nchi gani.

Ukiachilia mzozo huo wa Israel na maadui zake, hakuna asiyejua kundi la kigaidi lenye mlengo wa kiislamu lililotikisa Dunia kwa matukio ya kutisha kwa kuchinja, kupiga risasi au kujitoa Mhanga. Hii ya kujitoa mhanga ikapelekea Waislamu hasa waliojifunika mwili mzima kuogopwa sana kuhisi labda wamebeba mabomu ya kujitoa mhanga. Chini ya Osama Bin Laden, kundi hili liliisumbua Dunia hasa Marekani kwa kuipa Jeraha lisilosahaulika la Septemba 11.

Kwa kifupi huko Middle East (Mashariki ya Kati) kuna vikundi vingi sana vya kigaidi, vingine vinakuwaga vimelala tu, vinakuwa (Inactive) lakini viko tayari kwa mashambulizi. Na vikundi hivi ndivyo vinafanya Dola za kiislamu zinaendelea kusimama na sheria kali za kiislamu zifatwe, mfano moja wapo ni Kundi la Taliban kutokea pale Afghanistan ambalo baada ya kushika dola tu likaweka sheria kali za kiislamu ikiwemo wanafunzi kusoma madarasa kwa kuzingatia jinsia mpaka chuo kikuu yani mtoto wa kike na wakiume kila mtu darasa lake.

Kundi jingine la Kigaidi ni kundi la ISIS yani Islamic State. Kundi hili juzi kati limekiri kupiga Tukio pale Russia kwa kumimina Risasi katika Mall moja pale Moscow kwenye tamasha la mziki na kuua watu zaidi ya 150 na kuchoma jengo kwa vilipuzi. Lakini Rais wa Russia Vladimir Putin hajawaacha salama, kawadaka watu kadhaa ambao wanahusika na tukio hilo ambao wengi wao wanasema wamekodiwa kutokea nchi ya Uturuki ambayo ni yenye mlengo wa kiislamu.

Kwa ufupi makundi haya ni mengi sana na yana uhusiano wa moja kwa moja, kwa sababu mengi yanakuwa na link au uhusiano.

Kwani ndugu zetu waislamu mnapokuwa mnafundishwa Dini uwa mnapewa maelezo gani yanayowatia baadhi yenu mioyo ya kikatili, kutaka kumwaga Damu?
Hii ni dini iliyoanzishwa na kuenezwa kwa Jihad. Watu walilazimishwa kujiunga Uislamu karne ya 6-13 kwa lazima na siyo kwa hiari. Kama hukutakq Uislamu enzi hizo basi panga lilikuwa halali yako.

Hii ndiyo sababu ya vitavmaeneo hayo. No room for reasoning
 
Ndivyo mnavyolishwa matango pori na wachungaji wenu ??

Mambo hayo ya kulazimishwa ni ukristo , kwani kama kuna kulazimishana nyinyi nyote huku mngalikuwa waislamu kwani uislamu ulikuja mwanzo kuliko ukristo huku kwetu

angalia hii documentary ya BBC kuhusu ukristo ulivyoanza

View: https://www.youtube.com/watch?v=OnNBLLcN-fY&pp=ygUSamVzdXMgdGhlIGV2aXNlbmNl
 
Uislamu wenyewe ulianzishwa na Wakatolilki karne ya 6 ili kupambana na Dola ya Kirumi. Wakaandika kitabu wampa Muhamad halafu nyie mnadanganya kuwa aliteremshiwa kwa miaka 23. Wajinga ndiyo waliwao
 
Ndio sababu tukaisoma Biblia na ukristo ili tuwaonyeshe imeandikwa kitu gani kinyume na mnavyopotoshwa na wasaka tonge wachungaji matapeli huko makanisani kwenu
Hakuna muislam anayeweza kuielewa bible,hata Allah mwenyewe hawezi.

Sababu kila muislam anaisoma huku amekariri Quran kwanza.

Wacha nikuulize swali,unaamini Bible,ama vitabu ndani yake ni vya Mungu???
 
Tuiulize biblia yenyewe iseme
 
Tuiulize biblia yenyewe iseme
Bible hainaga tabia ya kujitetea wala kujieleza sana,wewe soma ukiamua uiamini sawa,ukiichukulia poa ni juu yako.

Leo hii hakuna muislam asiyependa au asiyetaka kufunua ajue kilichopo ndani yake,ila ni ngumu kukuta mkristo anapekua Quran,iman yetu juu ya bible haina mashaka kabisa,na kama tukiipoteza hakuna kitabu kitakuwa na mantiki tena kuhusu Mungu.
 
Unaongelea biblia ipi ambayo haisemi Yale yaliyoandikwa ndani yake ?
 
Uislamu wenyewe ulianzishwa na Wakatolilki karne ya 6 ili kupambana na Dola ya Kirumi. Wakaandika kitabu wampa Muhamad halafu nyie mnadanganya kuwa aliteremshiwa kwa miaka 23. Wajinga ndiyo waliwao
Yaani wakristo waanzishe uislamu unaosema Yesu si Mungu , Yesu hakusulubiwa, Hakuna utatu Mtakatifu, Maria si mama wa Mungu ? Nani kakulisha matango pori yenye sumu ?
 
Mimi ndio nilyekuuliza , nijibu kwanza swali langu
Wewe mbona hufanyi hivyo??

Nilikuuliza awali,unaiamini Bible ama vitabu vyake kama ni kutoka kwa Mungu??

Embu jibu kwanza hapa.
 
" (الله أَكْبَرُ من كلِّ شيء)."
 
Wewe mbona hufanyi hivyo??

Nilikuuliza awali,unaiamini Bible ama vitabu vyake kama ni kutoka kwa Mungu??

Embu jibu kwanza hapa.

Miswada sahihi

Wanazuoni wengi wa madhehebu na vikundi mbalimbali vya Kikristo wamethibitisha kuwa sehemu kubwa ya maandiko ya Biblia ina mashaka makubwa juu ya uhalisia wake.

Katika utangulizi wa Ngano za Mungu mwenye Mwili, Mtunzi ameandika yafuatayo:
"Katika karne ya kumi na tisa, Wakristo wa Kimagharibi walifanya marekebisho makubwa mawili ili kuitikia wito wa kupanuka kwa elimu ya wanadamu: imekubalika kuwa mwanadamu ni sehemu ya maumbile na ameibuka kuwa ni miongoni mwa wanamageuzi wa mfumo wa maisha duniani; imekubalika kuwa vitabu vya Biblia vimeandikwa na watu tofauti tofauti katika matukio tofauti tofauti na haviwezi kukubaliwa kuwa ni utunzi wa Mungu wa neno kwa neno.

Katika gazeti la kimataifa la, Newsweek2F3, lililobeba makala yenye kichwa 'Oo Bwana, Nani Aliyeandika Dua hii?'

kikosi cha wanatiolojia kutoka katika dhehebu kuu la kiporestanti, pamoja na Wasomi muhimu wa Biblia wa Kikatoliki nchini Marekani, baada ya ukaguzi wa kina wa miswada ya mwanzo kabisa ya Agano Jipya, wamehitimisha kuwa maneno pekee ya "Dua ya Bwana" ambayo yanaweza kunasibishwa barabara na Yesu Kristo ni "baba".

Na hilo, ni kwa mujibu wa wasomi hao wa kanisa, maneno yote yaliyokuja baada ya ibara ya kwanza, "Baba yetu", ambayo ni dua muhimu sana ya Kikristo, yaliongezwa karne nyingi na waandishi wa kanisa walionukuu miswada ya mwanzoni ya Injili.

Shirika la U.S News & World Report, linanukuu zaidi kuwa, kikundi cha wasomi kilisema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya maneno yaliyoandikwa katika Injili kumhusu Yesu huenda ni ya kubuniwa.

Miongoni mwa hayo likiwemo neno la Ekaristi ya Yesu ,katika Karamu ya Mwisho ("Chukua, kula. Huu ni mwili wangu…") na kila neno aliloambiwa kuwa amelitamka toka msalabani.
 
Wala hamna tatizo,ukisema utumie akili dkk 1 tu,hakuna kitu utakipokea ktk bible pale ni iman ndio inafanya kazi.
Katika utangulizi wa Ngano za Mungu mwenye Mwili, Mtunzi ameandika yafuatayo:
"Katika karne ya kumi na tisa, Wakristo wa Kimagharibi walifanya marekebisho makubwa mawili ili kuitikia wito wa kupanuka kwa elimu ya wanadamu: imekubalika kuwa mwanadamu ni sehemu ya maumbile na ameibuka kuwa ni miongoni mwa wanamageuzi wa mfumo wa maisha duniani; imekubalika kuwa vitabu vya Biblia vimeandikwa na watu tofauti tofauti katika matukio tofauti tofauti na haviwezi kukubaliwa kuwa ni utunzi wa Mungu wa neno kwa neno.
Kwanza tukubaliane kitu,bible ina maandiko yenye wasifu wa aina mbali mbali,kuna historia za watu,manabii na mitume,hakuna sehem yeyote panapodai bible imeandikwa na Mungu.huu upuuzi unapatikana ktk Quran tu.
Katika gazeti la kimataifa la, Newsweek2F3, lililobeba makala yenye kichwa 'Oo Bwana, Nani Aliyeandika Dua hii?'

kikosi cha wanatiolojia kutoka katika dhehebu kuu la kiporestanti, pamoja na Wasomi muhimu wa Biblia wa Kikatoliki nchini Marekani, baada ya ukaguzi wa kina wa miswada ya mwanzo kabisa ya Agano Jipya, wamehitimisha kuwa maneno pekee ya "Dua ya Bwana" ambayo yanaweza kunasibishwa barabara na Yesu Kristo ni "baba".

Na hilo, ni kwa mujibu wa wasomi hao wa kanisa, maneno yote yaliyokuja baada ya ibara ya kwanza, "Baba yetu", ambayo ni dua muhimu sana ya Kikristo, yaliongezwa karne nyingi na waandishi wa kanisa walionukuu miswada ya mwanzoni ya Injili.

Shirika la U.S News & World Report, linanukuu zaidi kuwa, kikundi cha wasomi kilisema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya maneno yaliyoandikwa katika Injili kumhusu Yesu huenda ni ya kubuniwa.

Miongoni mwa hayo likiwemo neno la Ekaristi ya Yesu ,katika Karamu ya Mwisho ("Chukua, kula. Huu ni mwili wangu…") na kila neno aliloambiwa kuwa amelitamka toka msalabani.
Haya naomba msimamo wako sasa.rejea swali.
 
Back
Top Bottom