Kwanini Ndege(Roketi/Contrail) huacha mstari wa Moshi Mweupe?

Umenikumbusha mambo ya utotoni.

Ni hivi, zile ni ndege kama ndege nyingine tofauti yake ni kwamba zenyewe ni ndege kubwa ambazo zinaruka kwenye anga ya juu sana ambapo nyuzijoto zinakuwa hadi zaidi hasi ishirini (-2). Kwa hiyo moshi wa injini ya ndege unapotoka tu unaganda maramoja na ndiyo maana sisi huona kitu kama mstari. Kifupi ni hivyo
 
Siyo lazima mtu akiwa angani
afungue dirisha la ndege kujua hali ya joto iliyopo nje kwani vipimo vya ndani ya ndege vinatoa taarifa ya hali ya hewa iliyopo nje ya ndege kwa waliopo ndani ya ndege.

Ndiyo maana Enzi za Mwalimu wakati watanzania wengi walikuwa hawana fursa ya kusafiri kwenda Ng'ambo yeye alikuwa akienda na kurudi afu anaanza kupiga stori wakati wa kutoa hutuba zake hadhira ikawa inaona ni mambo ya ajabu sana.
 
Huo Moshi kwa ufupi unaitwa MPEMBA EFFECT.
Erasto Mpemba alikuwa akichemsha maziwa na anaingiza kwenye friji wakati akiwa shule. Wenzake waliweka bila kuchemsha. Ila maajabu yalikuwa kwamba maziwa yake yaliganda mapema kuliko ya wenzake.

Alipomuambia Mwalimu alimuona kichaa kwani kwa sheria za Fizikia ni yale ya baridi yalitakiwa kuganda mapema kwa formula iitwayo q=mct (hii usiniulize kwa Kiswahili maana siwezi kuilezea)
Baada ya utafiti hapo UDSM na nchi za nje, waliamua kumuenzi Mtanzania huyo kwa kuipa hiyo kitu Mpemba Effect.

Kwa maana hiyohiyo, moshi/hewa na maji yanayotoka kwenye ndege ikiwa juu, yanaganda haraka sana na kutengeneza barafu ambayo unaiona. Baada ya muda huchanganyika au kulingana na eneo jingine na kupotea.
Ukiweza angalia hii video chini:


Mkuu Mwamba028, swali lako kwa nini ndege zinapita juu sana ni kwa sababu wanataka kuchoma mafuta kidogo kwa safari za mbali. Tuseme kama ndege ya KLM inapotoka asubuhi Schiphol Airport na kufika usiku Kilimanjaro na huwa angani kama masaa 10. Ili kupunguza utumiaji wa mafuta basi ndege huenda 10 km juu ya usawa wa bahari. Huko ndiyo huanza safari kwa speed ya 1000km/hr. Faida ya kuwa huko juu sana ni kwamba kwanza Gravitation (Msukumo uliopo kwenye sayari ya dunia kuvuta vitu kwenye uso wake) ni kubwa na matokeo yake kuishikilia ndege angani inahitaji mafuta mengi uchome. Ukiwa 10km angani, gravitation inapungua na unaokoa mafuta.

Pia upepo mkali uliopo ardhini huko juu unapungua hivyo ndege inateleza taratibu bila msuguano mkali na ardhi. Ila wanaweka hapo na si juu zaidi kwa sababu mambo ya hewa na Pressure wakipandisha ndege juu zaidi inakuwa shida.
Kama unakumbuka yule jamaa wa Baloon la Red Bull, aliruka hadi akawa amekaribia umbali huo bila kuwa na mitungi ya hewa ya Oxygen.

Mapanga Boy yanahitaji Msuguano na hewa ili yaendelee kuishika ndege angani na kusonga mbele. Hivyo huwa zinakuwa hazipai angani sana. Kama sikosei hata zetu zitakuwa zinakwenda kwenye speed hiyo ya 700km/hr na urefu kama 7km kutoka usawa wa bahari,

Wadau hamujaniambia kwann hizi ndege huwa zinapita juu sana kuliko ndege zingine

Nataka ninunue moja
 
mm nazani kwa elimu yangu ya hapa na pale yaani ya kubahatisha kule juu kuna vumbi sana linalotimuliwa na hizo jets zenu
 
To add on FAZA1980, due to the combustion of the engine some aerosols are produced and discarded through the engine exhaust. These aerosols act as condensation nuclei - since the moist air above is at a supercooled level but lack condensation nuclei to form clouds; the moment the exhaust air is released into the atmosphere it supplies that needed nuclei hence instant cloud formation that lags the moving plane.
 
Kwa ndege na rocketi principle ni ile ile. nyuma ya engine kuna exhaust system ambayo hutoa compressed air ambayo ni ya joto kali sana. Joto hili linatoka kwenye mazingira ambayo temprature pamoja na pressure ziko chini sana na matokeo yake ni kwamba ile hewa yenye joto kali sana hukutana na mazingira ya baridi sana na ndiyo huo mstari mweupe uuonao.
Unaweza kujaribu hata nyumbani. Chukua chuma na ukiweke kwenye moto mkali kwa muda halafu ukitoe na kukiingiza chuma hicho cha moto kwenye maji baridi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] umewasamehe?
 
Mnatuchosha mimi mwenyewe mimacho kodoo kupata maujuzi lakini holaa.
Ule kweli sio moshi kabisa , kama ingekuwa moshi basi hiyo ndege au kama ulivyoita ingekuwa haifai kabisa

ninavyofahamu kutoka kwa wataalam wa anga wanasema: chombo kile kipo juu sana na kule kuna baridi sana kwahiyo kwakuwa chombo kile kinaproduce joto bac ile inakuwa ule ubaridi mkali kama unatoweka kwa minajisi ya mvuke ndio maana kwa kadri kinavyoenda mbali au kusogea basi ule mstari uliosema kama moshi ambao sio unatawanyika. yaani kama unarudia ile hali yake ya awali kwani lile joto la chombo kile halipo tena.

(pengine atatokea ambaye anaweza kueleza vizuri zaidi ya hapo tena kitaalam zaidi hiyo ni kwa kifupi tu na kirahisi rahisi)
 
Zile ni ndege za kawaida ambazo nyingi huruka zaidi ya km 11 toka usawa wa bahari. Sasa ule moshi wake huwa ni muunguzo wa mafuta na Oxijen kutengeneza maji na kabon dioxide. Yali maji yakitoka yanakuwa kati ka hali ya mvuke. Ule mvuke unachukua mda kuganda na kufanya matone ya maji ambayo baadaye hupotelea huko angani.
 
Joto kali linalotolewa na injini za ndege linapokutana na baridi kali iliyopo huko juu, funua kifuniko kilichoziba kitu kichemkacho utaona kitu hicho uitacho moshi, ikiwa na injini 2 ugaona miatari miwili, zikiwa 4 utaona mi4.
 
...jion hii kwa hapa dar ukiangalia juu utaona kitu kimepita kinaacha kitu kama njia au moshi ni nini hicho...mwenye kujua tafadhal
 
...jion hii kwa hapa dar ukiangalia juu utaona kitu kimepita kinaacha kitu kama njia au moshi ni nini hicho...mwenye kujua tafadhal
Ndege inapita kwenye international airspace ni juu sana na kwasababu kuna baridi hewa ya moto inayotolewa na engine ndio inasababisha hio njia kama moshi. Ukienda sehemu za baridi puliza/pumua kwa mdomo utaona kitu kama hicho.
 
Ndege inapita kwenye international airspace ni juu sana na kwasababu kuna baridi hewa ya moto inayotolewa na engine ndio inasababisha hio njia kama moshi. Ukienda sehemu za baridi puliza/pumua kwa mdomo utaona kitu kama hicho.
Asante...hio ni ndege ya kawaida au special ndege zinazoweza kupita huko maana ni nadra kuziona
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji3] [emoji2] [emoji1]
 
Wakuu naomba kuuliza,kuna kile chombo huwa kinapita juu kabisa ya anga inaacha moshi nyuma,tukiwa wadogo tuliambiwa ni rocket.kwa hapa africa inatua south africa na egypt tu.ss tumekua najua rocket ni ile iendayo nje ya dunia.naomba kujuzwa wakuu ni ni nini ile?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…