mkorinto umeona unafiki huu?
Kafir US leo kwa jiwe kuu la msingi🤣 daah kosa yote upate elimu.
Kumbe ndio maana wanajaha na Israel bila kujua wao ndio chanzo.
Under the leadership of Prophet Mohammad, many lives were killed or forced to convert.
Toleo la Agano Jipya la Revised Standard Version lilichapwa mwaka 1946."
Toleo la Biblia la Revised Standard Version, linajumuisha Agano la Kale na Jipya, nalo lilichapwa mnamo Septemba 30, 1952, na likakubalika sana."
Katika Toleo la Biblia la Revised Standard Version, idadi kubwa ya mistari muhimu kutoka katika Toleo la King James Version ya Agano la Kale na Jipya, ambayo wasomi waliiona kuwa imeongezwa katika karne za baadaye, iliondoshwa kutoka katika matini na kuwekwa katika tanbihi.
Kwa mfano, kifungu maarufu sana katika Injili ya Yohana 8:7 kinachohusu mzinzi aliyetakiwa kupigwa mawe. Inasemakana Yesu amesema: "Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe."
Tanbihi za Toleo la King James (1952) zinaeleza "Mamlaka za kale mno zinaondosha aya za 7:53 – 8:11"
Kwa kuwa mswada namba 1209 wa Vatikani na mswada wa Sinaitic ya tangu karne ya nne haina aya kumi na mbili hizo, wasomi wa Biblia wamefikia uamuzi wa kuwa maneno hayo hayatoki kwa Yesu.
Mfano mwingine ni kifungu kinachohusishwa na Yesu na kinachotumika kama ushahidi wa rejeo la Utatu katika Maandiko matakatifu. Katika 1 Yohana 5:7, Inasemakana Yesu amesema: "Kuna watatu wanaoshuhudia huko mbinguni, Baba, Neno na Roho Mtakatifu: na watatu hawa ni mmoja"
Msomi maarufu sana wa Biblia, Benjamin Wilson, anaandika kuwa; maandiko haya yanayohusu "ushahidi wa mbinguni" hayamo katika mswada wowote wa Kigiriki ulioandikwa kabla ya karne ya kumi na tano!
Kwa hiyo, katika Toleo la Biblia la Revised Standard Version, mstari huu umefutwa na kutolewa katika matini tena bila ya kuwekewa tanbihi.
Hata hivyo, ili kuwe na idadi ya mistari iliyosawa baina ya Toleo la Biblia la Revised Standard Version, na ile ya Toleo la Biblia la King James Version, warejeaji wameugawa mstari wa sita na kuwa mistari miwili.
Toleo la pili la tafsiri ya Agano Jipya (1971) limefaidika kwa tafiti za matini na isimu tangu lilipotolewa toleo la The Rivised Standard Version, kwanza lilitolewa mwaka 1946.
Kwa hiyo, baadhi ya vifungu vilivyofutwa zamani viliandikwa upya, na baadhi ya vifungu vilivyokubaliwa vilifutwa.
"Vifungu viwili, vya mwisho mrefu wa Marko (16:9-20) na kifungu cha mwanamke aliyekamatwa kwa uzinzi (Yohana 7:53 – 8:11), vilirejeshwa katika matini, zikitenganishwa kwa nafasi wazi na zikiambatana na nukuu za kauli taarifa…
Kukiwa na kuungwa mkono na miswada miwili, vifungu viwili, Luka 22:19b-20 na 24:51b, vilirejeshwa katika matini, na kifungu kimoja, Luka 22:43-44, kiliwekwa katika tanbihi, kama ni ibara katika Luka 12:39."