#COVID19 Kwanini nchi zilizochanja wananchi wake na kuchukua tahadhari zote ndio zinaendelea kuongoza kwa maambukizi na COVD-19

Hao wimbi la kwanza ungewafahamu vipi kama sio kupitia takwimu zilizokuwa zinatolewa?!

Hizo nchi zingine umejuaje kwamba, pamoja na tahadhali zote wanazochukua lakini ndizo zinazoongoza kwa maambukizi kama sio kupitia takwimu wanazotoa kila siku?
Mkuu wimbi la kwanza kila.mgonjwa aliyefariki hakuambiwa amefariki na nini kama utakumbuka kuna waliolalamika ila pia kulitokea vifo vingi kiasi

IMPACT YAKE ilionekana VIVID Mtaani ila sil Kwa kiwango cha nchi zingine LILIPOPITA tumekuwa shwari kabsaa ukiachana na vifo vya viongozi ila kitaa shwari tu
 
Kwa nini nchi zinazotumia dawa za kuzuia au kutibu ugonjwa wa malaria ndizo pia zinazoongoza kwa maambukizi ya malaria?
 
Jamaa mbika una kumbukumbu za KUKU??

Nyungu za MUHIMBILI zikipozinduliwa unakumbuka walivyosema madaktari??

Unakumbuka Chanjo ya NIMRI walipoizindua walituambiaje?


So far mtaani kwako kuna wagonjwa that we dont know??

Tujifanye hatujui ulipo hii nyomi ya vyombo vya usafiri inafanana na nyomi za hospitalini kuhusu "changamoto ya upumuaji", pumu, and the like?
 
Na tarehe 3 tunaenda kujazana kwa Mkapa tukitoka hapo tunajazana kwenye daladala.
Hili wimbi la 3 sijui itakuwaje
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Acha upumbavu banaaa!!!! Lile la nyungu lilikuwa ni SHINIKIZO la dhalimu mwendazake wewe!!!! Na kutaka kutuaminisha Watanzania kwamba hatuna haja ya chanjo. Watanzania tumetumia chanjo mbali mbali kwa miaka chungu nzima lakini yule dhalimu mwendazake kwa kuwa alikuwa na Phd FAKE akawaingilia hata madaktari watoe kauli alizotaka yeye tuzisikie vinginevyo wangempinga wangefukuzwa kazi. Tumia akili yako japo KIDUCHU.

 
Kwa upande wangu, inabidi tusidhani sisi ni kisiwa na kwamba Mungu anatupenda zaidi kuliko wanaofariki. Labda kama ni kupenda, basi anawapenda zaidi hao wanaofariki kwa corona (kama tulivyozoea kusema ndugu, jamaa na rafiki akituacha: sisi tulimpenda, lakini Mwenyezi Mungu kampenda zaidi). Nitoea mfano huu. Mimi natoka UK ya Tanzania na wakati ugonjwa wa ukimwi ulipopiga sana, sisi UK tulidhani tuko salama na wanaofariki ni watu wanaoishi mjini. Hivyo, hatukuchukua tahadhari sana za kujikinga na watu waliendelea na maisha yao kama kawaida au kama hakujawahi kuwepo na ukimwi. Lakini leo hii nenda UK ya Tanzania na waulize watu kuhusu ukimwi kama umepiga sana au la na ujaribu kulinganisha na mjadala wetu huu. Itoshe tu kusema, kama hatutakuwa waangalifu na kuchukua tahadhari tutajifunza kwa njia ngumu maana tunaweza kudhani hao wagonjwa 100 aliowataja Rais kabla ya kugundua kama ni wagonjwa walishawaambukiza wangapi au je ndugu wa wale ambao wana virusi, lakini siyo serious si wanatunzwa au wanaangaliwa na ndugu zao? Na 'kidogo kidogo hujaza kibaba'. Hivyo, tusidharau kitu hata kama idadi bado ni ndogo maana hata hao walioathiriwa zaidi walianza pia na idadi ndogo tu ya wagonjwa.
 
Mimi niko Marekani hapa, we ni nani amekwambia hivyo? Kinga hizi zina kiwango cha efficacy yake na data ziko wazi. Hakuna kinga ambayo ni 100% na hizi hali kadhalika. Mfano Pfizer nadhani efficacy yake ni 96%. Hii ina maana kuna asilimia 4 ambao bado wanaweza kuambukizwa hata baada ya kuchanjwa. Na uzuri ni kwamba hata waliochanjwa wakiambukizwa mara nyingi severity ya ugonjwa ni ndogo na hata hawahitaji kulazwa labda kama ni wazee au kama wana compromised immune system kutokana na magonjwa kama kansa na mengineyo yanayoshambulia kinga ya mwili. Marekani hapa kila kitu kilikuwa kimefungwa nchi inapoteza mabilioni ya dola kila siku na sasa wamechanjana zaidi ya asilimia 60 kila kitu kimefunguliwa na maisha yanarudi kama kawaida. Sasa hizi stori za vijiweni huko sijui mnazipata wapi!
 
Hivi kwa Nini tunalazimishwa kuchukua mkopo kupambana na covid?

Na kwa Nini mkopo huo uwe na masharti ya jinsi ya kuutumia?

Nadhani Kuna shida kubwa Sana juu hili Gonjwa?

Je, hiyo chanjo mbona wanasema IPO kwenye majaribio?

Km IPO kwenye majaribio,kwa Nini ilazimishwe kutumika moja kwa moja kwa binadamu?

Je, uhakika ya kwamba inakinga Ni upi wakati IPO kwenye majaribio??
Na, kwa Nini hyo chanjo watu wachanje na bado tahadhari waendelee kuchukua??

Sasa Nini logic ya kuchanja??

Ni sawa na uchomwe chanjo ya sulua na bado unaambia usitoke nje, utaambukizwa kwa Nia ya hewa, Sasa nini maana ya chanjo?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mkuu nchi ina maigizo sana hii
 
Reactions: BAK
Malaria ipo nchi za TROPICAL sanasana
Lakini si watu wanaoishi nchi za tropical ingawa wanatumia dawa, lakini wanafariki pia? Mfano, kwa mujibu wa www.severemalaria.org, Tanzania is among the ten countries with the highest malaria cases and deaths (3% of the global cases, 13.4% of cases in East and Southern Africa and 5% of global deaths).
 
Mkuu kumbuka this is fake news NO KORONA
 
Ao mkuu mpo salama kwa 96%???
 
Hayati Magufuli hakuwa dhalimu kama ulivyo mwongelea hapo juu vibaya. Instead alikuwa mpenda haki, kipenzi cha wanyonge, mchapa kazi, asiyependa ufisadi na unyonyaji mwana mwema wa Africa. Wanao na wajukuu zako watasoma hivyo na wataelewa.
Mwenye chuki kama wewe ni muhanga wa matendo mema ya jpm. So sadist Pole.
 
Corona bongo haipo watuache tuendelee na uzalishaji haya mambo ya wanaharakati wa bongo kushadadia kila kitu cha kimagharibi ni upuuzi.
 
Tena unacjomwa AT YOUR OWN RISK
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…