Kwa sisi waisilamu na mayahudi Kuna kitu kinaitwa Dhabiha na Shechita hii ni njia ya kawaida ya kuchinja na kuacha damu imwagike.
Baadae Nchi za magharibi zikaanzisha hio njia ya kustun kwamba ili mnyama asipate maumivu anapigwa shoti Kisha anachinjwa.
Ila tafiti mbalimbali za kisayansi zilizofanywa ni kwamba mnyama anapata maivu makubwa akiwa stunned kuliko akichinjwa kawaida.
Utafiti huu umefanywa na Professor Wilhelm Schulze wa Chuo kikuu Cha Ujerumani, Na hata 2008 waziri wa Chakula wa Ufaransa kwenye report yake uchijani wa kawaida ilikuwa ni WA kibinadamu zaidi kuliko ku stun.
Utafiti mwengine wa Dr. Karuna Chaturvedi ulionesha Nyama ya kuchinja kawaida ni nzuri kuliko ya kustun ki afya sababu mnyama anapochinjwa kawaida bado moyo una pump damu, sababu pale anapochinjwa Pana mshipa mkubwa basi inamwagika damu nyingi hivyo damu inatoka na sumu sumu na micro organism wengine.
Pia utafiti wa Dr modi huko India Nyama ya kuchinja kawaida inakuwa ni soft na tamu zaidi, Ina PH chini ya 7 (wingi wa acid) sababu mnyama hapati shida sana anapokufa tofauti na ile ya kustun ambayo Ina acid ya kutosha.
Hivyo mkuu kama unataka kuishi Kwa afya mnyama akichinjwa kawaida ni vizuri zaidi kidini na kisayansi. Kama unataka magonjwa ya ajabu ajabu tafuta means za kumchinja mnyama bila damu kumwagika.