Kwanini nyumba yako unaiita "kakibanda kangu"? Mungu hapendi kujishusha sana. Having too much humility is self destructive

Kuna siku nilikuwa kwenye ibada za Hawa manabii wa kizazi kipya,kwenye maombi nabii akawa akisema"Mungu baba, sisi ni Kama sisimizi,ni wadudu tu mbele zako"nikapoteza network nikakumbuka tuliambiwa tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, Sasa kwa Nini hata tusiseme "Mimi ni pendo,Mimi ni nuru kwa kuwa nimeumbwa kwa mfano wako"nikawaza hata kujishushusha kuwe na kiasi,kujishushusha Sana mwishowe utakufuru.Moyo wenye shukrani humpendeza Mungu na Jamii yake.
Hakika friend. Upo sahihi. Tujifunze kushukuru katika kila hali.
 
Tatzo ni shiriki,wengi wana wahofia wachawi,wanaona wakisema huu mjengo wangu, wanahisi watarogwa kabisa wapotee wasifaidi Kukaa mjengoni,kwa hofu hyo wanasema kakibanda ili wabakie salama machoni pa wa wanafiki na wachawi.
 
Ukiona mtu anajishusha hivyo tofauti na uhalisia uliopo hapo ujue shida ni wewe mgeni,huaminiki,mzee wa kuzogoa,ndimi mbili na kadhalika.

Tena ukija kwangu sikwambii ni kakibanda bali ni kakijibanda alafu utajua mwenyewe.
 
Kuna mwamba alikuwa anajimwambafai sana amejenga nyumba ya nguvu siku amenipeleka kwake nilichoka sana banda fulani tu nahisi mchora ramani alikuwa kalewa na fundi alikuwa mzee wa miaka 80,finishing zero,nikabaki nashangaa tu!
Note;Acha watu wakusifie kwa ulichofanya sio wewe mwenyewe
 
Mungu hapendi kujishusha sana.
1. Unapoongelea Mungu ni bora ukatoa na nukuu wapi kasema hivo

2. Litazame pia kwa namna hii, Kichwa cha mtu hutoa tathmini kutokana ya kitu/hali kutegemea yale anayoyajua/aliyoyapanga. Mfano kama lengo/mpango wake ni kumiliki bonge la Mansion, mtu hyo hawez kujisifia kwa kuwa na cottage. Kwa namna jingine inawezekana msikilizaji ndo ukaona ni nyumba ya maana kwako ila kwake kutegemea na malengo yake akaona bado sana. Sio kujishusha mara zote, ni kukubaliana na hali alipo akitambua anapopaswa kufika
 
Ka Uzi kako kamejaa hekima ndo mana na Mm nimeweka ka post kangu
 
Uzi mzuri sana,ila hapo mwisho ulipo andika USISAHAU:....ingependeza pale mwishoni baada ya neno IPASAYO ungemalizia na CHAGUA MAGUFULI...
 
Hahahaha duh....this is an excellent piece...
 
Infantry soldier hongera. Unatupa nondo kwelikweli siku . Big up unatupa mada tofauti za kufikirisha na kuelimisha Ahsante kwa nguvu chanya unayotupa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…