Kwanini nyumba yako unaiita "kakibanda kangu"? Mungu hapendi kujishusha sana. Having too much humility is self destructive

Kwanini nyumba yako unaiita "kakibanda kangu"? Mungu hapendi kujishusha sana. Having too much humility is self destructive

Umesema kweli lastborn, shemejio siku moja katika stories akazungumzia maendeleo ya ujenzi wa nyumba yake mbezi, lakini hakuiita nyumba namnukuu;,"kakibanda kangu nilikojenga pale inabidi kabadilishwe maana wanaonizunguka wote wameweka nyumba za kisasa Sasa nimebaki katikati na pagale langu", hii lugha haikunifurahisha sana ila kwakuwa sikujua nikamute tu,,Sasa nilipokuja kuona kumbe kibanda chenyewe ni nyumba ya ghorofa 2 nilijisikia vibaya zaidi,, niliona kakosa shukrani kabisa,
 
Kuna watu wanaoishi vizuri na wanajiweza, lakini kuna wengine wapo tu kwa sababu walizaliwa. Kuna wenye nyumba na wanao miliki vibanda. Nadhani kila mtu anatakiwa kujitathimini kwa kuzingatia uhalisia.

Kibanda ni kibanda tu, hata ukiite ghorofa.
Ukilinganisha nyumba yangu na Kakobe yangu inabaki kuwa ni kibanda tu
 
Upo sahihi sana mkuu..yatupasa kushukuru kwa kila jambo,tuwe na mioyo iliyojaa shukrani mbele za Mungu. Tena mzaburi anatuambia "ATOAE DHABIHU YA KUNISHUKURU NDIE ANAENITUKUZA."Ukifanikiwa jambo lolote ukamtolea Mungu sadaka ukamwambia asante kwa kunifanikishia jambo flan hakika Mungu atakubariki na kukuongezea maradufu.Sio lazima tufanikiwe mambo makubwa sana ndipo tumshukuru hapana. Tukishukuru hata kwa mambo madogo madogo anayotujalia tunakua tumejiongezea nafasi ya kubarikiwa na kuongezewa zaidi.
 
Nilikuwa naita "nyumba yangu" kwa sababu ni nyumba ya kawaida tu, Ila wakati korona iliposhamiri Siku moja nikaamua kufanya matembezi ya kawaida tu kwa miguu ,kuzunguka Kama radius ya km 3 ebana nilikutana na mahekalu ya kutosha jirani kabisa na nilipo, kiukweli nyumba yetu haistahili hata kuwa Banda la kuku kwenye hizo mansions!!

Niliporudi home kiunyonge kabisa nikamwbia mke , next time ukiwaelekeza watu sema Kuna kibanda kipo so and so, sio nyumba maana nilikutana na nyumba fensi ina alluminium windows halafu imekula drewa paint , ni nyumba ya dogo tu ,Kama ndevu kunyoa labda aanze leo hii
 
Inawezekana anakuwa hajaridhika nayo kwa kusema hivyo.
Kutoka kupanga chumba na sebule mpaka kumiliki nyumba self-contained ya vyumba 3 vya kulala bado mtu anasema ni kakibanda huko ni kukosa shukrani
 
Nilikuwa naita "nyumba yangu" kwa sababu ni nyumba ya kawaida tu, Ila wakati korona iliposhamiri Siku moja nikaamua kufanya matembezi ya kawaida tu kwa miguu ,kuzunguka Kama radius ya km 3 ebana nilikutana na mahekalu ya kutosha jirani kabisa na nilipo, kiukweli nyumba yetu haistahili hata kuwa Banda la kuku kwenye hizo mansions!!
Okay...
 
Ni kweli kabisa...

Ndiyo maana kuna kabila fulani wanabezwa sana kwa kujikweza... Hapana ni wanaongea ukweli kwa nini ujishushe sana...

Cc: mahondaw
 
Niliporudi home kiunyonge kabisa nikamwbia mke , next time ukiwaelekeza watu sema Kuna kibanda kipo so and so, sio nyumba maana nilikutana na nyumba fensi ina alluminium windows halafu imekula drewa paint , ni nyumba ya dogo tu ,Kama ndevu kunyoa labda aanze leo hii
Sawa mkuu
 
Nyumba zote mtaa Fulani zimeezekwa kwa vigae ni yako tu mabati ya kuchoma macho wakati wa jua. Wenzako watakutania kibanda japo wewe unasema ni nyumba. Utabidi uende mtaa wa size yako.

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Wenzako watakutania kibanda japo wewe unasema ni nyumba. Utabidi uende mtaa wa size yako.
Wataalam wa "social psychology" wanashauri siku zote kuwa jaribu kukaa/kujenga na watu ambao haujatofautiana nao sana hali ya kiuchumi.

Kama wewe kipato chako kwa mwezi ni 3,000,000/= ukikaa na watu wanaoingiza 4,000,000/= au 2,000,000/= sio mbaya hapo utakuwa na amani sana.
 
Back
Top Bottom