Kwanini nyumba nyingi za Dar zinauzwa na Benki?

Halafu mtu hapo juu anakuambia bank sio wajinga
Matajiri wanachukua mikopo hata zaidi ya 2b kwa mashamba yasioendelezwa pori tupu
Wengine wafanyakazi wa bank ndio wanawasaidia mbinu za kupata mikopo hao hao wenye nyumba za udongo 😄 poa
Shida vijana wamekaririshwa na formality, hawajui nguvu ya coin kwenye ku unlock hizo formality.
 
Mifumo ya bank imeweka kupata faida na sio hasara.
Biashara ni betting wengi ukopa kwa matumaini ya kutoboa kutoboa kwa mkopo bila kuwa vizuri kiroho na kimwili sahau.
Maana biashara ni game win or loose.
Thus kwa mafundisho ya dini zote riba ni haramu
 
Ok,
Kwa hiyo yenyewe haitolewi kwa ajili ya kuanza ujenzi? Ni kwa kumalizia tu...Vipi mtu akitaka mkopo wa kuanza ujenzi?
 
Hupewi mkopo bila ya benki kutuma mtu wao wakufanya tathmini ya mkopo unaokopa na kitu unachokiwekea dhamana benki sio wajinga mkuuu
Kuna wafanya kazi wa bank wanaokiuka miiko yao ya kazi, kwa kushirikiana na wateja hupandisha thamani ya mali husika, ili mteja apewe kiwango kikubwa cha pesa na wao wakipata % kadhaa
C.c Nusratt
 
Mzunguko wa biashara Dar umebadilika sana,wafanyabiashara wanakuwa wengi kuliko wanunuzi.Pia mchina kashikilia soko kitu cha sh 2000 yeye anauza sh 1500.Sasa ukute umejaza store mzi sh mil 50.Hapo lazima ulie .Pia mzunguko wa Dar kwa sasa unaathiriwa na wenye mitaji mikubwa wao wakiuza kwa faida ndogo wanaendelea vizuri.Sasa wewe wa mkopo wa %18 utapataje faida na kulipa!!?
 
Labda inflation
 
Labda inflation au Wana overestimates
 
Labda inflation au Wana oberestimates
 
Shida vijana wamekaririshwa na formality, hawajui nguvu ya coin kwenye ku unlock hizo formality.
Mkuu, kila sehemu wapo wataalam wa ku-manipulate mifumo siku zote wapo.

Hata Black Sniper anavorejea kauli yangu ameelewa nilichokizungumza.

Kila mifumo yenye vigezo na masharti, kuna wataalamu wanaopita neno kwa neno kutafuta udhaifu wapite na fursa.

Bank ni kweli siku zote huwa inatoa mifumo secure sana kwenye mambo ya mikopo ila watu huwa wanatafuta njia ya kuwanyoosha, either wateja au bank yenyewe. Ndio maana kwa wafuatiliaji wanaelewa jindi hata serikali ilivogundua upigaji kwenye mifumo ya mikopo ya wafanyakazi wa serikali (Government Salaried Workers) mpaka Serikali ikatengeneza mfumo unaitwa ESS.

Pia upigaji mwingi unatokea iwapo Credit Committee imepokea Rushwa... Ambapo ni Afisa mikopo, Manager wa Bank ambaye ni Checker, na Third part Valuation Officer
 
Asante kwa kuwaelewesha hili, wengine wanadhani wafanyakazi wa Bank ni waadilifu.
Hawa nawajua vizuri sana tena acha hizo kubwa hata elfu 10 wanakuobia wakati wa hesabu

Ukiwapa hela nyingi lazina waangushe 10 kwa njaa walizonazo itakuwa mkopo wa fifty au 100m?
 
Upo vzr,ila sasa mambo yote ni digital,luchezesha ni Kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…