Kwanini ndizi mshare hazipatikani Kanda ya Ziwa?

Kwanini ndizi mshare hazipatikani Kanda ya Ziwa?

Mwanza, Shinyanga, Kahama, Geita, Kagera, na Kigoma! Kote huko sijawahi kukutana na ndizi mshare. Ndizi zinazopikwa maeneo tajwa ni ndizi ambazo kwa Arusha na Kilimanjaro, ukikuta mtu kazipika, ujue ni amekosa kabisa cha kupika. Si matumizi yake.

Nilikula ndizi kwa mara ya kwanza jijini Mwanza mwaka 2010. Nilishangaa nilipokuta ni ndizi ambazo kwa Arusha na Kilimanjaro zinatumika kwa kupikia mtori au kuvundikwa kwa ajili ya kutengenezea pombe. Nilikula kwa kuwa sikuwa na namna, isitoshe, nilikuwa ugenini na ziliandaliwa kwa ajili yangu.

Tokea nikiwa mdogo, nilikuwa nikijua kuwa ndizi zinazotumika kupikia "ndizi" ni NDIZI MSHARE, KIMALINDI, n.k., lakini si ndizi ng'ombe.

Ni kwa nini hizo ndizi hazipatikani Kanda ya Ziwa?
Sisi hio mshale ukikuta mtu kapika ni unashangaa kama wewe ulivyoshangaa ndizo bukoba. Mimi mara ya kwanza ndizi mshale nilikula dsm na nikashangaa hii ndizi au mhogo au hazikupkwa zikaiva. Ila sasa nimezizoea hasa iwe kwenye mchemsho
 
Nimezaliwa kanda ya ziwa,, naishi kanda ya ziwa na huenda nitafia kanda ya ziwa ama kuzikwa ziwani kabisa,, ngoja niseme ukweli wangu ndizi kama ndizi ni chakula rasmi kwa watu wa Kagera tu, huku Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Kahama, Musoma ni kitafunwa cha asubuhi kwa chai ama supu, huwa nawashangaa sana jamaa zangu wa kichaga kazini eti wanashindia ndizi,,
Ndizi zinapikwa na nyama au maharage. Uchagani wanapika na nyama nyingi. Tatizo lako ni kuwa bado unaishi yale maisha ya kimaskini ya kula ugali mwingi na mboga kidogo. Umewahi kusafiri kwenda majuu? Mara nyingi wanapotaja vyakula kwenye menu huanza na eg Kuku, Ng'ombe etc ndiyo wanataja side dish. Yaani kwenye chakula kinachozingatiwa ni ile main dish.
 
Kama anavyoshangaa ndivyo nami nilishangaa Kilimanjaro wanavyokula ndizi ngumuuu eti hadi za kukaanga ndio hizohizo🙆🙆🙆
Unakula ndizi zinabaki zimesimama tumboni!! Halafu hazina hata ladha.
Ndizi mshare ni laini. Inategemea tu na mazingira iliyostawishwa. Ukiweka mbolea na maji kwa wingi zinakuwa laini.
 
Sisi hio mshale ukikuta mtu kapika ni unashangaa kama wewe ulivyoshangaa ndizo bukoba. Mimi mara ya kwanza ndizi mshale nilikula dsm na nikashangaa hii ndizi au mhogo au hazikupkwa zikaiva. Ila sasa nimezizoea hasa iwe kwenye mchemsho
Ni mazoea tu. Hata Kilimanjaro siku hizi wanakula hizo ndizi Bukoba japo siyo sana. Zamani ilikuwa ni kama hakuna walaji. Kitu kingine ni kuwa wahaya wanapenda vitu bokoboko sana. Ni kama asili yao. Kwa upande mwingine wachaga wanakula vitu vigumu. Nyama hata iwe ngumu namna gani mchaga hashindwi kula.
 
Sisi hio mshale ukikuta mtu kapika ni unashangaa kama wewe ulivyoshangaa ndizo bukoba. Mimi mara ya kwanza ndizi mshale nilikula dsm na nikashangaa hii ndizi au mhogo au hazikupkwa zikaiva. Ila sasa nimezizoea hasa iwe kwenye mchemsho
Mshale❎
Mshare✅
 
Tembea uone.

Mimi mpaka leo nashangaa hao wa rugaruga wana kula je hizo ndizi ngumu kama miogo, mwanzoni ni lidhani na kwa ajili ya walevi kukatia hungerover zao za pombe, mpaka nilivo ona mama mjamzito naye anazila ndo ni kajifunza kwamba.

Hujafa hujaumbika
Ww mlughalugha wacha kujistukia 😅
 
Haya matoke mshare mnayependeaga nn madude magumu Kama nn.ndizi bukoba is the best hata kibogoyo anakula vzuri tu.kula ndizi Kama lunch au dinner ni dalili namba moja kuu ya umaskini.Over
 
Back
Top Bottom