Kwanini Nguvu kubwa inatumika kuonesha Rais Samia hafanyi vibaya?

Muheshimiwa, me nadhani ungeainisha mambo aliyoyafanya Magufuli yanayoonekana na mambo aliyoyafanya SSH mpaka sasa ndo hapo tuone kama kweli inatumika nguvu zaidi ya uhalisia.

Ukishindwa kuainisha basi utakua na agenda yako tu binafsi.
 
Kuna watu wanaojiita chawa wa mama walizindua kampeni yao, huenda ndo majukumu yao hayo kutangaza jinsi mama anavyoupiga mwingi.
 
Yeye mwenyewe anajua hakuna anachofanya zaidi ya kuzunguka zunguka basi
 
🐒🐒🐒
Your browser is not able to display this video.
 
Hakuna nguvu yoyote inayotumika, ni ukweli bayana kuwa mama Samia anafanya vizuri.
 
Hakuna wakati katika nchi hii nguvu kubwa ilitumika kumtangaza JPM kuwa anafanya mazuri kwa nchi kama awamu ya tano. Kumbe ilikuwa ni kinyume chake. Sasa mama naye anavurunda na nguvu kubwa imeanza kutumika kumpamba. Wapinzani kaeni chanjo.
 
Inaonekana we mfuatiliaji mzuri wa utendaji kazi wa Rais Samia Suluhu hakuna nguvu kubwa inayotumika lakini kinachotokea ni kwamba Mama anafanya sana yani kila siku tunapata updat ya kitu kipya alichokifanya ndani ya miaka miwili amefanya kazi kubwa ambazo zilitakiwa kufanywa kwa miaka 4 au 5 lakini yeye amefanya ndani ya miaka 2 Watanzania tumshukuru sana Mungu ametupa kiongozi Mchapakazi
 
Unataka aanze ukatili wa kutekana na kuokota maiti kwenye viroba ndio muone anachapa kazi
 
Nashukuru jana timu yetu ya taifa imefungwa maana nalenyewe lingeandikiwa bango barabarani, Sasahivi hivi Barabara ya Bagamoyo kutoka Mwenge hadi tegeta kumejaa mabango ya kusifu Samia utafikiri niwakati wa kampeini,sijajua 2025 itakuwaje,akuna haja ya mabango wananchi tuna macho tunaona,akuna haja ya kuharibu fedha ya Serikali kulipia mabango wakati Sisi wananchi tunayo macho.
 
Na ni kwanini unatumia nguvu kubwa sana kuonesha kuwa hafanyi vizuri? Jibu swali hili kwanza.
 
Ata jiwe ilitumika nguvu kubwa kumtangaza ilo mwisho wa siku wote ni ccm na ndio chanzo cha masumbuko na wizi katika taifa ili
 
Si kiongozi mzuri,ripoti ya CAG imeonyesha,ndio maana nguvu kubwa inatumika.Chema chajiuza,kibaya chajitangaza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…