Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.
Sio kila siku tunapaswa kuandika, kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya kizungu kama Cold War, jeshi na ujasusi wa KGB, CIA na Mossad. Leo ngoja tujadili kidogo masuala ya kimaisha katika jamii zetu hizi tunamoishi.
Ndugu zangu watanzania jifunzeni kujishusha lakini isiwe too much. Mungu hapendi mjishushe sana. Having too much humility is self destructive;
Unakuta mtu alikuwa anaishi katika nyumba ya kupanga vyumba viwili chumba na sebule, lakini kwa bahati nzuri akajinyima kisha kwa uwezo wa Mungu akajenga nyumba yake self-contained ya vyumba vitatu vya kulala.
Siku ama weeks kadhaa baada ya kuhamia unasema ngoja niende nikamtembelee ndugu, jamaa au rafiki yangu nifahamu anapokaa. Baada ya kufika na kusalimiana anakukaribisha ndani kisha anakwambia "karibu, haka ndio kakibanda kangu najifichamo na kafamilia kangu, si unajua tena ujenzi wa kimasikini"
Kwanini nyumba yako nzuri Mungu aliyokubariki uiite kakibanda? Au baadhi ya watu wanafikiri huko ndio kujishusha kwenyewe na ndio uungwana? Why don't you feel proud of what God blessed you with? Au haujui kuwa hata vinyonge havitaenda Mbinguni. Mtu amekuja kukutembelea mwambie kwa kujiamini kwamba, "hii ndio nyumba yangu. Nimeijenga mpaka stage hii ila Mungu akinijalia nitaimalizia taratibu tarabitu kwa maana pesa ngumu siku hizi"
Au unakutana na dada classmate wako wa secondary school na ulisikia aliolewa punde tu baada ya kumaliza shule. Unamuuliza "hongera Fatuma ninasikia uliolewa na fulani na umebarikiwa mtoto mmoja" utamsikia atakavyokujibu kwa kinyonge "kuolewa wapi kaka yangu, nipo tu ninasogeza naye maisha, si unajua tena mambo ya sogea tukae"
A thankful heart is one that is grateful and appreciative of who God is and the life He has given them despite the storms of life. I have learned that cultivating a thankful heart is a choice and it requires our intentional effort in achieving it.
Having too much humility is self destructive. Humility has to be practiced with care. Humility requires boundaries.
Watanzania msipende kujiweka kinyongenyonge na kujishusha saana. Jivunie kile ambacho Mungu amekubariki kwa wakati huo huku ukizidi kupambana ili usonge mbele zaidi.
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.