Kwanini ndugu zetu wazaramu wanawapa watoto majina fikirishi?

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
14,311
Reaction score
36,056
Amani iwe nanyi

Wakati tunakua, bado Dar es Salaam ilikua na wazaramu wengi na nilibahatika kusoma na watu wenye majina kama SIKITU, SIWATU, SIWAZURI, TABU, MATESO, HAVINITISHI, SIKUDHANI, KIDAWA, CHAUREMBO na majina mengi ya namna hiyo.

Sasa, sijui hekima ya wazee wa kizaramo ilikua ina kusudia nini?

Wakati mwingine, though it is a myth, jina linaweza kubeba au kusadifu aina ya maisha ya huyo mtoto baadae.

Watalaamu embu dadavueni
 
Haya ndio majina halisi ya mwafrica ambayo kawaida wanapewa kulingana na mazingira, siyo mtu unabeba majina ya kiarabu, kizungu....nawapongeza kulinda mila na tamaduni zetu
 
Majina ya wazaramu Yana message ...
Mara nyingi yalikuwa Yana define watu walivyo hasa ukweni ..
Binti akiolewa jinsi atakavyo pokelewa ukweni ndo atakavyo toa majina Kwa watoto wake....Sikudhani...manake hakudhani Hali iko kama alivyoikuta huko ukweni ..Siwatu...manake familia ya mume sio watu...labda wanamtesa...Sikitu manake hakuna shida atavumilia Tu n.k n.k Siwazuri...,Mateso n.k mostly huwa ni mama alieolewa ana define wakwe au majirani.....wazaramo wenyewe wanajua
 
Amani iwe nanyi

Wakati tunakua, bado Dar es Salaam ilikua na wazaramu wengi na nilibahatika kusoma na watu wenye majina kama SIKITU, SIWATU, SIWAZURI, TABU, MATESO, HAVINITISHI, SIKUDHANI, KIDAWA, CHAUREMBO na majina mengi ya namna hiyo.

Sasa, sijui hekima ya wazee wa kizaramo ilikua ina kusudia nini?

Wakati mwingine, though it is a myth, jina linaweza kubeba au kusadifu aina ya maisha ya huyo mtoto baadae.

Watalaamu embu dadavueni
Akina sinaubaya, havijawa, bahati, ...
Ni vile tu wao wanatumia kiswahili. Wengine wanatumia zaidi ya 'kilugha'

Japo ukienda usukumani wapo akina cherehani, bakuli, sahani, majaba, nk
 
Majina ya wazaramu Yana message ...
Mara nyingi yalikuwa Yana define watu walivyo hasa ukweni ..
Binti akiolewa jinsi atakavyo pokelewa ukweni ndo atakavyo toa majina Kwa watoto wake....Sikudhani...manake hakudhani Hali iko kama alivyoikuta huko ukweni ..Siwatu...manake familia ya mume sio watu...labda wanamtesa...Sikitu manake hakuna shida atavumilia Tu n.k n.k Siwazuri...,Mateso n.k mostly huwa ni mama alieolewa ana define wakwe au majirani.....wazaramo wenyewe wanajua
Ni fikirishi sana, nadhani hawawazi madhara yake kwa huyo mtoto, mfano ukimwita SHIDA mtoto si anaweza pigika maisha yake yote?
 
Wapo akina sinaubaya, chaurembo, bahati....
Ni vile tu wao wanatumia kiswahili. Wengine wanatumia zaidi ya 'kilugha'

Japo ukienda usukumani wapo akina cherehani, bakuli, sahani, majaba, nk
Wasukuma wanatisha!
 
Back
Top Bottom