Huo Moshi kwa ufupi unaitwa MPEMBA EFFECT.
Erasto Mpemba alikuwa akichemsha maziwa na anaingiza kwenye friji wakati akiwa shule. Wenzake waliweka bila kuchemsha. Ila maajabu yalikuwa kwamba maziwa yake yaliganda mapema kuliko ya wenzake.
Alipomuambia Mwalimu alimuona kichaa kwani kwa sheria za Fizikia ni yale ya baridi yalitakiwa kuganda mapema kwa formula iitwayo q=mct (hii usiniulize kwa Kiswahili maana siwezi kuilezea)
Baada ya utafiti hapo UDSM na nchi za nje, waliamua kumuenzi Mtanzania huyo kwa kuipa hiyo kitu Mpemba Effect.
Kwa maana hiyohiyo, moshi/hewa na maji yanayotoka kwenye ndege ikiwa juu, yanaganda haraka sana na kutengeneza barafu ambayo unaiona. Baada ya muda huchanganyika au kulingana na eneo jingine na kupotea.
Ukiweza angalia hii video chini:
Mkuu Mwamba028, swali lako kwa nini ndege zinapita juu sana ni kwa sababu wanataka kuchoma mafuta kidogo kwa safari za mbali. Tuseme kama ndege ya KLM inapotoka asubuhi Schiphol Airport na kufika usiku Kilimanjaro na huwa angani kama masaa 10. Ili kupunguza utumiaji wa mafuta basi ndege huenda 10 km juu ya usawa wa bahari. Huko ndiyo huanza safari kwa speed ya 1000km/hr. Faida ya kuwa huko juu sana ni kwamba kwanza Gravitation (Msukumo uliopo kwenye sayari ya dunia kuvuta vitu kwenye uso wake) ni kubwa na matokeo yake kuishikilia ndege angani inahitaji mafuta mengi uchome. Ukiwa 10km angani, gravitation inapungua na unaokoa mafuta.
Pia upepo mkali uliopo ardhini huko juu unapungua hivyo ndege inateleza taratibu bila msuguano mkali na ardhi. Ila wanaweka hapo na si juu zaidi kwa sababu mambo ya hewa na Pressure wakipandisha ndege juu zaidi inakuwa shida.
Kama unakumbuka yule jamaa wa Baloon la Red Bull, aliruka hadi akawa amekaribia umbali huo bila kuwa na mitungi ya hewa ya Oxygen.
Mapanga Boy yanahitaji Msuguano na hewa ili yaendelee kuishika ndege angani na kusonga mbele. Hivyo huwa zinakuwa hazipai angani sana. Kama sikosei hata zetu zitakuwa zinakwenda kwenye speed hiyo ya 700km/hr na urefu kama 7km kutoka usawa wa bahari,
Wadau hamujaniambia kwann hizi ndege huwa zinapita juu sana kuliko ndege zingine
Nataka ninunue moja