#COVID19 Kwanini nchi zilizochanja wananchi wake na kuchukua tahadhari zote ndio zinaendelea kuongoza kwa maambukizi na COVD-19

Na ile taarifa iliyotolewa juzi katika kituo kimoja cha habari nchini Marekani ya kwamba wanaopoteza maisha kwa Covid 19 ni wale ambao hawakupata chanjo,mtoa uzi huu unalizungumziaje kwa upande wako
Ulitaka waseme otherwise ili watu wasichome chanjo .....?!

Hili unalizungumziaje kwa upande wako?!
 
Una uhakika na hizo source hawatumanipulate na hizo information zao kwa manufaa yao binafsi??
 
Unasimamaje na alie lala...??
Mambo ya corona virus ni magumu kuelewa lakini.
Hayana ugumu wowote, Ni simple logic
Tabia hatarishi zipo kwa asilimia 100, lakini maambukizi Ni asilimia 0.
Kumbuka tangu tumeanza kutishwa na watanzania wenzetu wanaojikweza, huku wakisema sisi watanzania hatuna akili, kana kwamba wao Ni wamarekani.
Wakati wa mazishi ya hayati kwa mfano , Hawa wajikwezao walisema Sana humu kutokana na umati ule na kutozingatia kanuni za watu wale, wakatabiri kwa hesabu zao mbovu kwamba baada ya wiki mbili kutakuwa na msiba mkubwa maana watanzania wengi watakufa kwa corona, Nani anaweza kushuhudia kwamba baada ya maombolezo Yale, Ni waombolezaji wangapi walikufa au hata kuugua corona!!!?
Je watanzania wanavyojaa kwenye nyumba za ibaada, kumbi za starehe, viwanja vya michezo na mausafiri ya umma
Mnasemaje???
Nauliza watu mnaojisingizia kuwa na akili kuliko akili yenyewe!!!
 
Kama kuna watu wanafanya utafiti wa corona na madhara yake..
basi waanzie kwenye mwendo kasi
Halafu ile tume ya corona, ilitumwa kutafiti Hali ya corona Tanzania, Jambo la kushangaza , ripoti yao Haina maelezo yanayoonesha Hali ya corona Tanzania, badala yake wamekuja tu na mapendekezo namna ya kukabiliana na corona , ambayo hawajatuambia ipo kwa kiasi gani....
 
Mshukuru Mungu tunaomba anatujibu na sio kwamba sisi ni wema kuliko hao,unakosea kusimama na mfu, usije ukamfuata.
 
Tunazungumzia corona kama ugonjwa hatari sana na wenye kuambukiza kwa kasi na usio na dawa, Tanzania ambayo imeacha kuchukua tahadhari za kujikinga na huu ugonjwa kwa kipindi kirefu, hivyo tungetegemea hali ya maambukizi kwa huu ugonjwa kuwa mbaya hivyo tungeona japo huduma za hospitali kuelemewa kutokana na kutofuata njia za kujikinga na maambukizi ya huu ugonjwa, nakumbuka kuliwahi kutokea uvumi wa kwamba Dar hospitali zimezidiwa wagonjwa wa corona, hiyo yote ni kutokana na jinsi tulivyokuwa tuna shughulikia hili suala la corona na ndio hali tunayoendelea nayo hadi sasa.
 
Ni kweli kabisa, mfano humu huwa kuna watu wanadai kwamba madaktari huko mahospitalini ndio wanajua uhalisia wa corona, hivyo nilitaraji kusikia hilo suala kwenye ile ripoti ila ndio kwanza tunaona rais mpaka juzi hapo anaenda kutembelea hospitali huku akiwa hana taarifa zozote kuhusu uwepo wa wagonjwa wa covid kwenye hiyo hospitali.
 
Again. Wewe na watu wengi wenye mlengo wa Magufuli kuna details mnazi-mis. Hii ni kutokana na pengine kutokuelewa kiingereza sawasawa au uvivu wa kusoma makala na maelezo ya kitaalam kuhusu huu ugonjwa. Unaposikia vifo au hospital kuelemewa katika nchi kama USA au Ulaya kwa ujumla, wengi wa victims ni wazee wa miaka 65 na kuendelea. Sasa niambia, Bongo population ya wazee ipo kwa kiasi gani? Wazee wengi wenye miaka hiyo walishatangulia mbele ya haki. Kwa kuangalia demografia ya population ya nchi yetu, wengi ni miaka 35 kwenda chini, na huu umri kwa korona huwezi kuona effects zake kwa ukali. Bado nasisistiza statistics kama zingekuwa zinachukuliwa, Tanzania tumeshapoteza watu wengi tu kwa kulinganisha na umri wa population yetu. Nyie mnapiga bla bla bila na kulinganisha nchi inayoacha mambo yajiendee vs nchi zinazorekodi karibu kila mgonjwa na vifo.
 
Mkuu ni nani yuko responsible kutoa takwimu? Serikali kupitia Wizara ya Afya au watu Kitaa? IMF imetunyima mkopo wa $574 millions ili kupunguza athari za uchumi zilizosababishwa na COVID-19 mpaka hapo Serikali itakapoanza kutoa takwimu za kila siku kuhusu wagonjwa wa Covid nchini.

Utajuaje athari ya bila takwimu?
 
Juzi kasema juu juu tu kwamba kuna wagonjwa zaidi ya 100 nchini bila ya kusema wako mikoa ipi na idadi ya waliokufa na kama Serikali inafuatilia watu wa karibu wa hao wagonjwa zaidi ya 100 ili kujua wako salama au tayari wana maambukizi.

 
Unajua kuna dunia hii wainga hawaishi. Dunia yote kuanzia Uchina, Ujapani, India, Uarabuni, Urusi, Ulaya Magharabi, Mashariki ya Kati na Amerika wote wanazungumza lugha moja. Halafu wanatokea wajinga wachache wenye shahada za sayansi za uchochoroni wanawakosoa. Ujinga ulioje huu. Nilimsikia rais Samia juzi alipoulizwa maswali anasema anadhani mtu akijifukiza wakati virus ''wakiwa bado koooni'' kabla hawajaingia kwenye mapafu wanaweza kufa!!! Hii unaweza kuona kabisa ni sayansi ya vichakani na watu hawajui hata kidogo virus wanavyoambukiza na kusambaa ndani ya mwili. Magufuli hivyo hivyo alikuwa anasema ukijifukiza na mvuke wenye temperature 100 degraa cg eti virus hawa-survive!!!! Unaweza kuona kabisa hawajui jinsi virus wanavyoji-attach kwenye cells za mwili
 
Nadhani jamaa yupo sahihi, kwani kwa maisha yetu haya kama kuku wa kienyeji tungekuwa tumeshakwisha kabisa!!!lakini baada ya hofu kuondolewa maisha yanaenda kama kawaida tu sio kama ugonjwa haupo.Approaches nyingi za meko nilikuwa sikubaliani nazo kabisa lakini kwa hili la COVID19, hapa nampa shikamoo huko alipo!!Na ndio maana hata sasa itakuwa ngumu kwa wananchi kuelewa somo kwani ni mwaka sasa ugonjwa upo, na yeye maisha yanaendelea kama kawaida!!TUSITIANE HOFU.
 
Juzi kasema juu juu tu kwamba kuna wagonjwa zaidi ya 100 nchini bila ya kusema wako mikoa ipi na idadi ya waliokufa na kama Serikali inafuatilia watu wa karibu wa hao wagonjwa zaidi ya 100 ili kujua wako salama au tayari wana maambukizi.
Hizo ni takwimu tu za kuchukulia pesa kutoka IMF, WHO.hakuna lolote na wasiwatie wananchi hofu, chanjo sawa zije na anayetaka achanjwe!!aliyewalinda mwaka mzima ndio atakayeendelea kuwalinda tu, japo tahadhari ni muhimu.
 
Eti dhalimu alikuwa sahihi na bado akakimbilia chato kujificha kwa miezi miwili!!! Na kwa ubishi wake wa kutotaka kuvaa masks mwenyewe aliyaita matambara basi COVID-19 haikufanya ajizi bali kulala naye sambamba leo anaitwa MWENDAZAKE!!!! Hakuna anayekutisha ni maisha yako mwenyewe na MAKABURI umeyaona. Chukua hatua muafaka za kujikinga ubishi wa kijinga KAMWE hautakukinga kumbuka zaidi ya watu 3.5 duniani Covid-19 imesitisha uhai wao.

 
Eti takwimu za kuchukulia pesa IMF!!! 😂😂😂unadhani IMF ni Wapumbavu kiasi hicho!?


Hizo ni takwimu tu za kuchukulia pesa kutoka IMF, WHO.hakuna lolote na wasiwatie wananchi hofu, chanjo sawa zije na anayetaka achanjwe!!aliyewalinda mwaka mzima ndio atakayeendelea kuwalinda tu, japo tahadhari ni muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…