Kwanini ng’ombe wasipigwe nusu kaputi kabla ya kuchinjwa?

Kwanini ng’ombe wasipigwe nusu kaputi kabla ya kuchinjwa?

Msiwasahau kuku kwenye mjadala huu.
Wanachinjwa kwa wingi na kikatili. Angalau ng'ombe anaveshwa hadi hereni.
 
Hivi what if mtu ukifa unazaliwa tena kiumbe kingine, mfano unazaliwa ng’ombe? Incase ni hivyo, si ingependeza kama kabla ya kuchinjwa upigwe kwanza nusu kaputi, au nakosea?
Naona umedandia kitu ambacho hukifahamu! Ulishawahi kwenda kwenye machinjio yoyote ya kisasa? Kuna kitu kinaitwa stunning gun, hiki ni mfano wa pistol yenye bolt ambayo hufyatuliwa na Baruti lakini pia inaweza kuwa ya kufyatua na umeme. Bolt hiyi hutumia kumfanya mnyama awe unconscious, yaani anapoteza fahamu. Hapo ndipo huchinjwa pasipo maumivu yoyote! Na kuna sehemu ya kulenga hiyo bolt ili mnyama atakapopigwa azimie. Kitaalam tunaita Humane slaughter!!
 
Changamoto ni "wash out period" yani muda ambao dawa itaishi kwenye mwili wa ng'ombe kabla ya kutoka nje kupitia mkojo au njia zingine.

Inapaswa ng'ombe alie kwenye tiba akae walau siku 14-28( kutegemea na dawa) ndipo achinjwe, ili kiruhusu dawa hiyo itoke nje ya mwili na kuepuka madhara kwa mtumiaji

Ndio maana hatutumii nusu kaputi kabla ya kuchinja wanyama hawa
Hili jamaa yetu halijui! Ndiyo shida ya mtu wa maendeleo ya jamii kutoa ushauri kwenye sekta za kitaalam!
 
Naona umedandia kitu ambacho hukifahamu! Ulishawahi kwenda kwenye machinjio yoyote ya kisasa? Kuna kitu kinaitwa stunning gun, hiki ni mfano wa pistol yenye bolt ambayo hufyatuliwa na Baruti lakini pia inaweza kuwa ya kufyatua na umeme. Bolt hiyi hutumia kumfanya mnyama awe unconscious, yaani anapoteza fahamu. Hapo ndipo huchinjwa pasipo maumivu yoyote! Na kuna sehemu ya kulenga hiyo bolt ili mnyama atakapopigwa azimie. Kitaalam tunaita Humane slaughter!!
Safi sana
 
Kama ni hivyo, apigwe risasi ya kichwa, then ile akipoteza fahamu tu, achinjwe papo hapo.., tafiti ziendelee, vyovyote iwavyo, si vyema kwa sisi viumbe tuliopewa ufahamu (intelligence) kuendelea kutesa viumbe wengine namna hii wakati tunaweza kufanya tafiti na kuwapa unafuu. Ila hiyo ‘Bolt stunning’ bado naamini ni nzuri, maana ubongo unachomwa na kitu chenye ncha kali, hivyo lazima apoteze fahamu
Hatakiwi kupoteza fahamu that's the point, na kuchinja kawaida hapati maumivu kama kupiga risasi.
 
Kwa sisi waisilamu na mayahudi Kuna kitu kinaitwa Dhabiha na Shechita hii ni njia ya kawaida ya kuchinja na kuacha damu imwagike.

Baadae Nchi za magharibi zikaanzisha hio njia ya kustun kwamba ili mnyama asipate maumivu anapigwa shoti Kisha anachinjwa.

Ila tafiti mbalimbali za kisayansi zilizofanywa ni kwamba mnyama anapata maivu makubwa akiwa stunned kuliko akichinjwa kawaida.

Utafiti huu umefanywa na Professor Wilhelm Schulze wa Chuo kikuu Cha Ujerumani, Na hata 2008 waziri wa Chakula wa Ufaransa kwenye report yake uchijani wa kawaida ilikuwa ni WA kibinadamu zaidi kuliko ku stun.

Utafiti mwengine wa Dr. Karuna Chaturvedi ulionesha Nyama ya kuchinja kawaida ni nzuri kuliko ya kustun ki afya sababu mnyama anapochinjwa kawaida bado moyo una pump damu, sababu pale anapochinjwa Pana mshipa mkubwa basi inamwagika damu nyingi hivyo damu inatoka na sumu sumu na micro organism wengine.

Pia utafiti wa Dr modi huko India Nyama ya kuchinja kawaida inakuwa ni soft na tamu zaidi, Ina PH chini ya 7 (wingi wa acid) sababu mnyama hapati shida sana anapokufa tofauti na ile ya kustun ambayo Ina acid ya kutosha.

Hivyo mkuu kama unataka kuishi Kwa afya mnyama akichinjwa kawaida ni vizuri zaidi kidini na kisayansi. Kama unataka magonjwa ya ajabu ajabu tafuta means za kumchinja mnyama bila damu kumwagika.
Stunning mnyama anakuwa unconscious..ila akichinjwa damu yote ina mwagika tembelea machinjio ya kisasa kama dodoma ama arusha uone inavyofanyika.

Acha kupotosha watu..

Hiyo ya kusema anapata maumivu sana hujatolea ufafanuzi..ila kisayansi kiumbe kilicho nusu kaputi kinapataje maumivu?

Acha illusion zako za kidini hili ndio tatizo la wafia dini.
Sikatai ni mawazo yako ila in modern world mambo hayaendi kwa hisia bali kwa tafiti..na stunning ilifanyiwa tafiti hadi kuwa recommend way ya kumuua mnyama bila maumivu.

Na hii husaidia sana damu nyingi kutoka kwenye nyama ili kuogeza quality ya nyama.
Kasome articles mbalimbali zinaelezea hili kwa undani acha kuleta illusions.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hatakiwi kupoteza fahamu that's the point, na kuchinja kawaida hapati maumivu kama kupiga risasi.
Unazijua aina za stunning ama unaongea tu..kasome kitu kinaitwa captive bolt..kuna kutumia gas stunning..electrical stunning n.k

Kajielimishe itakusaidia zaidi kuliko kuishi kwa hisia.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mboresho kwenye uchivaji nadhani yavenze na walaji wakatae then iletwe stuming hiyo ilakuwa powa wana,yaani kuchimba kawaida ng'ombe ni ukavili kweli yani...that why mimi sipendi nyama kebisa
 
Stunning mnyama anakuwa unconscious..ila akichinjwa damu yote ina mwagika tembelea machinjio ya kisasa kama dodoma ama arusha uone inavyofanyika.

Acha kupotosha watu..

Hiyo ya kusema anapata maumivu sana hujatolea ufafanuzi..ila kisayansi kiumbe kilicho nusu kaputi kinapataje maumivu?

Acha illusion zako za kidini hili ndio tatizo la wafia dini.
Sikatai ni mawazo yako ila in modern world mambo hayaendi kwa hisia bali kwa tafiti..na stunning ilifanyiwa tafiti hadi kuwa recommend way ya kumuua mnyama bila maumivu.

Na hii husaidia sana damu nyingi kutoka kwenye nyama ili kuogeza quality ya nyama.
Kasome articles mbalimbali zinaelezea hili kwa undani acha kuleta illusions.

#MaendeleoHayanaChama
Safi sana, tunataka hoja kama hivi, sio hisia za mtu
 
Kwanza hatupaswi kuwachinja. Sisi ni wauaji
Usipoua basi unakufa ww, haiwezekani species zote tukaishi bila kuuana, Nadhani system ya maisha hairuhusu hili. Lazima uue ili uishi na kuna siku utauwawa ili kiumbe kingine kiishi. Inawezekana hakuna kitu kinaitwa natural death bali kuna viumbe vingine ambavyo huvioni kwa macho ya kawaida vinauvamia mwili wako na kuua either kwa magonjwa, uzee n.k Hapo kaburini ww ni chakula kizuri sana kwa viumbe wengine. Hadi fuvu lako ni msosi.

Mfano: Ukiachia mbali kuua ng'ombe Mwili wako kupitia seli zinazokuumba unaua seli, virus na bakteria kila wakati ili uendelee kuwa hai na ukiacha huo mchezo basi zenyewe zinakufa na zikifa ndo ww hivyo.

Huenda MUNGU aliumba pumzi akaipa makazi duniani na ikajigawanya katika vyanzo vya maumbile tofauti matrilioni yaliyopo humu duniani. Huenda pumzi ya uhai ni ile ile ila miili ndo tofauti na ikitoka kwenye umbile lako inaenda kwenye umbile jingine, huwezi kukumbuka sababu kumbukumbu ni sehemu ya mwili kupitia ubongo sio pumzi na ukifa ubongo nao unakufa. HUENDA LAKINI.
.
 
Back
Top Bottom