Kwanini nyumba nyingi za Dar zinauzwa na Benki?

Hyrax

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2023
Posts
1,458
Reaction score
4,409
Nimefanya utafiti kupitia ukurasa wa Dsm Brokers (Instagram) mpaka sasa nimegundua nyumba nyingi za dar zinauzwa na benki kwasababu ya madeni sasa sijui tatizo ni nini ikiwa mkoa wa dar unasifika kuwa kitovu kikuu cha fursa za kifedha na biashara,

Katika utafiti wangu kupitia ukurasa wa hao jamaa kati ya nyumba 50 atakazopost Dsm Brokers nyumba 30 mpaka 35 zote zinauzwa na benki sehemu inayobaki unakuta jamaa wamendika nyumba inauzwa Binafsi.

Wadau tatizo nini juu ya nyumba nyingi kuuzwa na benki kwasababu ya madeni ni kwamba mkoa ni mgumu au matumizi yamezidi kipato?
 
Changamoto za maisha hizi. Mkopo una raha yake kama utaupatia. Mkopo ukikupatia matokeo yake ndio kama hayo ya mali zako kuanza kuuzwa na wadeni wako.
 
Nimefanya utafiti kupitia ukurasa wa Dsm Brokers (Instagram) mpaka sasa nimegundua nyumba nyingi za dar zinauzwa na benki kwasababu ya madeni sasa sijui tatizo ni nini ikiwa mkoa wa dar unasifika kuwa kitovu kikuu cha fursa za kifedha na biashara,

Katika utafiti wangu kupitia ukurasa wa hao jamaa kati ya nyumba 50 atakazopost Dsm Brokers nyumba 30 mpaka 35 zote zinauzwa na benki sehemu inayobaki unakuta jamaa wamendika nyumba inauzwa Binafsi.

Wadau tatizo nini juu ya nyumba nyingi kuuzwa na benki kwasababu ya madeni ni kwamba mkoa ni mgumu au matumizi yamezidi kipato?
Mkuu mjini unatakiwa uje na akili tu tabia utazikuta hukuhuku na waliosema mjini mipango wala hawakukosea.
Watu wanajenga nyumba mfuko mmoja wa sementi tofali 70 ila inapigwa finishing iliyoenda skonga kisha wanaenda kuichukulia mkopo bank.
Nyumba inajengwa kwa milioni 15 watu wanavuta mkopo wa milioni 100 wanamtia Milioni 5 afisa mikopo ili aharakishe mchakato kabla mvua hazijaja zikaondoka na chokaa yote.
Wakishavuta mkopo wanalipa miezi mitatu halafu jamaa anajifanya kafulia kama vipi mjengo upigwe mnada.
Msala unabaki kwa bank na watu wa bima
 
Hatari hiyo jamani
 
Hv nikichukulia mkopo nyumba kwa thamani ya Mil 50 wakati thamani halisi ya nyumba ni Mil 30 kisha nikapita hiv, benki si ndio wanapata hasara ya Mil 20 au?
Mifumo ya mikopo ya bank,
Mara nyingi ni kwamba, uwe na chanzo cha pesa cha kupata marejesho. Chanzo hicho kiwe nkinajitosheleza kupata thamani ya rejesho kulingana na muda mlioahidiana. Kwa mfano, biashara, turn-over itoshe ku retain mtaji, faida na rejesho.
Na pia kuwe na Collateral kama nyumba au asset isiyohamishika ambayo itakuja kutumika kurejesha pesa kama mkopaji akishindwa kulipa. Na Collateral hiyo inafanyiwa tathmini na wataalam wa masoko na brokers waliobobea.
Pia, kila mkopo unaotolewa huwa unakatiwa Bima. Ila makampuni ya bima, huwa yana withdraw claim nyingi sana yakigundua kuwa mkopaji amekwepa au pengine, pesa ya mkopo hakuipeleka kwenye lengo aliloiombea.

Hope that helps
 
Nimefanya utafiti kupitia ukurasa wa Dsm Brokers (Instagram) mpaka sasa nimegundua nyumba nyingi za dar zinauzwa na benki kwasababu ya madeni sasa sijui tatizo ni nini ikiwa mkoa wa dar unasifika kuwa kitovu kikuu cha fursa za kifedha na biashara,

Katika utafiti wangu kupitia ukurasa wa hao jamaa kati ya nyumba 50 atakazopost Dsm Brokers nyumba 30 mpaka 35 zote zinauzwa na benki sehemu inayobaki unakuta jamaa wamendika nyumba inauzwa Binafsi.

Wadau tatizo nini juu ya nyumba nyingi kuuzwa na benki kwasababu ya madeni ni kwamba mkoa ni mgumu au matumizi yamezidi kipato?
Mikoani pia nyumba nyingi.zinauzwa na mabenk ila gari zinapita kutangaza.Kutokana na mikoani hakuna mishe mishe na foleni za magari
 
Mifumo ya mikopo ya bank,
Mara nyingi ni kwamba, uwe na chanzo cha pesa cha kupata marejesho. Chanzo hicho kiwe nkinajitosheleza kupata thamani ya rejesho kulingana na muda mlioahidiana. Kwa mfano, biashara, turn-over itoshe ku retain mtaji, faida na rejesho.
Na pia kuwe na Collateral kama nyumba au asset isiyohamishika ambayo itakuja kutumika kurejesha pesa kama mkopaji akishindwa kulipa. Na Collateral hiyo inafanyiwa tathmini na wataalam wa masoko na brokers waliobobea.
Pia, kila mkopo unaotolewa huwa unakatiwa Bima. Ila makampuni ya bima, huwa yana withdraw claim nyingi sana yakigundua kuwa mkopaji amekwepa au pengine, pesa ya mkopo hakuipeleka kwenye lengo aliloiombea.

Hope that helps
Sawa nimeelewa vizuri sana maelezo.
Pia kuna wale ambao husema kuwa wamewaingiza benki hasara kwa kuwapa nyumba au kiwanja kisicho na thamani sawa na mkopo.
Hii imekaaje?
 
Back
Top Bottom